Samsung wasipoiga design ya iphone 12 basi apple wamepunguza wafuasi

instagram

JF-Expert Member
May 27, 2014
2,091
4,715
Apple siku zote ndiyo wamekua wakitoa muongozo wa design za smartphones zote duniani kuanzia muonekano wa kasha hadi camera na kioo.

Sasa iphone wametoa toleo jipya la iphone 12 ambalo kimuonekano ni kama limerudi kwenye iphone 5 ya boksi boksi.

Sasa apple kwa mabadiliko haya ya shepu ya iphone tunategemea wafuasi wake wote samsung, tecno, xiaomi, mi, lg etc wataiga kwa matoleo yao yajayo.

Basi kama itatokea samsung na wafuasi wenzake wa apple hawataiga muonekano mpya wa apple basi tutachukulia kuwa nguvu ya ushawishi ya apple kwa wafuasi wake imepungua sana.

Ila nna uhakika muda si mrefu tutaone wafuasi wa apple akina samsung na wenzake watakuja na matoleo yao mapya yenye muonekano wa boksi kama wa iphone 12 as soon as possible.

IMG_5900.jpg

IMG_5899.jpg
 
Watoe simu ambayo sihitaji kuhofia kuishiwa charge.

Hivi hakuna nambn wakatumia mwanga kucharge simu? More or less kama baadhi ya calculators zilivyo.
 
Mi nasikia Samsung anamuuzia display apple na Sony au LG wanauza camera kumbe apple akishamaliza kununua hivi vitu anawafanya wenzake wafuasi wake? Tabia mbaya sana

Apple kanunua display kwa samsung za iphone x tu napo zilikua na quality kuliko hata za samsung oled lakn sahv ameamua kutoa za kwake super retina xdr
 
mleta uzi umepuyanga...
.
hao Apple ndo mabingwa wa kuiga miundo ya sim za wengine mfano mkubwa ni macho matatu waliiga kuoka kwa huawei mate 20 pro, ukiangalia mate 20pro imetoka 2018 afu iphone 11 imetok 2019.
.
pia kwa ishu ya tyle wa kioo waliga kwa huawei p20 bro. fanya uchunguzi kbla ya kuleta uzi...
 
Back
Top Bottom