Wadau,
Hii iacheni kwa muda kabla ya kuipeleka kwenye matangazo.
Kwa masikitiko makubwa nawajulisheni kifo cha Samson Kipepe ambaye alikuwa anafanya kazi umoja wa vijana wa CCM. Kifo kimetokea asubuhi hii pale hospitali ya Lugalo.
Aliwahi kugombea kuwa mwenyekiti wa vijana nafikiri wakati ule Nchimbi anagombea kwa mara ya kwanza. Mwaka 2005 aligombea ubunge wa Kyela pamoja na akina Dr. Mwakyembe na Mwakipesile.
Nilimpokea Kipepe Rungwe miaka ya 80 baada ya kuombwa na mamake ambaye wakati huo alikuwa ameolewa kijijini kwetu. Nilikuwa mentor wake kwa muda mpaka nilipomaliza Rungwe sec. School.
Baadaye nilionana na Kipepe nchini Sweden miaka ya 90 wakati tukiwa wanafunzi Ulaya. Wakati huo alikuwa anasoma Ukraine.
Alikuwa mchekeshaji mzuri sana na furaha kuwa naye karibu.
Alivyorudi TZ alijiunga na umoja wa vijana wa CCM kama mhasibu wao, kazi ambayo aliendelea nayo kwa muda mrefu.
Nawapa pole ndugu na marafiki wote wa marehemu kwa msiba huu. Ni pigo kubwa kwa watu wa Kyela maana alikuwa katika vijana ambao walikuwa wanajishughulisha na maendeleo ya wilaya yetu.