Samia tumaini jipya Tanzania: The Economist baada ya kumsakama sana Magufuli, sasa angalau lina matumaini na Samia, laanza naye vizuri

Marekani uionayo leo kwamba imeendelea sana imekua hivi tuionavyo leo kwasababu ya FED...bila FED isingekua hivi...

Lakini hapohapo kumbuka nilikwambia kwamba kuundwa kwa FED kulikua kinyume na katiba ya Marekani.Nadhani utakua unaelewa namaanisha nini hata kama uwezo wa ubongo wako ni mdogo.

Narudia,katiba ni maandishi tu,binadamu ndio mtendaji.
 
Katiba ni maandishi tu yaliyoandikwa na mwanadamu,maandishi hayana uwezo wa kutenda,atendaye ni binadamu....

Katiba ni upuuzi tu kama utampata kiongozi anayejielewa....maana atatenda kulingana na hali ilivyo kwa wakati huo....

Dini kama uislam na ukristo zina katiba zake ambazo ni quran na biblia...lakini leo hii watu wenye dini hizi ndio wanaofanya maovu kupindukia kuliko wasio na dini....

Je,haikuandikwa kwamba usizini? Je wewe hujawahi kuvunja katiba/yaani msahafu wako kwa kuzini?...hujawahi kutamani kisicho chako?...hujawahi kusema wongo?....huoni kama umevunja katiba yako kama muislam/mkristo?....sasa kama wana dini wanavunja katiba aliyoiweka Mungu wao,Je,kuna kitu gani cha kuogopwa zaidi ya Mungu?

Katiba is Bullshit like any other bullshit!

Marekani wenyewe hawafuati katiba yao kwenye mambo mengi sana ya muhimu....
Kwani wewe hujui kama kuundwa kwa FED ni kinyume na katiba ya Marekani?Sasa kama ni hivyo katiba ina umuhimu gani kama inaweza kukiukwa pale viongozi wanapoamua kufanya hivyo?

Acheni kufikiri kwa kutumia mawazo ya kibeberu,mabeberu wanatufanya tufikiri kwa tune yao ili tucheze mziki wao na tusahau wa kwetu.
Mkuu nime PM nisaidie mawasiliano yako
 
Wanabodi,
nitoe pongezi kwa President Samia kuwa rais wa JMT, kuongoza awamu ya Sita, hongera sana Mama Samia, umeanza vizuri kwa kuonyesha kuwa japo una nia ya kuyaenzi mazuri yote ya mtangulizi wako, umeonyesha kila mtu ana size yake ya viatu, sio vema kuvaa viatu vya mtu yoyote, bali viatu vyako vya size yako. Magufuli anazikwa na viatu vyake, huku ametuachia only mazuri yake ambayo ndio yanabebeka, na kwasababu he was a human being, lets carry only his good luggages, but not his baggages zake on his human side, awe amezikwa nazo na ikibidi, tuzungumzie his human side, only his good deeds.
Kilichofanyika leo bandarini, kilipaswa kufanywa jana. Kwenye bandiko hili nilizungumzia luggages na baggages, nikasema Samia abebe mizigo mema ya Magufuli, aendelee nayo, lakini asibebe mafurushi yake.

Bandari lilikuwa ni moja ya mafurushi hayo, leo ndio Samia amelitua, TRC kuna furushi, ATC kuna furushi, etc, ili Samia aende vizuri, abebe tuu ile mizigo ya JPM inayobebeka, yale mazigo, mafurushi na ma pakacha, yasiyo bebeka, lazima ayabwage, vinginevyo yatamuelemea ama yakamuangusha, ama akaanguka nayo!.

P
 
..jambo lingine linalompoza Mama Samia ni uoga wake kwa nchi za magharibi.
Mkuu JokaKuu , sio uoga bali ni kuzingatia ukweli mchungu kuwa mabeberu ndio wanaoendesha dunia!. JPM alikaza na kuwagomea, nini kilichompata na sasa yuko wapi?.

Hawa jamaa sio mchezo!. Niliwahi kuuliza humu

P
 
Hii ni MTR ya Bandiko hili
Tatu, nitoe pongezi kwa President Samia kuwa rais wa JMT, kuongoza awamu ya Sita, hongera sana Mama Samia, umeanza vizuri kwa kuonyesha kuwa japo una nia ya kuyaenzi mazuri yote ya mtangulizi wako, umeonyesha kila mtu ana size yake ya viatu, sio vema kuvaa viatu vya mtu yoyote, bali viatu vyako vya size yako. Magufuli anazikwa na viatu vyake, huku ametuachia only mazuri yake ambayo ndio yanabebeka, na kwasababu he was a human being, lets carry only his good luggages, but not his baggages zake on his human side, awe amezikwa nazo na ikibidi, tuzungumzie his human side, only his good deeds.
Hapa nilimpongeza Rais Samia kwa kuvaa viatu vyake vya size yake na sio kumtumbukiza mguu wake kwenye viatu vya mtangulizi wake.
President Samia umeonyeshwa uwezo kwanza ni kwa kulibwaga hilo zigo ulilolikuta hapo mlangoni kwako Ikulu. Pia asante kutuletea a real diplomat pale MFA na sio yule Mwalimu wangu Orator mzuri tuu, pale hapahitaji oration ni diplomacy.
Hapa pia alianza vizuri na a real experienced diplomat sijui nini kilitokea njiani, akamtoa, hatukuambiwa kosa lake lolote, na mpaka leo hatujui, ila akamleta yule Mama wa SADC, aka flop, sasa tuna kijana shababi pale!.
Mtihani pekee mkubwa kwako ni kuukubali ukweli kuhusu Corona and do the right thing. Kwenye hili nimewahi kushauri mahali na hapa nashauri tena, "Kwavile Magufuli alikuwa hapendi kupangiwa na hatukumpangia, nawaombeni members humu, tusimpangie Samia". Samia Suluhu yuko vizuri sana, anajua nini cha kufanya, tumwache afanye vile anaona inafaa, please let's give her space ".
Mtihani huu wa Corona, Rais Samia amepasi 100% kwa 100% with flying colours.
Kabla sikaanza, naomba kutoa angalizo muhimu. Kwa vile sasa Samia ndie rais, kuna watu sasa ndio wataanza kujipendekeza kwa Samia, hivyo kila mtu atakayeandika jambo lolote zuri kumhusu Samia akaonekana ana jipendekeza. Naomba usome bandiko hili uone nilisema nini kumhusu Samia na ni lini!.
Ukimsifu Rais Samia, unaonekana chawa wa Mama, huo ni uthibitisho wa baadhi ya sifa za Rais Samia ni sifa zake mwenyewe na hivyo ndivyo alivyo natural, yaani ni nature yake, ila sasa anaanza kubadilika mdogo mdogo, powers corrupt!, mtu mwenye sifa kama hizo za Rais Samia nilizo ziorodhesha hapo, haiwezekani leo aje atamke maneno kama haya Mama, I'm here to support you, to serve our country. I'm here sio tu kuonesha ujuzi wangu kwa nchi yangu, bali pia kuutumia. But... au Kauli ya Rais kwa waandishi 'Wapara' kuwa wakimpara "Atawaparua", Je Rais Samia ni katili?, Soma Jinsi ya kuwabaini makatili!. Ni kutumia macho tu!. hizi kitu lazima aachane nazo zina bad karma!.
Baada ya hayo sasa nije kwenye topic hii.
Kwanza mimi ni muumini wa kitu kinachoitwa karma, everything that happens, it happens for a reason, hivyo lolote likitokea, hakuna ubaya kulitafakari bila kumuuliza Mungu sababu, Mungu ana sababu zake kumchukua Magufuli na pia ana sababu zake kumleta Samia, we don't question God's authority.
We don't question God's authority at all!, lakini serikali yetu ilikuwa na wajibu wa kutupatia taarifa, keep us informed kuhusu hali ya afya ya rais wetu kuwa rais wetu ni mgonjwa, tuna watu wana powerful prayer powers wangeweza kumuombea akapona!, kuna watu wana powers hadi za kufufua, wangeambiwa on time, you never know labda wangemfufua!.
Japo kifo cha rais Magufuli ni kazi ya Mungu, lakini pia kuna vitu vya kibinaadamu vimechangia, kama heshima kwa marehemu, naomba nisivitaje, lakini kama kuna kitu unakijua kumhusu Magufuli na kinaweza kuwa kimechangia, na sasa unakiona kinaanzishwa mdogo mdogo kuelekezwa kwa Samia, ukiweza kukizuia, kizuie, mimi sina uwezo wa kukizuia, ila nina uwezo tuu wa kukisema ili wenye uwezo wazuie, wakiona hakuna haja ya kuzuia ni kupuuzia tuu, let it be, mimi kwa upande wangu nitakuwa nimesema na nimetimiza wajibu wangu, to inform.
Kuna wengi tumesema sana kuhusu kitu kinachoitwa karma, kwa Rais Magufuli, hakusikia, na sasa tunakisema kwa Rais Samia, sijui kama Rais Samia anasikia, ila kwa vile Samia ni mwema wa asili, ukiwa mwema, ukiwaza mema, ukitenda mema na ukitenda haki, hakuna adhabu ya karma kwa mtu kama huyu!
Siku zote nimekuwa nikihubiri humu, kauli huumba, hakuna kitu kina nguvu humu duniani kama kauli. Pia nikasema uongo ukisemwa sana na kuachwa kujirudia rudia bila kukanushwa, huwa na mtindo sio wa kuonekana kama ukweli, bali kauli hizo za uongo kuumba huo uongo in reality na kuufanya ukatokea kweli.
Ni kweli kauli huumba.
Moja ya majarida makubwa kabisa ya kimataifa ya kibeberu, The Economist, kwa miaka yote mitano limekuwa likiandika makala za uongo mwingi na ukweli kidogo za kumsakama rais Magufuli. Uongo huu umekuwa ukirudiwa rudiwa bila kukanushwa, na matokeo yake ukaja kugeuka ukweli, sasa Magufuli hatunaye tena, sasa tuna Samia, jarida hili sasa linajipanga kuanza na Samia!. Jee Tanzania tuendelee kuacha uongo ukisemwa kuhusu taifa letu na viongozi wetu hatu lini?!. Hivi ni hatuna uwezo wa kukanusha, au ni tunapuuza kwa hoja kuwa wasomaji wao hawatuhusu, sisi wanaotuhusu ni Watanzania tuu?!. Sasa tunaishi kwenye global world, ulimwengu wa kiganjani, uongo ukisemwa popote unaingizwa kwenye social media, kila mtu anausoma, mkisingiziwa uongo, msipo kanusha, uongo huo unaonekana ndio ukweli. Tanzania ya Samia must do something on this.
Awamu hii ya Rais Samia, anawatu wazuri zaidi kwenye Kurugenzi yake ya Mawasiliano, na Idara ya Habari Maelezo, kutokana na usafi wa Rais Samia, uongo na uzushi ni mdogo na ukitokea unakanushwa fasta.
Katika toleo lake la wiki inayoanzia April 3, The Economist limeibuka na makala hii kuihusu Tanzania ya Samia. Katika toleo hili this time angalau limeanza kwa kuonyesha Tumaini Jipya Tanzania: The Economist Baada ya Kumsakama Sana Rais Magufuli, Sasa Angalau Lina Matumaini na Rais Samia!, Laanza Nae Vizuri kwa kumtaka aachane na makosa ya Magufuli kwenye kudeal na Covid!. Yakwepa kuzungumzia chianzo cha kifo kilichotangazwa rasmi, waisingizia...

20210403_map502.jpg

Hoping for change​

Tanzania’s new president surely can’t be worse than the old one​

Paskali
Tunapoelekea mwisho wa mwaka, huku tukielekea mwaka wa uchaguzi, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko yangu kumhusu Rais Samia na kumfanyia MTR, ya tathmini ndogo ya political expectations zangu na awamu hii ya Rais Samia, nili expect nini, nini kimefanyika, nini bado hakijafanyika, na nini kinaweza kufanyika kabla ya 2025 ili Watanzania tufanye Uchaguzi Mkuu huru na wa haki unaosimamiwa na Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi. Ili kutuwezesha Watanzania tukafanya uchaguzi Mkuu huru na wa haki.
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 
Wanabodi,

Moja ya majarida makubwa kabisa ya kimataifa ya kibeberu, The Economist, kwa miaka yote mitano limekuwa likiandika makala za uongo mwingi na ukweli kidogo za kumsakama rais Magufuli. Uongo huu umekuwa ukirudiwa rudiwa bila kukanushwa, na matokeo yake ukaja kugeuka ukweli, sasa Magufuli hatunaye tena, sasa tuna Samia, jarida hili sasa linajipanga kuanza na Samia!. Jee Tanzania tuendelee kuacha uongo ukisemwa kuhusu taifa letu na viongozi wetu hatu lini?!. Hivi ni hatuna uwezo wa kukanusha, au ni tunapuuza kwa hoja kuwa wasomaji wao hawatuhusu, sisi wanaotuhusu ni Watanzania tuu?!. Sasa tunaishi kwenye global world, ulimwengu wa kiganjani, uongo ukisemwa popote unaingizwa kwenye social media, kila mtu anausoma, mkisingiziwa uongo, msipo kanusha, uongo huo unaonekana ndio ukweli. Tanzania ya Samia must do something on this.

Katika toleo lake la wiki inayoanzia April 3, The Economist limeibuka na makala hii kuihusu Tanzania ya Samia. Katika toleo hili this time angalau limeanza kwa kuonyesha Tumaini Jipya Tanzania: The Economist Baada ya Kumsakama Sana Rais Magufuli, Sasa Angalau Lina Matumaini na Rais Samia!, Laanza Nae Vizuri kwa kumtaka aachane na makosa ya Magufuli kwenye kudeal na Covid!. Yakwepa kuzungumzia chianzo cha kifo kilichotangazwa rasmi, waisingizia...
Paskali
Kumbe hawa jamaa kutusema vibaya walianza zamani toka enzi za Mwinyi
Rais Samia amesema baada ya Rais Mwinyi kuingia madarakani Gazeti la Economist la UK liliandika " Rais Mwinyi hawezi kuleta nafuu yoyote kwenye Uchumi dhaifu sana wa Tanzania kwa sababu Mwinyi ni Mtu wa Nyerere"

Ambacho The Economist hawakukijua ni kwamba Nyerere aling'atuka ili kuruhusu Mageuzi ya Kiuchumi na hayati Mwinyi alipewa Kazi hiyo, amesema Rais Samia
Source:TBC
Ni kweli. Hawa The Economist ni media ya kibeberu, siku zote wanatusema vibaya na walimwandama sana Magufuli, ila Samia walimfagilia. Samia tumaini jipya Tanzania: The Economist baada ya kumsakama sana Magufuli, sasa angalau lina matumaini na Samia, laanza naye vizuri na hapa TZ Trends & Analysis: Hoja 30 za The Economist Kumhusu President Samia. Kuna za Kweli, za Uongo na Uzushi na Kutaka Kumpangia Watakacho Mabeberu, Jee?

Hata mimi nimemfagilia Mwinyi Buriani Mzee Ruksa!. Ni Deng Xiaoping Wetu wa Mageuzi ya Kiuchumi, Demokrasia, Haki za Binaadam na Uhuru wa Habari. Asante kwa Ruksa Zako, Pumzika!.
P
 
Wanabodi,
Japo kifo cha rais Magufuli ni kazi ya Mungu, lakini pia kuna vitu vya kibinaadamu vimechangia, kama heshima kwa marehemu, naomba nisivitaje, lakini kama kuna kitu unakijua kumhusu Magufuli na kinaweza kuwa kimechangia, na sasa unakiona kinaanzishwa mdogo mdogo kuelekezwa kwa Samia, ukiweza kukizuia, kizuie, mimi sina uwezo wa kukizuia, ila nina uwezo tuu wa kukisema ili wenye uwezo wazuie, wakiona hakuna haja ya kuzuia ni kupuuzia tuu, let it be, mimi kwa upande wangu nitakuwa nimetimiza wajibu wangu, to inform.

Paskali
Kuupuuzia mchakato wa katiba mpya ni moja ya sababu, Rais Samia, anapaswa kufanya minimum reforms za katiba ili kuufanya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kuwa ni uchaguzi mkuu huru na wa haki.
P
 
Back
Top Bottom