Samia Suluhu: Wapinzani wako makini, CCM acheni kurusha vijembe!

Heri Mama Samia umesema kweli! Badala kujibu hoja wanaendelea kwenye matusi na upuuzi!

Uzuri wananchi wameshajua kuwa wabunge wa ccm wanapoteza muda na kujinufaisha wao sio wananchi waliowatuma! Angalia huyo kijana mpuuzi badala kuwakilisha kero za wananchi waliomtuma baada mama yake kufariki yeye anaenda kutukana wabunge wa kike! Ndio walichomtuma??

Naamini wananchi wameshakuwa na upeo sasa kazi wanayo wao! Piga chini hawa wabunge wa mbeleko!
 
Katika hali isiyotarajiwa makamu wa rais Samia Suluhu Hassan amekiri kwamba vyama vya upinzani vina wabunge makini wenye hoja za kuibana serikari. Amesema jinsi ya kupambana nao si kwa wabunge wa Ccm wa Ccm kurusha vijembe.

Katika mafunzo ya UWT kwa madiwani na wabunge yanayofanyika Dodoma Samia amekita Ccm kuandaa mafunzo maalum kwa wabunge wa wake kukabiliana na nguvu ya wabunge wa upinzani. Makamu huyo wa rais pia amekiri kwamba uchaguzi uliopita walikumbana na nguvu kubwa kutoka vyama vya Ukawa.

Chanzo: Mwananchi
 
Hakuna jambo gumu na ujasiri kama kubadilisha gea ya ndege angani. !
 
Kuna wabunge wanawapotosha wenzao...kuwa wapinzani wakitoa hoja nzito wewe toa Pumba ili kuidhoofisha ile hoja! Hawajui kuwa ndio wanajipoteza wenyewe! Sasa hata wakuu wao wameshaona wabunge wao hawajielewi!
 
Hebu naomba nieleweshwe!wabunge wa CCM wanaelekezwa wakapambane na upinzani au wakaisimamie serikali kwa niaba ya wananchi?
 
Wabunge wa CCM hawana hoja zaidi ya kupiga vijembe na kusubiri zipigwe kura waitikie "Ndiyoooooo!"

CCM ilipata upinzani mkubwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 na bila shaka wataendelea kupata upinzani hata 2020 kwa kuwa bado hawajabadilika. Wabunge wao wameendelea kuonesha ujinga na upumbavu wao pale bungeni na wananchi tunafahamu hilo licha ya serikali yao kuzuia bunge kuoneshwa live ili tusione upuuzi waufanyao.

CCM inakwenda kufa, amini usiamini. Kuna vijana wengi sana wa CCM wanaona hata haya kuvaa sare au zile fulana na kofia za chama wanazopewa ili kujipambanua katika matukio tofauti ya kichama.

Wana CCM hawana uwezo wa kujenga hoja. Wanachoweza ni vijembe tu na kuongopa, si unaona hata hapa JF, vijana wa CCM walio wengi ni wale waliojawa na ukasuku.
 
Heri Mama Samia umesema kweli! Badala kujibu hoja wanaendelea kwenye matusi na upuuzi! Uzuri wananchi wameshajua kuwa wabunge wa ccm wanapoteza muda na kujinufaisha wao sio wananchi waliowatuma! Angalia huyo kijana mpuuzi badala kuwakilisha kero za wananchi waliomtuma baada mama yake kufariki yeye anaenda kutukana wabunge wa kike! Ndio walichomtuma?? Naamini wananchi wameshakuwa na upeo sasa kazi wanayo wao! Piga chini hawa wabunge wa mbeleko!
Wakikutana wenyewe wanaongeaga ukweli juu ya akili kubwa wanayokutana nayo, wakienda bungeni Lao moja, hata huyu makamu akiingia bungeni maslahi Ni ya chama kwanza, mmemsahau kwenye bunge la katiba Mara hii?
 
Kuna wabunge wanawapotosha wenzao...kuwa wapinzani wakitoa hoja nzito wewe toa Pumba ili kuidhoofisha ile hoja! Hawajui kuwa ndio wanajipoteza wenyewe! Sasa hata wakuu wao wameshaona wabunge wao hawajielewi!
Na mbunge kilaza anakubali kumwaga pumba zake kujibu hoja makini!
 
Back
Top Bottom