Uchaguzi 2020 Samia Suluhu: Hata mkipigia kura kule kwingine CCM ndio inaenda kuunda Serikali, tutashinda vikubwa sana Tanzania

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,931
25,261

Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, (CCM), Mh. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 15/10/2020 amewambia wakazi wa Chunya mkoani Mbeya kuwa wasipige kura kwa Chama Kingine kwa sababu hata wakipiga kwingine Chama Cha Mapinduzi kinaenda kuunda serikali.

Amesisitiza kuwa watashinda vikubwa sana Tanzania, na amefananisha kupigia kura kwa chama kingine kama kitendo cha kumwaga sukari Ziwa Viktoria na kutegemea maji yatakuwa matamu, ambacho ni sawa na kupoteza sukari yako.

Mh. Samia amesisitiza kuwa maendeleo watakayoyaleta sio kwa wana CCM peke yake na wale ambao hawatokipigia Chama Cha Mapinduzi basi kura yao itawasuta pale watakapokuwa wanaletewa maendeleo.
 
Duh...
Kuna nini lakini

She shouldn't have said that line.

Kauli hii kama wanajua wataunda serikali kwanini wafanye kampeni.

Alafu hayo maendeleo yanayo yanayozungumzwa kwa zaid ya miaka 60 na CCM hii hii ni yapi.
 
'… Kwa upande wetu uchaguzi unaanzia wakati wa kuhesabu kura na unamalizikia wakati wa kutangaza matokeo…' Kinana kwny Mkutano Mkuu wa kumpitisha JPM
Ujinga kama huu hautarudiwa tena , njia zote zinajulikana

2332550_matokeo_uchaguzi_3.jpg
 
Back
Top Bottom