Samia Suluhu Hassan anatarajia kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwenye Mkutano wa dharura wa pamoja baina ya SADC Organ Troika

Watanzania wenzangu pamoja na tofauti zetu za kiitikadi, lakini ni vema tukaonyesha heshima kwa mkuu wetu wa nchi, kwa nafasi yake kama mkuu wa nchi, inampa hadhi ya tofauti kabisa na Watanzania wengine

Kwa taarifa yako tu, kwenye mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi za SADC, ulifanyika agosti 2019, hapa jijini Dar es Salaam, lugha ya kiswahili ilipitishwa rasmi na kuwa mojawapo ya lugha rasmi kwenye SADC
Nadhani Kiswahili ni lugha ngumu kwako mkuu..ni wapi Mheshimiwa Rais Mzalendo ameondolewa hashima yake?
Kumbuka ata Katiba inasema yeye ndiye anabidi kuheshimiwa tu
 
Watanzania wenzangu pamoja na tofauti zetu za kiitikadi, lakini ni vema tukaonyesha heshima kwa mkuu wetu wa nchi, kwa nafasi yake kama mkuu wa nchi, inampa hadhi ya tofauti kabisa na Watanzania wengine

Kwa taarifa yako tu, kwenye mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi za SADC, ulifanyika agosti 2019, hapa jijini Dar es Salaam, lugha ya kiswahili ilipitishwa rasmi na kuwa mojawapo ya lugha rasmi kwenye SADC
Haya kiongozi, heri yako wewe mwenye ID inayotambulika! Jitahidi uteuzi upo karibu sana.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwenye Mkutano wa dharura wa pamoja baina ya SADC Organ Troika (Botswana, Malawi na Zimbabwe), na nchi zinazochangia Vikosi vya ulinzi na amani vya Umoja wa Mataifa, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwenye Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC utakaofanyika tarehe 28 Novemba 2020, mjini Gaborone, Botswana.

Akithibitisha kuhusu ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo utaongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye atakuwa anamwakilisha Mhe. Rais.

Kwa mujibu wa Prof. Kabudi, mkutano huu utatanguliwa na mkutano wa Maafisa Waandamizi/Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama na kufuatiwa na mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama tarehe 26 Novemba 2020.

"Pamoja na Mambo mengine, mkutano huo utajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda ya SADC na kuweza kuona changamoto mbalimbali zilizojitokeza na kupata majibu ya kutatua changamoto hizo," Amesema Prof. Kabudi

Makamu wa Rais ataambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi Dkt. Faraji Mnyepe pamoja na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda na Mratibu Kitaifa wa Masuala ya SADC, Bibi Agnes Kayola.

ASASI ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) inawajibika kukuza amani na usalama katika eneo la SADC na pia ina wajibu wa kuongoza na kuzipatia nchi Wanachama mwongozo kuhusu mambo ambayo yanatishia amani, ulinzi na usalama.
Tatizo ni Lugha
Lazima kuwe na delegations za hapa na pale
 
When language is a barrier you become a prisoner of yourself.
Prison of your own imaginations doesn't apply to everybody buda, he's living his best life, he chooses not to go, not bcoz of language, there are translation headphones dumby.
 
Watanzania wenzangu pamoja na tofauti zetu za kiitikadi, lakini ni vema tukaonyesha heshima kwa mkuu wetu wa nchi, kwa nafasi yake kama mkuu wa nchi, inampa hadhi ya tofauti kabisa na Watanzania wengine

Kwa taarifa yako tu, kwenye mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi za SADC, ulifanyika agosti 2019, hapa jijini Dar es Salaam, lugha ya kiswahili ilipitishwa rasmi na kuwa mojawapo ya lugha rasmi kwenye SADC
Jina zuri, mwenye jina hovyo. Verified member chizi!
 
Anamdhalilisha tu mama Samia,kuwa amepewa hicho cheo kwenda kwenye mikutano...
 
Back
Top Bottom