Samia Suluhu, doa la kumfunga Mbowe halitafutika, watangulizi wako wote walilikwepa

Mama anahuruma sana, amefanya mazuri kwa viongozi wenu, wengine amewakuta lockup amewatoa, na faini mmerudishiwa lakini pamoja na yote bado mkaendelea mnamfanyia dhihaka, dharau na kujichukulia maamuzi mnavyotaka kwakuwa tuu huyu ni mwanamke acha tufanye tunavyotaka. Sasa hiyo ndiyo shukurani!!! Ninyi hata awafanyie wema gani huyu mama mtaendelea kumchukia, kumzarau na kujichukulia maamuzi.

Mimi acha niseme ya moyoni, chama kikiwa chini ya viongozi wa kichagga sitegemei kuja kushika dola, wengi wenu mnaasili ya ujeuri na ukorofi sasa mmpewe dola kweli!! Si mtatumaliza kabisa.

Ili chadema iendelee kuwepo na kufika mbali na hata kushika dola yawapasa mkivuruge, toeni viongozi wote wa kichagga safisheni kabisa mwanze upya na makabila mengine kama vile wasukuma, wazigua, wanyakyusa, wanyamwezi, waha na akina tundu lisu n.k utaona kama hamjafika mbali na hata kushika nchi.
Hiyo tunaita ni Inferiority Complex kwa wote kwako na kwa rais.
 
Sawa kwahiyo Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli wote hawakuona jinai ya Mbowe kaja Samia hata hajamaliza miezi mitatu kaiona? Think!
Kwani Mbowe anashutumiwa kwa kosa alilotenda lini? -labda kama unafahamu kuwa tangu enzi za Nyerere alitenda jinai ! Tujuavyo sisi jinai hii ni wakati wa awamu ya 5
 
nyie siasa hamuijui hapo mbowe hafungwi kinachofanyika ni kumchosha tu na kumpotezea muda baaadaee anaachiwa watu washafanya yao wala msifikiri anafungwa siasa ni kazi kama kazi zingine tu
Kwaiyo ni ujanja kumpotezea mtu mda na kumchosha?
 
Kwani Mbowe anashutumiwa kwa kosa alilotenda lini? -labda kama unafahamu kuwa tangu enzi za Nyerere alitenda jinai ! Tujuavyo sisi jinai hii ni wakati wa awamu ya 5
Samia kairithi na kujihakikishia? Hakuwa na option nyingine zaidi ya kumfunga? Ndio maana nasema uongozi ni karama.
 
Tukiacha mahaba ya vyama, au kati ya mtu na mtu kwanini inatumika nguvu kubwa kuiaminisha jamii kuwa Mbowe kaonewa ihali kesi bado inaendelea na anamawakili mahili kupata kutokea nchi hii.
Tuache sheria ichukue mkondo wake na mahakama zifanye kazi yake.
Jiulize pia kwanini Rais wa nchi na Mkuu wa Polisi walitumia nguvu kubwa kuuaminisha ulimwengu kua Mbowe ni Gaidi wakati mahakama zipo?
 
Hajaingilia mahakama labda kama hujui huo mkondo wa sheria ulivyo. Mkondo huu unaanzia kwa vyombo vya serikali kukusanya ushahidi dhidi ya mtuhumiwa. Serikali ikishajiridhisha kuwa ushahidi dhidi ya mtuhumiwa umekuwa wazi ndipo serikali humkamata mtuhumiwa na kumpeleka mahakamani. Serikali haiwezi kupeleka mahakamani mtuhumiwa ye yote kama haijapata ushahidi ulio wazi dhidi yake. Baada ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani, mkondo wa kisheria wa mahakama huanza na hukamilika kwa maamuzi/ hukumu ya hakimu / jaji. Serikali huwa haiingilii huo mkondo (mchakato) wa kisheria wa mahakamani.
Unawakamata wakina Fupi lakini Bin Laden unamwachia atambe?

Amandla...
 
hakuna umaarufu anapata huyo jamaa kesi inaisha uchaguzi ushapita sasa mpaka miaka kumi tena mbowe keshazeeka na chadema hoi

..na baada ya uchaguzi Maza akifa kama Magufuli itakuwaje?

..Magufuli aliukamia Uraisi matokeo yake akafa miezi michache baada ya ushindi wa tsunami.

..Jambo la msingi ni kutenda HAKI wakati wote.
 
nyie siasa hamuijui hapo mbowe hafungwi kinachofanyika ni kumchosha tu na kumpotezea muda baaadaee anaachiwa watu washafanya yao wala msifikiri anafungwa siasa ni kazi kama kazi zingine tu
We baba yako angepotezewa muda ungefurahi
 
usimlnganishe mandela na hawa jamaa mandela ile kichwa nyingine acha kabisa mbowe alishaonyesha udhaifu hata ndani ya chama chake kukatalia kwenye uenyekiti hataki wenzie warithi miaka nenda rudi mandela uliona anatabia hizo
Amekalia au anachaguliwa
 
..na baada ya uchaguzi Maza akifa kama Magufuli itakuwaje?

..Magufuli aliukamia Uraisi matokeo yake akafa miezi michache baada ya ushindi wa tsunami.

..Jambo la msingi ni kutenda HAKI wakati wote.
kwani mbowe akiwa rais akaja akafa mtafanya nini au yule ni mtu wa chuma kama robot hafi yeye? unamaswali ya kiuchi wa kike kweli we jamaa
 
Tukiacha mahaba ya vyama, au kati ya mtu na mtu kwanini inatumika nguvu kubwa kuiaminisha jamii kuwa Mbowe kaonewa ihali kesi bado inaendelea na anamawakili mahili kupata kutokea nchi hii.
Tuache sheria ichukue mkondo wake na mahakama zifanye kazi yake.
Nguvu kubwa inatumiwa na Lumumba kuwaleta Kaaya, mama muuza Mbege, Mzee wa Ballistic,Kingai ili kutoa ushahidi wa uongo
 
Kwani hao wafungwa wote walioko gerezani wao sio binadamu?? Mpaka doa lionekane kwa kufungwa kwa mbowe? Kama unampenda mtuu unamshauri kablaa hajapatwa na matatizo. Mbowe akionekana na kosa sheria ichukue mkondo wake bila upendeleo.
Kwa ushahidi wa Kaaya na muuza Mbege,, yaani umfunge Raila odinga afu wakenya wasipige kerere, umfunge, Trump afu Americans wasipige kerere, ukweli Ni kuwa si Kongai, Hangaya, mawakili wa serikali wanaotaman kesi hii hisiwepo Ila wanatafuta jinsi ya kuitema
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom