Samia Suluhu awatangazia ‘kiama’ waliosalimika kwenye uhakiki wa vyeti feki

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewaonya watumishi wenye vyeti feki waliosalimika akisema awamu ya pili inakuja.

Akizungumza katika ufungaji wa kilele cha maadhimisho ya siku ya maadili duniani kwenye Viwanja vya Nyerere mjini hapa jana, alisema kutokana kutoridhishwa na utendaji kazi wa baadhi ya taasisi, Serikali imeamua kufuatilia idadi halali ya watumishi wa umma, uhalali wa vyeti na ulipaji wa mishahara.

“Kazi hii itakuwa endelevu ndugu zangu, kama kuna mtu alinusurika wimbi la kwanza naomba akae vizuri wimbi la pili linakuja. Serikali imekuwa ikipoteza fedha kutokana na watumishi hewa, jambo hili hatuwezi kulifumbia macho,” alisema.

Alisema Serikali haiwezi kuendelea kuwa na watumishi hewa, wasiowajibika na wasiofanya kazi kikamilifu au kufanya kazi kwa ugoigoi.

Akizungumzia utendaji, Samia alisema katika kutatua changamoto za utumishi, Serikali imeanza kuweka mfumo wa kanzi data na mifumo ya kutoonana wakati wa kutoa huduma.

Alisema kwamba kuna tabia ya baadhi ya watumishi wa Serikali kufanya kazi bila kufuata mikataba ya huduma kwa wateja.

Makamu wa Rais alisema ni vyema huduma zinazotolewa zikaanishwa bayana na muda utakaotumika.

“Kama kuna mtu mzembe mahali popote nawataka viongozi wasisite kumuondoa, hakutakuwa na mapengo mengi katika ajira. Kuna vijana wengi wanasubiri ajira ambao tunataka tuwajengee uzalendo, ubunifu na uadilifu mkubwa,” alisema.

Alisema kuna kesi nyingi katika Mahakama ya Kazi ambazo zinahusu upotevu wa maadili kwa vijana, wizi na kutowawajibika.

“Hatuwezi kusema tunajenga Tanzania ya uchumi wa kati kama vijana wako kwenye njia hii ya maisha. Lazima kampeni hii (ya uzalendo na utaifa) kufundisha vijana wetu,” alisema.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), George Mkuchika alisema katika mapambano dhidi ya rushwa, kuelimisha inachukua nafasi kubwa kwa sababu Watanzania wakielimishwa masuala ya maadili na rushwa kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu tatizo hilo litapungua kwa kiasi kikubwa.

“Tuanze na wafanyakazi wa Serikali, leo kuna mkutano wa baraza la wafanyakazi, tunaomba mkiwa na mikutano kama hiyo mtualike kuja kutoa semina,” alisema.

Alisema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imekuwa ikitumia fedha nyingi kwa kodi ya majengo, hivyo ameiomba Serikali kuwasaidia.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alisema hivi karibuni yamejitokeza madai kama vile haki ya ndoa za jinsia moja.

“Ukweli ni kwamba hiyo ndiyo haki hatarishi dhidi ya binadamu. Kwa sababu watu watakosa fursa ya kuzaliana. Hii ndio inakwenda kuua Taifa. Binadamu hawatakuwapo,” alisema.

Spika wa Bunge Job Ndugai alisema Bunge liko tayari katika utungaji, urekebishaji wa sheria na kwamba kama kuna sheria zinazotakiwa kutiliwa mkazo katika eneo la maadili wako tayari kufanya hivyo.

“Bunge litakuwa tayari kuweka fedha nyingi zaidi katika maeneo hayo ya utawala bora,” alisema.


Chanzo: Mwananchi
Muhakiki hadi ktk jeshi la polisi sio muwaonee walimu tu.
 
Nadhani sasa ndi ile amawamu ambayo haitamuacha mtu salama na itakata shauku ya watanzania wengi walio tega sikio juu ya jambo fulani
 
Hii Awamu mbovu sn. Kijana atapataje kuwa Goi goi kama maslahi duni hasa sekta ya elimu ambyo inavijana wengi? Maslahi ni kitu Cha msingi ktk tathnia yeyote ile. Ajira ya serikali haijawai kuwa mateso awam zote. Serikali haijawai kuwa ya kibaguz wa wazi miaka ya nyuma. Kuna kada zina hakikiwa zengine hapana. Maana ya uhakiki ni ipi? Upuuz mtupu
 
Hakuna wimbo naupenda kama huu "Ccm mbele kwa mbele,
Wacha waisome nambaaeee,waisome nambaaaa
Ccm mbele kwa mbele

Ngwa,ngwa....,ππππππππππππ"

Kila neno moja lina maana kubwa sana kwenye wimbo huu!
 
Back
Top Bottom