Samia Suluhu: Amani ya kweli haimaanishi kutokuwepo kwa fukuto au migogoro bali ni kuwepo kwa Haki kwa jamii

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania amesema, amani inatokana na haki.

Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) tarehe 24 Januari 2021, jijini Mwanza amesema, haki ndio msingi wa amani.

“Mheshimiwa Jaji Mkuu sote unatambua kuwa kuendelea kwa taifa lolote, kiuchumi, siasa na kijani inategemea amani na utulivu uliopo katika jamii husika.

“…amani ya kweli sio kutokuwepo na fukuto, migogoro na mivutano, bali ni uwepo wa haki ambayo itazuia hayo yote, na hilo ndilo jukumu la mahakama.”

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma; Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dk. Eliezer Mbuki Feleshi, umewakutanisha wanachama wake zaidi ya 200.

Miongoni mwa wanachama hao ni Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Wasajili, Naibu Wasajili, Mahakimu na maofisa wengine wa mahakama katika ngazi mbalimbali.

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma
Mama Samia amesema, haki ni mojawapo ya misingi mikuu ya kuleta amani katika taifa lolote duniani, hivyo haki ikitolewa kwa wakati, itaongeza maendeleo kwa haraka, na pia ikicheleweshwa, huchelewesha maendeleo.

“Lakini ucheleweshaji huo husababisha migogoro inayopelekea kuvurugika kwa amani, utulivu na kupelekea watu kutoweza kuishi vizuri,” amesema.

Amesema, Mahakama Kuu ilianza na majani watatu, Jaji Mkuu na majaji wawili, baada ya mageuzi na mapito mengi, kwa sasa Mahakama Kuu ina majaji wanawake 23 na wanaume 50.

Na kwamba, kwa sasa kuna majaji wa rufani, wanawake saba na wanaume tisa “nataka nipongeze sana hatua hii iliyofikia, ilikua ni ndoto kuona mwanamke anasimama kama jaji wa mahakama ya rufani au jaji wa mahakama kuu, lakini kwa mageuzi mbalimbali, mifumo ya elimu na mambo yaliyotokea, sasa imewezekana.”

Amesema, katika kipindi cha miaka 100, mahakama imepitia mapito mengi kutoka kuwa chombo cha kikoloni mpaka kuwa chombo huru na kwamba, mahakama imeweza kuhimili mabadiliko mbalimbali ya kikanda na kimataifa.

“Hakika hii ni safari ndefu sana, iliyojaa mabonde na milima lakini hatimaye mmevuka na kufika hapa mlipo katika Karne ya 21, mkikabiliana na yanayotokana na wimbi la mapinduzi ya nne ya viwanda,” amesema.
 
Leo ndio amejua amani ni tunda la haki?

Kumbe wakati akiwa kule Mbeya kwenye kampeni aliposema CCM lazima washinde hata kama hawatapigiwa kura alikuwa hajui amani ni tunda la haki.

Wanawanyima wapiga kura haki yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka makusudi, halafu wakishapata wanachotaka ndio wanasema amani ni tunda la haki, this is pure politics.
 
Kwa mara ya kwanza tangu kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana kiongozi wa serikali hii ametamka neno HAKI.

Neno haki kwa Wana CCM wanaliogopa kama ukoma!
 
Haki ipi hiyo? Ya kuibia wananchi kura? Samia unafikiri kuwa tumesahau uliposema wakati ule wa kampeni kuwa hata kama wananchi wataichagua chadema CCM itaunda serekali?
 
Pamoja na kujitambulisha kama mfuasi wa kristo kweli kweli lakini Magufuli hajawahi kutamka neno HAKI!! sijui ni Mungu yupi wanaemhubiri.
 
Back
Top Bottom