Samia Suluhu aipongeza Azam TV kwa kutoikosoa Serikali sana

Umenitoa Gizani

JF-Expert Member
Dec 3, 2016
387
179
Makamo wa rais ameipongeza azam TV kwa kutokuwa na ukosoaji mkubwa kwa serekali na kusapoti shughuli za ki serekali.

Aidha azam TV imekuwa ikiwaalika viongozi wa serekali kutolea ufafanuzi mambo yenye kuhitaji ufafanuzi badala ya kuhukumu
 
Serikali kubalini kukosolewa maana hataninyi nibinadamu mnamapungufu yenu.. Lakini kazi zenu ninaanza kuzikubali japo sijalizika mpa majizi yalio iba pesa za esikulo yafilisiwe bila aibu hii sasa itakua selikali yamfano balani afrika..
 
Siku hizi tbc inakosoa serikali?
Mbona haisifiwi maana ni chombo chao, na kwani hawaaliki viongozi na kutolea ufafanuzi baadhi ya mambo?
Lakini angepaswa ashukuru zaidi wale wanaowakosoa maana bila kukosolewa hamna kitu...
[HASHTAG]#Tuwakosoe[/HASHTAG] tu..!
 
:D:D:D:D Hii nchi yetu bana. Yaani inabidi kucheka tu. Kwasasa na mimi nimeamua kuwa Mtazamaji tu. Ngoja nitafute pesa nisije kupunguza siku zangu za kuishi na baraka zangu kwa ujinga ufanywao na serikali ya Mtakatifu John.
 
Aljazeera, CNN, BBC, DW zimekuwa maarufu duniani kutokana na weledi wa kuandika na kufuatilia na kukosoa uozo wowote ule uwe wa serikali, upinzani au waasi. Cha msingi ni kuzingatia weledi na facts.

AZAM jiangalieni, kamwe hamtajenga jina lenu kama mtakuwa TBC2; msiingie mtego huo kama mnataka kutawala soko la media na kujitanua kikanda na kimataifa. Ushauri tu.
 
Duuh huyu mama kabla ya ile tetes ya kusema aliomba ajiuzuru alikuwa anaenda pouwa sasa kama simuelewi alisema kaokoa milion 40 kisa kapanda atc lkn anapokodi ndege hasemi! Hii ya leo kupongeza mtu asiyekukosoa hii ni maajabu na haya maajabu yanapatikana nchi maskini! Kwa kuwa wenye uelewa ni wachache! Naomba hii awamu hii ipite haraka sijui mmebaki na miaka 3 sijui nane but mmezidi, mnapendwa msifiwe? Yaani kodi zetu mmekuja mmeomba kura kwetu na bado tusiwakosoe!
 
Ajabu! Kitu kinachoitwa kukosolewa, ni msisitizo wa viongozi wote duniani wanao waongoza watu, isipo kuwa manabii walio tumwa na mungu peke yao ndio hawasemi; mnapo niona nakosea mnikosoe nipate kujirekebisha
 
Hii ndio serikali yetu ya muujiza inayosifia vyombo vya habari visivyo kosoa serikali licha ya kwamba inamakosa kibao. wanaogopa kukosolewa kama ukoma, Serikali isiyojiamini, woga, isiyo thubutu,
 
Ndg. Tido Mhando, isaidieni serikali kuendeleza 'shughuli' zake au inusuruni fani ya habari inayoangamia!
Pia jitahidi kuhudhuria mazoezi ya viungo kila jumamosi ...sijui baada ya kufanya usafi!
 
Naona kauli " Kama unaona huwezi acha nitateua mwingine" imemtia mama wenge nae sasa anacheza ngome ya mkuu!!! Kweli kwa sasa hamna aliebaki kwani aliekuwa amebaki mwenye hafadhali alikuwa yeye peke yake!!!!!!
 
:D:D:D:D Hii nchi yetu bana. Yaani inabidi kucheka tu. Kwasasa na mimi nimeamua kuwa Mtazamaji tu. Ngoja nitafute pesa nisije kupunguza siku zangu za kuishi na baraka zangu kwa ujinga ufanywao na serikali ya Mtakatifu John.
Nilipanga kununua Azam Dish...kwa heri!
 
Haya maneno kasema kweli Makamu wa Rais? Basi kumbe hakuna kwenye afadhali.
Sasa serikali sii imeanzia ngazi ya serikali za mitaa mpaka Magogoni, bila ukosoaji wa yale mabovu watajuaje huko juu?
Sifa pekee zitatupeleka wapi?
Kumbe na huyu ndio walewale tuu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom