Samia Rais wa Ustawi

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,649
2,911
Katika Taifa moja, kuna wakati watu waliambiwa, "Taifa hili ni tajiri. Ninyi ni matajiri". Wengi wakaamini.

Wakaamini kuwa ghafla wamekuwa matajiri. Japo wengine hata kupata milo miwili ni shida, waliamini kuwa labda matajiri ndivyo wanavyoishi. Wengine japo kununua nguo mpya ni shida, waliamini kuwa huenda matajiri wote huvaa mitumba iliyokuwa awali imevaliwa na malaika. Japo wengine hata kupata nauli ya basi ili aende kwenye matibabu ya bure haikuwezekana, waliamini matajiri wa siku hizi za mwisho, huenda hawahitaji matibabu. Pamoja na yote hayo, wote walishangilia kwa kuwa ni matajiri, na wana mfalme wao asiyetikiswa wala kutikisika kwenye maisha ya utajiri.

Mshtuko mkubwa ni pale mfalme wao alipowakataa kuwa yeye siyo mfalme wao tena. Siyo mfalme wa matajiri. Yeye siyo mfalme wa nchi ile tajiri bali ni mfalme wa wanyonge, yaani yeye ni kiongozi wa Taifa nyonge lenye raia wanyonge, raia maskini. Matajiri wale wa mlo mmoja wakabakia bila mfalme. Wakaulizana, mfalme wao atawapata wapi hao wanyonge maskini wa kuwaongoza kwenye Taifa lile tajiri lenye watu matajiri? Na wao wataongozwa na nani?

Mfalme yule kwa vile hakuwa na watu wa kuwaongoza ( watu wanyonge), akaanza jitihada kubwa ya kutengeneza wanyonge ili awe na wafuasi wengi wa kutosha, awe na watu wanyonge, watakaomwimbia na kumwabudu yeye pekee aliye imara. Wenye pesa bank, baadhi yao, zilinyang'anywa kwa kutumia ART. Wengine walitekwa kwa kuonesha wana dalili ya kukataa kuwa wanyonge. Kesi za kutengenezwa za uhujumu uchumi, zilitamalaki ili mfalme ajipatie kundi kubwa la wanyonge. Mfalme alihitaji wanyonge wa akili na mali.

Mfalme alifanikiwa kuigeuza Dunia vichwani mwa wanyonge wake. Wote wakakubali kuwa Dunia ni ya pembetatu, na wala siyo ya mviringo tena. Wanyonge wakawa wanyonge kweli, wakageuka kutoka kuwa wanyonge wa mali mpaka kuwa wanyonge wa akili. Baada ya kuwa wanyonge wa akili, walichokijua ni kuabudu na kumsifu mfalme, maana yeye pekee hakuwa mnyonge. Waliobahatika kuwa wanyonge wa mali pekee, lakini wakabakiwa na akili, japo kidogo, wakalia na kusaga meno. Maombi yao kwa mola wao hayakuwa haba. Wale wanyonge wa akili, walijua kuwa juu ya mfalme wao hapakuwa na nguvu nyingine yoyote.

"Nimekisikia kilio cha watu wangu", ikasikika sauti kutoka juu. Mfalme akapumzishwa. Katika nchi ile, mpaka leo, wapo wanyonge waliogundua kuwa walinyongeshwa lakini wanyonge wa akili wanaendelea kujivunia unyonge wao.

Ndugu zangu unyonge ni laana, unyonge ni kupungukiwa mali au akili, unyonge siyo sifa. Unyonge ni ugonjwa. Unyonge ni udhaifu. Mtu mwenye akili timamu hawezi kujivunia ugonjwa au udhaifu. Unyonge unatakiwa kupigwa vita, na wala siyo wa kujivunia. Mtu anayeweza kutamka hadharani kuwa wewe ni mnyonge, yupo kwaajili ya wewe, ni adui wa nafsi yako. Mtafute mtu anayekerwa na unyonge, anayeudhiwa na unyonge, anayeongoza mapambano ya kuushinda unyonge.

Rais Samia, kwa matendo na kauli zake, inaonekana anachukizwa na unyonge, anatafuta ustawi wa kila mmoja kwa sababu ustawi wa mtu mmoja mmoja ndiyo ustawi wa Taifa, na ustawi wa Taifa ndiyo uimara wa Taifa. Ili vita ya kuushinda unyonge ifanikiwe, kwanza tuuchukie unyonge, na pili tuukatae na tatu tutafute njia za kuushinda unyonge. Rafiki mkubwa wa unyonge ni woga. Unyonge na zao la uoga wa kuchukua hatua sahihi, wakati sahihi kwenyeazingira sahihi.
 
Story ndefu sn kifupi kwasasa hakuna uchumi wa kati wala wanyonge, mauji, utekaji, ubambikaji kesi za uhujumu uchumi n.k, maza ni dhaifu lakini tuna amani sn hana time na mtu, maendeleo kila mtu atatafuta kwa muda wake. maana hata fisi wana maendeleo wanakula na kunywa
 
Kiukweli maelezo yaliyo katika fumbo yamekuwa mengi sana ila kontenti yako ni ndogo tu. Juu yakuupinga vita unyonge pamoja nakumsifia Samia. Sodhan kama ulikuwa namaana tofauti zaifi yahiyo yakumpakazia Hayati JPM nakumsifia Samia.
 
Back
Top Bottom