Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,451
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na Makala zangu elimishi za "Kwa Maslahi ya Taifa", Makala ya leo ni jinsi Rais Samia alivyo ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Rais Samia, Akifanikiwa kwenye hili, atabarikiwa sana na taifa la Tanzania, litabarikiwa!

Natoa wito kwa wote wenye mapenzi mema na nia njema na taifa letu la Tanzania, sote katika umoja wetu, tupaze sauti zetu juu na kumshukuru Mungu kwa kutuletea Samia, "Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, ili atimize mapenzi yako"!

Mungu Ibariki Tanzania"!

Screen Shot 2022-07-10 at 8.40.45 AM.png
Screen Shot 2022-07-10 at 8.41.09 AM.png

Naomba kuanza bandiko hili kwa angalizo hili la tofauti kati ya pongezi za kujikomba kutafuta uteuzi, na pongezi za kweli bonafide genuine.
Humu jf, toka enzi za Ben, JK, JPM na Sasa Samia, kuna baadhi ya waandishi wa habari, wamekuwa wakila shavu la kulamba uteuzi kwa kuteuliwa, DC, Ras, Das au Wakurugenzi, hivyo mwandishi yoyote wa habari, akisifu jambo lolote zuri au jema linalofanywa na rais wa nchi, atanyooshewa vidole vya kusifu kwa uchawa tuu ili kujipendekeza kusaka fursa za uteuzi.

Declaration of Interest Kuhusu Kusifu
Mimi Pascal Mayalla ambaye ni Mwandishi wa habari wa kujitegea kwa kujitolea, naandika kwa kutanguliza mbele Maslahi ya Taifa tuu, na ikitokea nimesifu au kumpongeza mkuu wa nchi, sifa hizo na pongezi hizo ni pongezi bonafide genuine za kupongeza na sio kusaka fursa ya uteuzi wa kula shavu lolote katika teuzi za kwenye kisahani cha chai. Mimi sitafuti uteuzi wowote kwa yeyote, naondelea tuu kumuombea Mama azidi kuifungua nchi, mfano sasa nimerudi kwenye Maonyesho ya Saba Saba. Katika ziku ziku 10 za Saba Saba pekee, Mimi Pascal Mayalla, kupitia vipindi vyangu vya SabaSaba na PPR, vitaiingizia serikali kodi ya zaidi ya TZS milioni 100!. Sasa ni mshahara wa DC gani utachangia kodi ya serikali ya milioni 100
ndani ya siku 10!?. Sasa mtu wa maokoto hayo, autafute u DC wa nini?. Acheni Hizo!.

Tofauti ya Pongezi za "Uchawa" na Pongezi Bonafide Genuine.
Kiukweli kabisa, the dividing line between pongezi za uchawa na kujikombakomba na pongezi za kweli za encouragement bonafide genuine is very thin!, tofauti ya uchawa kama mataga, na pongezi za kweli mataga ni pongezi za fagilia, ni wakati pongezi za kweli ni critical, tunapongeza kwa jambo zuri la kweli la kustahili pongezi. lakini siku huyo anayepongezwa kwenye pongezi za kweli, akiharibu, anakula spana!, machawa wao kazi yao ni kupongeza tuu hata akiaharibu vipi wao watapongeza tuu lakini mimi pongezi zangu kwa Samia ni bonafide Genuine, na siku akiharibu, tuna mpara ila kwa heshima.
Sasa twende kwenye mada ya leo.

Kila jambo hutokea kwa sababu, hata likiwa jambo baya, kunaweza kutokea jambo mbaya kumbe lina wema ndani yake, mfano wa Yesu kwa Wakristu, alikuja ili kuukomboa ulimwengu, Yesu aliteswa hadi kufa kifo cha aibu kwa kuwambwa msalabani! hiki ni kifo kibaya kuliko vifo vyote, ila ni kwa kupigwa kwake na kwa kuteswa kwake sisi tuliponywa, ukombozi ulipitia mateso na kifo cha msalabani ile dhambi ilikufa, ila aliyashinda mauti kwa ufufuko na kutuachia uzima wa milele kwa waaminio japo miili hii ya kidunia itakufa, lakini mwili wa kiroho haufi na tukapata uzima wa milele!

Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa JPM, alikuwa ni chaguo la Mungu kwa Tanzania, baada ya Tanzania ya JK, Tanzania aliyoipokea JPM, mahali ilipofikia, ilimhitaji mtu wa JPM type kuinyoosha kwanza, Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania ilihitaji Dikiteta, tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba! ndipo aje mtu kama Samia, kuipaisha, aliyoyafanya yale aliyoweza kuyafanya, ikiwemo kuchonga mabarabara mengi katika mambo mengi hadi kuitwa Tingatinga, baada ya kuukamilisha mpango wa Mungu kwa Tanzania kupitia JPM, Mungu akamuita kwake kwa namna ambayo ilituachia majonzi, lakini ndio mpango wa Mungu yeye kuondoka kwa namna hiyo, na hatuwezi kuhoji kwasababu kazi ya Mungu haiina makosa.

Kama JPM alikuwa ni mpango wa Mungu kwa Tanzania, na baada ya Mungu kumuita JPM kwake na kumpangia majukumu mengine kule, ujio wa Samia pia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania, mpaka hapa tulipofika, Rais Samia, ameisha onyesha kwa kauli na matendo, kuwa na yeye ni mpango wa Mungu kwa Tanzania, Watanzania wote wapenda mema na ustawi wa taifa hili, sote tuseme Asante Mungu kwa Samia.

Hatusemi asante Mungu kutuondolea JPM na kutuletea Samia, tunasema asante Mungu kwa JPM na asante Mungu kwa Samia, kila zama na zama zake, kwa vile JPM alikuwa binaadamu na sio malaika, yale mambo ya kibinaadamu yasiyotupendeza enzi za JPM, tuyaache, tusiendee kuyasema sema ni kama kumsimanga marehemu, tumuache JPM apumzike kwa amani, na kwa mazuri ambayo Samia sasa anayafanya, tumpongeze Samia kwa mazuri yake bila kumlinganisha na mtangulizi wake.

Samia alipoingia tulishauri Mwaka 2021 ulikuwa ni Mwaka wa Majanga kwa Tanzania. Mwaka 2022 uwe Mwaka wa Mabadiliko, Watanzania tubadilike! Happy New Year!

Enzi za JPM, kuna baadhi yetu tulikuwa hatukohoi, na JPM alisema wazi “mimi sipangiwi” na hatukumpangia, Samia mara tuu baada ya kuingia, ameruhusu watu sasa tunakoa, kwa vile JPM hatukumpangia, nashauri hata kwa Samia, kama ni kukohoa tukoe lakini na yeye tusimpangie!

Pamajo na hoja hii kuwa tusimpangie rais wetu Samia, kufanya jambo lolote, lakini kukiwa na jambo lolote ambalo sio jema sio zuri sio la kupendeza, tulisema kwa nia ya kulionyeshea, na tutoe ushauri wa nini cha kufanya, huo ushauri wa kupendekeza nini cha kufanya, sio kumpangia ni kumshauri tu.

Kwa muda mrefu baadhi yetu tumekuwa tukilalamikia baadhi ya sheria ambazo zinawakosesha haki Watanzania na baadhi ya sheria hizo zinahusiana na uendeshaji wa siasa za vyama vingi nchini Tanzania. Ukilalamikia jambo fulani, ukaliangazia, wenye mamlaka wakalisikia, wakatoa kauli kuwa jambo hilo litashughulikiwa. Kitu cha kwanza ni kwa wewe uliolalamika kusema asante, kilio chako kimesikika, na kitu cha pili ni kumshukuru huyo aliyesikia kilio chako na kuahidi kushughulikia hilo jambo lako.

Baadhi ya hoja zangu kulalamikia sheria na kutaka watu tutendewe haki ni hizi
kwa wanaopenda Rejea. Kwa wasiopenda rejea you can just jump
Hii section ni kwa wapenda rejea, kama wewe sii mmoja wao, just jump
  1. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
  2. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  3. Japo Kazi ya Upinzani ni Kupinga, Lakini Sio Kupinga Kila Kitu, Kwenye Maslahi Ya Taifa, Tutangulize Utaifa, Tuwe Wamoja, Wakweli na Tusipotoshe.
  4. Pascal Mayalla: NEC ni Tume huru ya uchaguzi kama lilivyo bunge na mahakama kwa sababu vyote hivi msingi wake ni Rais
  5. Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?
  6. Je Wajua kuna Fupa Fulani la Dhulma kwa Watanzania, Liliwashinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, Jee Mama Samia Ataliweza Fupa Hili?.
  7. Kwa Kauli Hii, Rais Samia atabarikiwa sana kuliko Rais mwingine yeyote! Huu ni wema mkubwa kabisa kuwahi kuwa Rais yeyote ukimuondoa Nyerere
  8. Je, jicho la Rais Samia litauangazia Ubatili huu ndani ya Katiba yetu unaopora Haki ya Msingi, uliochomekewa kibatili ili kuuhalalisha?
  9. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  10. Kutotambua Matokeo ni Kutomtambua Rais, Serikali na Bunge. Rais Akiishaapishwa ni Rais! Tutaendelea kuruhusu hali hii Mpaka Lini?
  11. Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
  12. Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?
  13. Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.
  14. Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?
  15. Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…
  16. Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?
  17. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  18. TZ Trends & Analysis: Hoja 30 za The Economist Kumhusu President Samia. Kuna za Kweli, za Uongo na Uzushi na Kutaka Kumpangia Watakacho Mabeberu, Jee?
  19. Samia tumaini jipya Tanzania: The Economist baada ya kumsakama sana Magufuli, sasa angalau lina matumaini na Samia, laanza naye vizuri
  20. Thinking Aloud: Hongera JF kulisaidia Taifa, "Atakuwa anaingia JF in person na kutusoma!". 2021 let's be more responsible, more strategic
Wiki hii Tanzania imeadhimisha miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi nchini, vyama vingi vilipoanza tena nchini Tanzania ile 1992, umenikuta mimi tayari nina mwaka mmoja kazini, nimeanza kazi Januari 2, mwaka 1990, hivyo mfumo wa vyama vingi umenikuta kazini, mpaka leo tunatimiza miaka 30 ya vyama vingi nchini, mimi niko Newsroom, na kati ya marais 6 wa Tanzania, nimapata bahati ya kufanya mahojiano ya ana kwa ana na marais 4, maombi ya kufanya mahojiano na Samia yako njiani.

Katika hii miaka yangu 30 ya mfumo wa vyama vingi, nimefanya vipindi vingi, nimehoji watu wengi, akiwemo Mama Samia nimefanya nae mahojiano ya saa moja mara mbili, mara ya kwanza akiwa Waziri Ofisi ya Makamo wa Rais na Mara ya pili akiwa Makamo Mwenyekiti Bunge Maalum la Katiba, kuna siku nitarushia vipindi vya mahojiano hayo, hivyo kuna wengi ndio watamjua kumbe Samia na demokrasia, hakuanza leo!.

Miongoni mwa makubwa ambayo nimekuwa nikilalamikia ni sheria yetu ya uchaguzi, na makala zangu mbili zilizotangulia kabla ya leo, nikaeleza jinsi sheria hizo batili na kinyume cha katiba, zilivyokuja kuhalalishwa kwa kuchomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu hivyo kuinajisi katiba!.

Juzi katika waraka wake wa Miaka 30 ya Vyama Vingi nchini Tanzania, huku kwenye mtandao wa jamii unaoongoza nchini Tanzania, Jamii Forums, kuna makala inayosaamba inayodaiwa kuandikwa na mwandishi kwa jina la “Ameandika Rais Samia Suluhu Hassan: Miaka 30 ya Vyama Vingi - Changamoto na Mustakabali Kusonga Mbele”

Sina uhakika kama ni kweli ameandika Samia, kwasababu nimetembelea Mtandao wa :Mawasiliano Ikulu, sikuiona makala hii, ila ingekuwa ni fake, taarifa ingeishatoka kuwa hii ni fake, ila hata bila ya udhibitosho mwandishi ni Samia, maadam imesema jambo jema naomba kuinukuu.

“Nimedhamiria, kwamba kwenye kuenzi miaka yetu ya demokrasia ya vyama vingi. Serikali yangu itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi.

Lengo, ni kwamba Tanzania yetu iende na wakati na kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo, hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika.


Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi, yataleta ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza” Mwisho wa kunukuu.

Japo hii ni ahadi tuu, lakini hili ni jambo jema kwasababu tumelipigia sana kelele.

Haki huinua taifa, kwa ahadi kama hizi, Rais Samia anazidi kuthibitisha yeye ni Chagua la Mungu kwa Tanzania, na akitekeleza haya, Rais Samia, atabarikiwa na Taifa la Tanzania litabarikiwa sana!. Asante Mungu kwa Rais Samia,
Mungu Mbariki Rais Samia ayaweze kupitia YEYE.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 
Kwa Mungu hakuna Mpango wa Uovu, (CCM na mambo yake yote - mengi ni uovu)

Kwa Mungu kunatoka, HAKI, Baraka na Faraja, (kwa Magu na Samia tumeshuhudia Utekaji, Mauaji na uonevu wa vyombo vya Dola dhidi ya Wananchi hususani vyama vya Siasa na sasa Masai Eviction)

Ukweli si Magufuli wala Samia ni mipango ya Mungu. Shetani naye ana mipango yake.

Imeendikwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa MAARIFA

Acha kupotosha na kumuunganisha Mungu na Uovu.

Katubu.
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na Makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", Makala ya leo ni jinsi Rais Samia alivyo ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Rais Samia, Akifanikiwa kwenye hili, atabarikiwa sana na !, Taifa la Tanzania, litabarikiwa!. Natoa wito kwa wote wenye nia njema kwa taifa letu, sote tupaze sauti zetu katika umoja wetu kwa kumshukuru Mungu kutuletea Rais Samia, "Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania"!.

Ubarikiwe sana mkuu pascal,,
 
Kwa Mungu hakuna Mpango wa Uovu..., (CCM na mambo yake yote - mengi ni uovu )

Kwa Mungu kunatoka, HAKI, Baraka na Faraja..., ( kwa Magu na Samia tumeshuhudia Utekaji, Mauaji na uonevu wa vyombo vya Dola dhidi ya Wananchi hususani vyama vya Siasa na sasa Masai Eviction)

Ukweli si Magufuli wala Samia ni mipango ya Mungu...Shetani naye ana mipango yake...

Imeendikwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa MAARIFA


Acha kupotosha na kumuunganisha Mungu na Uovu.

Katubu.
Mambo mengi maovu sn yanafanyika
 
Vitu vinavyosumbua watu wengi sio sijui tume sijui.katiba mpya viko vitu direct mfano vikwazo kwa kupata Passport kwa watafuta fursa nje misharti waliyoweka ni ya kuomba visa ya ubalozini ambayo haiwahusu

Pili Tanzania kuruhusu watanzania kupokea pesa kupitia PayPal kwa mauzo ya online

Ukweli vyama vya siasa hasa upinzani havibebi agenda za wananchi zinakomalia agenda za viongozi
 
Back
Top Bottom