Samia awapiga ‘stop’ mawaziri kuajiri maofisa habari binafsi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,352
8,033
Rais Samia Suluhu Hassan amezitaka wizara kujibu kauli za upotoshaji zinazotolewa na wanasiasa kuhusu utendaji wa Serikali.

Katika kulitekeleza hilo, amewataka mawaziri kuacha kuajiri maafisa habari binafsi, badala yake wavitumie vitengo vya habari kutoa taarifa za Serikali.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Machi 2, 2023 wakati wa hotuba yake katika mkutano wa faragha na Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Mikutano wa Arusha (AICC).

Agizo lake hilo kwa wizara linatokana na kile alichokitolea mfano kuwa, amewahi kuibuka mwanasiasa aliyeikosoa Serikali kutumia fedha nyingi kutafuta vyanzo vipya vya maji, ilhali kuna visima kadhaa vilishachimbwa.

Amesema wizara inayohusika na hilo, ilipaswa kusimama haraka na kutolea ufafanuzi kuhusu hilo, badala ya kusubiri taarifa za upotoshaji zisambae.

“Nimewahi kuona kiongozi wa kisiasa akiilaumu Serikali inatumia fedha nyingi kutafuta vyanzo vipya vya maji kupeleka kwa wananchi, ilhali kuna visima kadhaa vilichimbwa nyuma na serikali iliviacha.

“Wizara inayohusika na hili, ilipaswa kusimama haraka kujibu kutoa facts (ukweli), fugures (takwimu) na kumueleza kwanini visima hivyo viliachwa na kwamba vimeachwa au havikuachwa,” amesema.

Mkuu huyo wa nchi amefafanua visima vilivyotajwa na mwanasiasa huyo ndiyo vilivyoisaidia Dar es Salaam wakati wa changamoto ya ukame.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka mawaziri kuacha kuajiri maafisa habari binafsi.

“Najua kila Wizara ina kitengo cha habari, vitengo hivi vinatumikaje, vipo tu vimekaa havifanyi kazi lakini bado mawaziri mmeajiri maafisa wenu habari binafsi wa kutoa taarifa zenu na si taarifa za Serikali, sasa hili tukarekebishe” amesema.

MWANANCHI
 
Namhurumia sana Bi Samia, hapo ni kama kumpigia mbuzi guitar.

Kama zipo sera na taratibu za kuendesha kila wizara na idara ya serikali, anaekiuka ni safari na kuhukumiwa na adhabu aionje, kwanini akakiuka sera na taratibu.

Kama hakuna, ziwepo.

Kazi kubwa ya bunge sio kwenda pale kupiga porojo zisizo mpango, watunge sera na taratibu za kuendesha kila kitu kwenye nchi, na kila sera itungiwe sheria na adhabu ya kuikiuka.
 
Kama zipo sera na taratibu za kuendesha kila wizara na idara ya serikali, anaekiuka ni safari nankuhujumiwa na afhabu aionje kwanini kakiuja sera na taratibu.

Afhabu- adhabu
Kakiuja- kakiuka
 
Wewe kama nani umuonee huruma amri jeshi mkuu?

Ulienda shule kusomea nini?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Rais Samia Suluhu Hassan amezitaka wizara kujibu kauli za upotoshaji zinazotolewa na wanasiasa kuhusu utendaji wa Serikali.

Katika kulitekeleza hilo, amewataka mawaziri kuacha kuajiri maafisa habari binafsi, badala yake wavitumie vitengo vya habari kutoa taarifa za Serikali.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Machi 2, 2023 wakati wa hotuba yake katika mkutano wa faragha na Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Mikutano wa Arusha (AICC).

Agizo lake hilo kwa wizara linatokana na kile alichokitolea mfano kuwa, amewahi kuibuka mwanasiasa aliyeikosoa Serikali kutumia fedha nyingi kutafuta vyanzo vipya vya maji, ilhali kuna visima kadhaa vilishachimbwa.

Amesema wizara inayohusika na hilo, ilipaswa kusimama haraka na kutolea ufafanuzi kuhusu hilo, badala ya kusubiri taarifa za upotoshaji zisambae.

“Nimewahi kuona kiongozi wa kisiasa akiilaumu Serikali inatumia fedha nyingi kutafuta vyanzo vipya vya maji kupeleka kwa wananchi, ilhali kuna visima kadhaa vilichimbwa nyuma na serikali iliviacha.

“Wizara inayohusika na hili, ilipaswa kusimama haraka kujibu kutoa facts (ukweli), fugures (takwimu) na kumueleza kwanini visima hivyo viliachwa na kwamba vimeachwa au havikuachwa,” amesema.

Mkuu huyo wa nchi amefafanua visima vilivyotajwa na mwanasiasa huyo ndiyo vilivyoisaidia Dar es Salaam wakati wa changamoto ya ukame.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka mawaziri kuacha kuajiri maafisa habari binafsi.

“Najua kila Wizara ina kitengo cha habari, vitengo hivi vinatumikaje, vipo tu vimekaa havifanyi kazi lakini bado mawaziri mmeajiri maafisa wenu habari binafsi wa kutoa taarifa zenu na si taarifa za Serikali, sasa hili tukarekebishe” amesema.

MWANANCHI
Mi nadhan sindano imeanza kuingia waliporuhusu hii mikutano ya siasa, mana facts zilizowekwa hadharan na Mhe Rungwe wa Chauma kwenye kile kpindi cha dakika 45 ITV sioni kama kuna kiongozi anaweza simama na kumjibu

Hoja za Rungwe ni nyingi na kweli tupu nilizowahi kuzisikia kutoka upinzani hata kuliko zile za Tundu Lissu wa chadema, yule mzee anajua sana madhaifu ya serikali, natamani angekuwa rais wa nchi
 
Endelea kujidanganya kama waliokua na nguvu kubwa kisiasa saa hizi hawasikiki sidhani kama hiko CHAUMA kina cha kufanya 2025 hakuna mwenye hoja wote walamba asali bora tuendelee na CCM
 
Ameamua abadili na neno kabisa badala ya kusema “ hili nalo mkalitizame “ kaamua kusema “mkarekebishe “ maana wasaidizi wake hawasikii kabisa
 
Namhurumia sana Bi Samia, hapo ni kama kumpigia mbuzi guitar.

Kama zipo sera na taratibu za kuendesha kila wizara na idara ya serikali, anaekiuka ni safari na kuhukumiwa na adhabu aionje, kwanini akakiuka sera na taratibu.

Kama hakuna, ziwepo.

Kazi kubwa ya bunge sio kwenda pale kupiga porojo zisizo mpango, watunge sera na taratibu za kuendesha kila kitu kwenye nchi, na kila sera itungiwe sheria na adhabu ya kuikiuka.
Takbriiir!.
 
Nataka nimrithi gozi.
 
Back
Top Bottom