Wote tumesikia karuhusu na kiukweli kalazimisha watu waikosoe serikali.
Tumeshaona wabunge tena wa CCM wakiwa mbele kuikosoa serikali. Hawa watataka wawazidi CHADEMA na wenzao katika kuikosoa serikali na tayari tumeona wameshaanza.
Wapinzani kama CHADEMA na wenzao nao wataendelea kukosoa huku na kule kama kawaida yao.
Magazeti yote yatafunguliwa na yatakosoa karibu kila leo, yaani MWANAHALISI, MAWIO, TANZANIA DAIMA na mengine. Humu Jamii Forum watu watakosoa kila dakika.
Matokeo yake ni nini? Kitakachotokea ni hiki. Madudu mengi yataiibuliwa kila kukicha na rais atapenda aonekane anashughulikia.
Kimsingi ni kama vile Rais Rais Samia kaitupa kazi ya uchunguzi na upelelezi kwetu na hatakuwa na kazi kubwa ya kuibua madudu kwani wabunge wataibua, magazeti yataibua, mitandao itaibua yaani yatakuwa ni mashindano ya kuibua madudu.
Yeye atafanya kazi moja rahisi sana yaani madudu yakiibuka anayashughulikia. Atawatumbua wahusika na wengine kuwapeleka mahakamani.
Matokeo yake watatumbuliwa ambao hutatarajia watumbuliwe na atakapofanya hivyo itaonekana siyo yeye aliyeanzisha bali ni madudu yaliyoibuliwa na wadau kama wewe na mimi. Hataonekana ana kinyongo au amempania mtu fulani.
Kwa mfano, tuhuma za hela kuibwa Benki Kuu wakati wa ugonjwa wa Rais Magufuli zilianzishwa na Kigogo. Rais Samia alichofanya ni kumuagiza CAG afanye auditing pale kwa transactions za kuanzia January hadi March.
Hivyo lazima madudu yatapatikana na watatumbuliwa wasiogusika na hivyo ndivyo itakuwa staili yake
Hivyo, tutegemee kuwa na rais bora kuliko wanavyodhani wengi.
Viva Samia,
Jamhuri ya Muungano, kazi inaendelea