Samia aliandikiwa kuwa Rais wa Tanzania hata kabla hajazaliwa

Kuna linalofanyika bila ya MUNGU kutaka?!!

Kama kuna mipango ya SHETANI...basi shetani hawezi kuizidi mipango ya MUNGU.....

#SiempreChifuHangaya
#SiempreJMT

Mungu yupi anaeruhusu kuroga ??ni Mungu yupi alie wahakikishia Samia atatawala mpka 2030? acheni kumchanganya Mungu kwenye mahaba yenu binafsi
 
Mungu yupi anaeruhusu kuroga ??ni Mungu yupi alie wahakikishia Samia atatawala mpka 2030? acheni kumchanganya Mungu kwenye mahaba yenu binafsi
Endelea kuishi mashimoni kifikra.....

Mungu Mwenyezi yuko juu ya kila kitu....
 
kuna muda maandiko yanafikirisha sana, hayo hayo maandiko yanatueleza mwanamke hafai kua kiongozi sa sijui tushike lipi.
 
Watu wengi walimtabiria kutawala kipindi kimoja na ikatokea. Ni ajabu kweli.
Mkuu hali ilishakua worst kila mtu akawa anafkiria huyu mtu akichkua mitano mingne itakuaje..
Kila mtu alikua anaomba jamaa amalize kile kipind chake kimoja aondoke madarakani ndo ivo mungu akampenda zaid..
 
Ongea vitu conscious kama mwanaume tena vya kuisaidia nchi badala ya kutuonesha unavyoweza kupamba mtu / kulamba miguu...msifu basi muumba wako upate thawabu
Aisee!
Kwani hapo hajamsifu muumba mkuu? Mbona km ameonyesha kunyenyekea, kuamini na kukubali maamuzi yake? Au ulitakaje?
 
Ya Mungu yanakuja na pande mbili na moja kati yao ndio inakuwa imelengwa.
  • Kukuonesha ulipokosea/kuwakumbusha njia sahihi ni ipi (kupokea malipo ya makosa mliyofanya)
  • Kuwakomboa kutoka katika njia/utawala mbovu
Sasa usimsifu kwa kuchaguliwa kwake na Mungu(kama ni kweli) pasipo kujua dhumuni la Mungu kumchagua ni lipi.
 
Mambo ya Mungu huwa ni makuu sana, nawaambieni enyi watanzania, kuna watu walibarikiwa tangu wakiwa Tumboni mwa mama zao

Samia Suluhu ni mfano hai tulionao mpaka sasa achilia mbali manabii wa zamani waliochaguliwa angali bado wapo tumboni,

Samia suluhu hakuwai kuwa mwanaharakati wala mpambanaji wa chama wala hakuwa na wafuasi na makundibya watu , alikua mpole tu na mnyenyekevu lakini jicho la Bwana kupitia Hayati Johm Magufuli lilimuona na kumchagua kuwa makamu wa Rais,

Hizo ni njia ambazo Mungu alikua anamtengenezea.

Wazee wa CCM wamesota sana kuutafuta Urais wametengeneza makundi kwa makundi wameunda makandokando wametengeneza channel ndani na nje ya nchi, wamemwaga pesa nyingi wameunda ukaribu na matajili ili tu wawe marais wa JMT imeshindikana

Lakini Samia ameukwaa Urais kiulaini tu bila gharama yyte kama kumsukuma mlevi

Samia kashika nchi ikiwa kwenye taharuki, uchumi umeyumba lakini mpaka sasa bado nchi imetulia,

Huo ni mkono wa bwana u ndani yake halleluya!

Kama si Bwana aliekua naye israel na aseme sasa!

Hakika Mungu akisema ndiyo hakuna atakayepinga, Nyote mlioko ndani ya chama na ndani ya serikali ambao kwa namna moja mnajaribu kumuhujumu Rais mtahaibika, kwa mlango mmoja mtaingia lakini mtatawanyika kwa milango saba! ni bora mcheze na sumu kuliko kucheza na chaguo la Bwana wa Majeshi,

Samia umebarikiwa kabla ya kuzaliwa kwako.

Mungu atasimama na wewe mpaka kipindi chako chote kitakapoisha 2030

watakaompinga ndani ya Chama 2025 nawapa pole, maana mtapotea kabisa katika ulimwengu wa siasa za Tanzania

Piga kazi Iron Lady, kipenzi cha watu mama wa Taifa, Samia Suluhu Hassan the Big Boss

Weka namba yako mkuu, wizara ya ulinzi kuna nafasi ya kazi
 
Aisee!
Kwani hapo hajamsifu muumba mkuu? Mbona km ameonyesha kunyenyekea, kuamini na kukubali maamuzi yake? Au ulitakaje?
Msijidai kumsemea Muumba kujidai manabii mnaooneshwa...
Vijana mjifunze kufikiri critically sio kubobea kwenye uchawa hamtoisaidia nchi
 
Back
Top Bottom