Samia aliandikiwa kuwa Rais wa Tanzania hata kabla hajazaliwa

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Mambo ya Mungu huwa ni makuu sana, nawaambieni enyi watanzania, kuna watu walibarikiwa tangu wakiwa Tumboni mwa mama zao

Samia Suluhu ni mfano hai tulionao mpaka sasa achilia mbali manabii wa zamani waliochaguliwa angali bado wapo tumboni,

Samia suluhu hakuwai kuwa mwanaharakati wala mpambanaji wa chama wala hakuwa na wafuasi na makundibya watu , alikua mpole tu na mnyenyekevu lakini jicho la Bwana kupitia Hayati Johm Magufuli lilimuona na kumchagua kuwa makamu wa Rais,

Hizo ni njia ambazo Mungu alikua anamtengenezea.

Wazee wa CCM wamesota sana kuutafuta Urais wametengeneza makundi kwa makundi wameunda makandokando wametengeneza channel ndani na nje ya nchi, wamemwaga pesa nyingi wameunda ukaribu na matajili ili tu wawe marais wa JMT imeshindikana

Lakini Samia ameukwaa Urais kiulaini tu bila gharama yyte kama kumsukuma mlevi

Samia kashika nchi ikiwa kwenye taharuki, uchumi umeyumba lakini mpaka sasa bado nchi imetulia,

Huo ni mkono wa bwana u ndani yake halleluya!

Kama si Bwana aliekua naye israel na aseme sasa!

Hakika Mungu akisema ndiyo hakuna atakayepinga, Nyote mlioko ndani ya chama na ndani ya serikali ambao kwa namna moja mnajaribu kumuhujumu Rais mtahaibika, kwa mlango mmoja mtaingia lakini mtatawanyika kwa milango saba! ni bora mcheze na sumu kuliko kucheza na chaguo la Bwana wa Majeshi,

Samia umebarikiwa kabla ya kuzaliwa kwako.

Mungu atasimama na wewe mpaka kipindi chako chote kitakapoisha 2030

watakaompinga ndani ya Chama 2025 nawapa pole, maana mtapotea kabisa katika ulimwengu wa siasa za Tanzania

Piga kazi Iron Lady, kipenzi cha watu mama wa Taifa, Samia Suluhu Hassan the Big Boss

images (1).jpeg
 
Nakumbuka kipindi Niko shule ya msingi.

Shekhe yahya husein aliwahi kutabiri hv kwamba.

Tanzania itapata raisi na huyo raisi atafia madarakani baada ya hapo raisi atakaefata atakuwa mwanamke.

Na kweli imetokea huu uzi umenikumbusha
 
Wanaoutafuta urais ni wengi Ila Wanaoupata ni kwa ajili ya MAJALIWA toka tumboni mwa mama zao.....

Ingekuwa URAIS unapatikana kwa MIPANGO YA KUUTAFUTA basi "yule Komredi" aliutafuta kwa kuweka mipango zaidi ya MIAKA 20.....🤣🤣

SIEMPRE CHIFU MKUU HANGAYA
SIEMPRE MH.RAIS SSH🙏

Mwenyezi Mungu azidi kumpa afya njema na ulinzi tele aaaamin🙏

#KaziIendelee
#SiempreJMT
#NchiKwanza
 
Ni kweli kabisa lakini Mungu anakupa uamue mwenyewe hatima yako kama Mfalme itaishia wapi? Katika Biblia wako waliondolewa wakaishi porini na kula nyasi kamba pundamilia. Sauli alinyanganywa Ufalme na Mungu wa Mbinguni. Mafanikio ya Mfalme inategemeana anampa nafasi gani Mungu.
 
Mambo ya Mungu huwa ni makuu sana, nawaambieni enyi watanzania, kuna watu walibarikiwa tangu wakiwa Tumboni mwa mama zao

Samia Suluhu ni mfano hai tulionao mpaka sasa achilia mbali manabii wa zamani waliochaguliwa angali bado wapo tumbon...
😍
 
Ongea vitu conscious kama mwanaume tena vya kuisaidia nchi badala ya kutuonesha unavyoweza kupamba mtu / kulamba miguu...msifu basi muumba wako upate thawabu
 
Mambo ya Mungu huwa ni makuu sana, nawaambieni enyi watanzania, kuna watu walibarikiwa tangu wakiwa Tumboni mwa mama zao

Samia Suluhu ni mfano hai tulionao mpaka sasa achilia mbali manabii wa zamani waliochaguliwa angali bado wapo tumboni...
Umeandika kweli tupu, Mungu amlinde Mama Samia,
 
Mambo ya Mungu huwa ni makuu sana, nawaambieni enyi watanzania, kuna watu walibarikiwa tangu wakiwa Tumboni mwa mama zao

Samia Suluhu ni mfano hai tulionao mpaka sasa achilia mbali manabii wa zamani waliochaguliwa angali bado wapo tumboni...
Ni sawa na kweli pengine Lkn Kama Ni Mungu wa kweli Basi Rais wetu atafakari jukumu lake la kiMungu hapa duniani. Yaani nje ya uraisi wake ninaamini kusudi la Mungu la kumfanya yeye awe kiongozi wetu si kuruhusu serikali yake kusingizia watu wa Mungu kesi na kutojali kuzingatia kiapo Cha kulinda katiba Kila siku analalamika polisi wanaonea watu na Ni kweli ila hachukui hatua kwa Nini? Kuna Nini? Yeye Ana dhamana na Mamlaka yote.!! Duuuu!!!!??
 
Back
Top Bottom