Samehe saba mara sabini: Kisa cha Papa Yohane Paulo II kupigwa risasi mwaka 1981

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
PAPA YOHANE PAULO II(POPE JOHN PAUL II)alipigwa risasi mwaka 1981 na raia wa uturuki aliyejulikana kwa jina la Mehmet Ali Agca.

Papa alinusurika kufa na Mehmet alikamatwa na kufungwa Maisha Lakini mwaka 1983 Papa akaenda kumtembelea Mehmet jela na kumsamehe kosa alilolifanya la kujaribu kumuua.

Papa yohane paulo jina lake la kuzaliwa alikuwa anaitwa Karol Jozef Woj Tyla alizaliwa tarehe 18 Mei 1920 na kufariki tarehe 2 April 2005.Alikuwa Papa wa 264 kuanzia tarehe 16 oktoba 1978 Hadi kifo chake akidumu kwenye huduma hiyo Kipindi kirefu kuliko Mapapa wengine wote.

Alifanya ziara ya nchi 129 dunia nzima, alitembelea nchi nyingi ambazo zilikuwa hazijawahi kutembelewa na papa yoyote,Kama vile Tanzania mwaka 1990 alipokuja Mwanza Kawekamo.

Papa Yohane alilaumu ubepari wa nchi za magharibi na kudai haki katika jamii zote,akitetea hasa uhai wa binadamu na Uhuru wa dini.U pande wa dini aliboresha uhusiano Kati ya kanisa katoliki na madhehebu mengine ya ukristo na pamoja na ule wa dini mbalimbali kuanzia Uyahudi,Ubudha na Uislamu.

Mwaka 2000 alipotembelea Yerusalemu akawa Papa wa kwanza kuhiji kwenye ukuta wa maombolezo, na alikuwa Papa wa kwanza kuingia msikitini Damasco Syria mwaka 2001. Alikuwa na miaka 58 Kipindi anachaguliwa kuwa papa na ndiye papa aliyekuwa na umri mdogo kuliko Mapapa wote waliochaguliwa baada ya Papa pius IX mwaka 1846 akiwa na miaka 54.

Papa Yohane alikuwa anaongea lugha 13 ikiwemo Kipoland, Kiitalia, kiingereza, kihispania, kireno, kiukraina, kirusi, kiserbokratia, kiesperanto, kilatini na kigiriki cha kale.

Tarehe 13 May 1981 Papa alipigwa risasi akiwa kwenye gari la wazi eneo la St Peter's square jijini Vatikani wakati akiwasalimia watu waliojitokeza kumuona.

Raia wa uturuki aliyejulikana kwa jina la Mehmet Ali Agca alifyatua risasi nne(4) ambazo moja ilimpiga mlinzi na risasi moja ikampiga papa mkono wa kushoto.Papa aliwahishwa hospitali na Mehmet alikamatwa na kuhukumiwa kifungo Cha Maisha, mwaka 1983 papa alienda jela kumtembelea na kumsamehe.

FB_IMG_1624697468377.jpg
 
Papa alifanya uduwanzi tu. ANGEKUFA ANGEENDA KUSAMEHE HUKO KUZIMU. Kila mbuzi ale urefu wa kamba yake. MIMI NINGETAKA AFE. Lissu mwenyewe hatakaa amsamehe Magu japo kafa.
 
Back
Top Bottom