Same: Watu 11 wafariki kwa ajali ya gari

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Moshi, Same. Watu 10 wamefariki katika ajali ya gari iliyotokea kijiji cha Kirinjiko Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea leo jioni Jumanne Aprili 13, 2021 baada ya gari aina ya Toyota Alphard kugongana uso kwa uso na gari jingine aina ya Toyota Noah, ni waombolezaji waliokuwa wakitoka mkoani Arusha kwenda Lushoto mkoani Tanga.

Awali Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale aliieleza Mwananchi Digital kuwa watu sita walikufa papo hapo lakini taarifa zilizomkariri mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule zinaeleza kuwa idadi ya waliokufa ni 10 na majeruhi ni 12.

Amesema abiria waliokuwamo katika Alphard walikuwa wakitokea Arusha kwenda Lushoto kwenye msiba na kwamba Noah ilikuwa ikitoka Hedaru kwenda Same.

“Alphard ilipata tyre bust (kupasuka gurudumu) ya nyuma ikayumba ikaenda kugongana na hiyo Hiace na wamekufa watu 10 na majeruhi 12. Watu 12 waliojeruhiwa walipelekwa hospitali ya wilaya ya Same.”

“Majeruhi watano wakawa na hali mbaya ikabidi wapelekwe KCMC. Hapa kwetu wamebaki watu saba ambao wanaendelea kupatiwa matibabu. Miili minne imetambuliwa na sita ndugu zao walikuwa wanaendelea kutafutwa,” amesema.

UPDATE 14/04/2021: VIFO VYAFIKIA 11

Idadi ya vifo vilivyotokea katika ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro vimeongezeka na kufikia 11 baada ya majeruhi mmoja kati ya saba waliolazwa Hospitali ya Wilaya ya Same kufariki dunia.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule amesema hali za majeruhi wawili kati ya sita si nzuri na wamekimbizwa katika katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC huku wanne hali zao zinaendelea vizuri baada ya majibu ya X-ray kuonyesha wamepata majeraha madogo madogo.

Ajali hiyo ilitokea jana wilayani Same ambapo magari mawili yaligongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu 10 papo hapo na majeruhi 12 kati ya hao sita walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same na wengine saba Hospitali ya KCMC.

Same.jpg
 
Alphad imechomoka tairi ikakosa muelekeo ndio ikagonga haisi ilio kua na abiria wanao toka hedaru kuelekea same, na hata hvyo tumepoteza majirani zetu na ndugu pia. Innalillah wainna ilayranjuin.
Duh pole kwa wote waliopatwa na kuguswa na msiba huo.
 
Moshi, Same. Watu 10 wamefariki katika ajali ya gari iliyotokea kijiji cha Kirinjiko Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea leo jioni Jumanne Aprili 13, 2021 baada ya gari aina ya Toyota Alphard kugongana uso kwa uso na gari jingine aina ya Toyota Noah, ni waombolezaji waliokuwa wakitoka mkoani Arusha kwenda Lushoto mkoani Tanga.

Awali Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale aliieleza Mwananchi Digital kuwa watu sita walikufa papo hapo lakini taarifa zilizomkariri mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule zinaeleza kuwa idadi ya waliokufa ni 10 na majeruhi ni 12.

Amesema abiria waliokuwamo katika Alphard walikuwa wakitokea Arusha kwenda Lushoto kwenye msiba na kwamba Noah ilikuwa ikitoka Hedaru kwenda Same.

“Alphard ilipata tyre bust (kupasuka gurudumu) ya nyuma ikayumba ikaenda kugongana na hiyo Hiace na wamekufa watu 10 na majeruhi 12. Watu 12 waliojeruhiwa walipelekwa hospitali ya wilaya ya Same.”

“Majeruhi watano wakawa na hali mbaya ikabidi wapelekwe KCMC. Hapa kwetu wamebaki watu saba ambao wanaendelea kupatiwa matibabu. Miili minne imetambuliwa na sita ndugu zao walikuwa wanaendelea kutafutwa,” amesema.

1618377587449.png
 
Back
Top Bottom