Same: Mfugaji Hassan Cheyavyo (43), apigwa risasi tumboni na askari wa TFS

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Mfugaji Same amenusurika kifo baada ya kupigwa risasi tumboni.

Mfugaji aliyefahamika kama Hassan Cheyavyo (43) mkazi wa kijiji cha Masandare wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro amenusurika kifo baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kupigwa sisasi tumboni na aliyedaiwa kuwa askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wakati akimfukuza kuacha kufuatilia mifugo yao inayodaiwa kukamatwa ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Chambogo uliopo wilayani Same.

Wakazi wa mtaa wa Stelingi kata ya Kisima wilayani Same wameshikwa na taharuki na msituko mkubwa baada ya kusikia milio wa risasi katika makazi yao ambapo wameeleza jinsi tukio hilo lilivyo wastua huku mwenyeki wa wafugaji wilaya ya same lekey mulakon akilaani vikali kitendo hicho.

ITV ikafika katika hospitali alikolazwa mgonjwa huyo ambapo Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo daktari Idd Juma amesema wamempokea mgonjwa huyo akiwa katika hali mbaya na kufanya juhudi za kuokoa maisha yake .

Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wilayani hapa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Same Bi, Rosemary Senyamule amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakwamba askari aleyehusika na tendo hilo anashikiliwa na Jeshi la Polisi.


Chanzo: ITV
 
Hawa ndugu zetu walioaminiwa kupewa Jukumu la kutunza na kutumia Silaha za Moto sijui wana shida gani..,
 
hivi ITV wanafikaga kila mahali kivipi?? utaskia hata tukio likitokea ndani ndani kabisa mikoani, baada ya dk 15 utaskia "ni mimi....wa ITV. inaonekana wana ajira nyingi, mm husafiri sana, siwanipe hiyo part time job? maana juzi safarini nimeshudia matukio 4 tofauti ambayo yangefaa yawe habari
 
Kazi imeanza kwa kasi.
Hakika ule usemi wa washikabunduki kua ni vilaza nakubaliana nao.
 
Back
Top Bottom