Samatta anazidi kuwaka huko ulaya

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,542
7,450

Video: Goli alilofunga Sammata

Mbwana Samatta ameendelea kuandika historia barani Ulaya baada ya kufunga kwenye mechi yake ya kwanza ya kimataifa kwa ngazi ya klabu barani Ulaya. Usiku wa Julai 14 Genk ilikuwa inacheza dhidi ya Buducnost Podgorica mchezo wa mtoano kuwania kufuzu kwenye michuano ya Europa League katika msimu huu wa 2016/17.

Pambano hilo limemalizika kwa Genk kuibuka na ushindi wa bao 2-0. Genk walianza kupata goli lao la kwanza dakika ya 17 kwa mkwaju wa penati uliozamishwa wavuni na Neeskens Kebano.

Mbwana Samatta akaihakikishia ushindi timu yake kwa kufunga bao la pili dakika ya 79 kipindi cha pili. Nyota huyo wa Tanzania alipumzishwa dakika ya 88 na nafasi yake ikachukuliwa na Leandro Trossard.

Samatta alianza kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Peter Maes akimuweka benchi Nikos Karelis anayehusishwa sana kujiunga na klabu ya Nottingham Forest ya England. Karelis aliingia dakika ya 76 kuchukua nafasi ya Kebano mfungaji wa goli la kwanza.
 
I'm not a soccer fan, but I wish him all the best
 
Ule mgoli amenikumbusha goli nilofunga mechi yangu ya mwisho ya soka huko ulaya.
Ilikua kati ya timu yangu ya Sheffield united na Nottigham forest.
 
Safi sana kijana wetu... Ni muendelezo mzur sana ,natamn siku awe kama aubumeyang.ila akilewa sifa tu nadhan atamalizia soka lake mchangani
 
Ulaya kucheza mpira sio kazi kubwa kama Africa... Kwa sababu ya miundombinu....tatizo ni wao kukibali kama wewe kutoka Africa ni bora kuliko wako....samatta kama mwafrika mwingine anatakiwa kuujua ubaguzi wa rangi ndio unaofanya waafrica wengi wasidumu kwa viwango vyao....akitambua hilo samata atakua moja wa washambuliaji bora ulaya...katiba kipindi cha miaka 2ijayo....sababu kubwa ..naona inayomfanya kufikia hapo....ni shabaha ya kurenga gori na kucheza na mwili wa adui na kuweza kupita....na uwezi wake wa kufunga magori....goal score... Ulaya ukiwa na hiyo tarent ...wewe basi ...namfanaisha sana na samweli eto wa Cameroon.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom