Samaki waliokufa ufukweni Dar, hawakufa kwa sumu - Waziri

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ametoa ripoti ya uchunguzi wa samaki walionekana wakizagaa katika fukwe za Hospitali ya Aga Khan na Ocean Road, akisema hawakufa kwa sumu.

Tukio la samaki kilogramu 164 kuonekana kuzagaa katika maeneo hayo lilitokea Julai 21 mwaka huu, ambapo Serikali ilichukua sehemu ya sampuli ya samaki hao kwa ajili ya kupeleka maabara kuzifanyia uchunguzi huku 156 zikiteketezwa.

Katika maelezo yake, Ndaki amesema katika uchunguzi wao walibaini aina tisa samaki hao waliokuwa wamezagaa ambao ni kui, mkizi, janja, tambanji, chaa, kuku bahari, kolekole pandu, kaa, kambamiti na kambakochi.

“Kwa ujumla, samaki hawa hupatikana kwenye kina kifupi cha maji na wengi wao walikuwa wachanga. Sehemu kubwa ya matumbo ya samaki hayakuwa na chakula, ingawaje kui, mkizi na tambanji walikutwa na dagaa, kaa na uduvi katika matumbo yao.

“Samaki waliochunguzwa walikuwa na hali nzuri, ngozi ilikuwa haikutatuka na ikiwa na rangi angavu, macho yao yalionekana meusi na angavu, na mapezi yalikuwa angavu bila utelezi. Walikuwa na nyama imara na hakukuwa na harufu mbaya,” amesema Ndaki katika mkutano wake na wanahabari leo Jumatano Julai 28, 2021 Dodoma.

Ndaki amesema hatua hiyo inaondoa uwezekano wa vifo vyao vimetokana na sumu au vilipuzi. Hata hivyo, samaki wengi walionekana kuwa na midomo wazi kuashiria kuwa walikosa hewa au walikufa wakitafuta hewa.
 
Hayo ni matokeo ya Ocean Deoxygenation...

Kwa mazingira ya kwetu, inawezekana inatokana na uchafuu kujaa baharini na kusababisha polution.
... Tuna wizara inayohusika na mazingara na Nemc pia ipo. Hebu tuwasikilizie nao watakuja na story gani.
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ametoa ripoti ya uchunguzi wa samaki walionekana wakizagaa katika fukwe za Hospitali ya Aga Khan na Ocean Road, akisema hawakufa kwa sumu....
Wanashindwa kuchuguza maiti za samaki na kuja na report kamili ndo muweze kuchuguza chanjo ya corona......hizi ni nchi masikini kweli kweli na wana sayansi uchwara.
 
Walikufa na nini sasa? Mbona ni bla bla tu haijasema lolote?
We ndo kilaza mkuu
Taarifa imesema hawakufa kwa sumu it means uchunguzi umebaini hawakuwa na sumu ila kwa sababu ulitaka kukomenti haraka haraka hukujipa muda wa kutafakari hilo.

Shida yetu watanzania tunasikiliza au tunasoma ili tujibu sio kuelewa kwanza.
Sasa wewe unaweza pingana na Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali?

We unaweza kupingana na Maabara ya Uvuvi ya Taifa?

Unaweza kupingana na maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania?
 
Ujenzi wa daraja haujachangia? Nemc hawana majibu?
... Hoja fikirishi! Hebu waweke ripoti ya upembuzi yakinifu public haraka sana. Daraja linaharibu mazingira. Sijui kule Selous hali ikoje pamoja na kelele zote za "kibeberu" zilizopigwa kipindi kile.
 
Wanashindwa kuchuguza maiti za samaki na kuja na report kamili ndo muweze kuchuguza chanjo ya corona......hizi ni nchi masikini kweli kweli na wana sayansi uchwara.
.... Ha ha ha. Walikutwa na minofu imara, mapezi hayatelezi ila midomo wazi. Conclusion: walikosa hewa. That simple!
 
... Kwa nchi ambazo brains zinafanya kazi ni concern kubwa sana. Ni interest kubwa mno ya research institutions na papers za kutosha zingechapwa. Ila kwa hapa herd immunity inaachwa ifanye kazi yake hata wakiisha wala sio big deal.
Kwetu bla bla tu...
 
Water pollution

Haijatazamwa kama hapana basi tuseme walipata rimonia
ni aibu sana eti viumbe wafe useme walikosa hewa

Sawa walikosa hewa
Tupewe jibu nn kilipelekea wafe kwa kukosa hewa
 
We ndo kilaza mkuu
Taarifa imesema hawakufa kwa sumu it means uchunguzi umebaini hawakuwa na sumu ila kwa sababu ulitaka kukomenti haraka haraka hukujipa muda wa kutafakari hilo.

Shida yetu watanzania tunasikiliza au tunasoma ili tujibu sio kuelewa kwanza.
Sasa wewe unaweza pingana na Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali?

We unaweza kupingana na Maabara ya Uvuvi ya Taifa?

Unaweza kupingana na maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania?
Mzee umejitahidi kujibu...ila umejibu ujinga sana...kwahiyo imetumika wiki moja kuja na jibu samaki wamekufa bila sumu wakati katika kilo 164 hao 154 wametupwa....unajua implication yake.........kwanini wasingegundua ile siku wavuvi wakapata kitoweo....tuambiwe chanzo kama ni vilipuzi,daraja,uchafuzi au.?nemc wenyewe ujinga wao wanawaza kufunga mabar tu yanayopiga kelele
 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ametoa ripoti ya uchunguzi wa samaki walionekana wakizagaa katika fukwe za Hospitali ya Aga Khan na Ocean Road, akisema hawakufa kwa sumu.

Tukio la samaki kilogramu 164 kuonekana kuzagaa katika maeneo hayo lilitokea Julai 21 mwaka huu, ambapo Serikali ilichukua sehemu ya sampuli ya samaki hao kwa ajili ya kupeleka maabara kuzifanyia uchunguzi huku 156 zikiteketezwa.

Katika maelezo yake, Ndaki amesema katika uchunguzi wao walibaini aina tisa samaki hao waliokuwa wamezagaa ambao ni kui, mkizi, janja, tambanji, chaa, kuku bahari, kolekole pandu, kaa, kambamiti na kambakochi.

“Kwa ujumla, samaki hawa hupatikana kwenye kina kifupi cha maji na wengi wao walikuwa wachanga. Sehemu kubwa ya matumbo ya samaki hayakuwa na chakula, ingawaje kui, mkizi na tambanji walikutwa na dagaa, kaa na uduvi katika matumbo yao.

“Samaki waliochunguzwa walikuwa na hali nzuri, ngozi ilikuwa haikutatuka na ikiwa na rangi angavu, macho yao yalionekana meusi na angavu, na mapezi yalikuwa angavu bila utelezi. Walikuwa na nyama imara na hakukuwa na harufu mbaya,” amesema Ndaki katika mkutano wake na wanahabari leo Jumatano Julai 28, 2021 Dodoma.

Ndaki amesema hatua hiyo inaondoa uwezekano wa vifo vyao vimetokana na sumu au vilipuzi. Hata hivyo, samaki wengi walionekana kuwa na midomo wazi kuashiria kuwa walikosa hewa au walikufa wakitafuta hewa.
MBONA MTU AKISOMA HADI CHINI INAONEKANA HAMNA JIBU SAHIHI..
 
Back
Top Bottom