Samaki Wakasirika

ukara

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
285
168
Samaki hao watoka majini kwenda kuwaona ndugu zao wa sokoni. Wadai kuwa kuendelea kunyamaa kunawaongezea ndwele.

Kwa sauti moja wanapaza sauti zao wakisema "Tumenyanyaswa kiasi cha kutosha, Tumeonewa kiasi cha kutosha, Tumepuuzwa kiasi cha kutosha, Tumedharauliwa kiasi cha kutosha, Tumedharirishwa kiasi cha kutosha, Tumenyonywa kiasi cha kutosha, Tumeumizwa kiasi cha kutosha, Tumeuawa kiasi cha kutosha, Tumedhihakiwa kiasi cha kutosha na Tumedanganywa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliosababisha haya yote." Lakini swali la msingi ni "Nani anajali kilio chao? Nani asimame apaze sauti kwa niaba yao ili sauti hiyo ipenye katika kuta nzito za masikio ya watesi wao? Nani anajali?" Kweli kilio cha Samaki machozi yamekwenda na maji
 
Mkuu, wewe ni mwalimu wa fasihi chuo kikuu?Nimekupata lakini!Na huyo anaewala samaki anachekaaa, anajiandaa kuwala hao wote wanaolalamika!
 
Samaki hao watoka majini kwenda kuwaona ndugu zao wa sokoni. Wadai kuwa kuendelea kunyamaa kunawaongezea ndwele.

Kwa sauti moja wanapaza sauti zao wakisema "Tumenyanyaswa kiasi cha kutosha, Tumeonewa kiasi cha kutosha, Tumepuuzwa kiasi cha kutosha, Tumedharauliwa kiasi cha kutosha, Tumedharirishwa kiasi cha kutosha, Tumenyonywa kiasi cha kutosha, Tumeumizwa kiasi cha kutosha, Tumeuawa kiasi cha kutosha, Tumedhihakiwa kiasi cha kutosha na Tumedanganywa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliosababisha haya yote." Lakini swali la msingi ni "Nani anajali kilio chao? Nani asimame apaze sauti kwa niaba yao ili sauti hiyo ipenye katika kuta nzito za masikio ya watesi wao? Nani anajali?" Kweli kilio cha Samaki machozi yamekwenda na maji
Kwa hiyo unamaanisha mvuvi amesikia kilio chao
 
Nakumbuka kuna raisi mmoja wa kule Zanzibar aliwahi kuwambia jamaa flani hivi kuwa akili zao kama za samaki. Namie leo nikiunganisha dots napata picha hapa, you mean the same thing he spoke about....
 
Back
Top Bottom