Samaki waelea ufukweni Dar. Serikali yachunguza chanzo…

Naamini katika mazingira hao ni kwamba wamekufa,

Hivi kweli mtu unakuta samaki kafa mwenyewe unabeba ukalee???
Huku ni kuendekeza njaa kulikopitiliza,

unafika nyumbani na lijibesi lako unajifanya umetoka kununua samaki kumbe umeokotaaa, ukiua familia???
Eti familia imelazwa au imekufa(yote hatuombei yatokee) kisa pelege????

Hofu yangu ni hao samaki kuingizwa kitaa na kuuzwa. Maana raia tunanunua tu pasipo kujali. Ukikuta wamepangwa utachagua tu pasipo kujua kama wameokotwa na hawajavuliwa.
 
Mpo busy kuandika barua mara sijui sample imepekekwa huku ishu ya emergency kwa maisha ya watu ilitakiwa jana hiyo hiyo kuwe na majibu...huku wananchi wakiendelea kuwaokota na kuwauza..
 
Hilo tumezoea kule ziwani, kuna kipindi samaki hasa sangara huwa wanaelea, ni kwenda kukamata tu unaenda na kitoweo nyumbani bila nyavu yaani. Wenyewe wanasema wanakuwa wamekosa hewa ya kutosha ndani ya maji ila kwa baharini sina experience.
Sawa kabisa.hicho kipindi wanaita kiferezi.ata mwaka huu mwezi wa pili na tatu walikufa sangara wengi sana.
 
Maeneo ya Ufukwe wa Bahari kuanza nyuma ya Hospital ya Agha Khan, viwanja vya Gymkhana mpaka nyuma ya Ikulu kuelekea soko la Feri.

Kuna Samaki wengi wamekufa, wanaokotwa na wananchi na kuelekea soko Feri kuuzwa.

TAHADHALI KWA WANANCHI SAMAKI HAO BADO HAWAJATHIBITISHWA KAMA WANAFAA KWA MATUMIZI YA BINADAMU. NI VIZURI TUKAJUA NINI KILICHOWAUA.

CHUKUENI TAHADHARI.
 
Ni vema kuepuka kitoweo cha samaki wa maji bahari kwa siku mbili tatu hizi hasa kutoka kwa wachuuzi mitaani
Mama ntilie
Migahawa na mabanda ya chakula
Michemsho ya samaki kwenye vilabu vya pombe
 
Mbona tunaona picha ya barua hatujaona picha ya samaki wakiteketezwa na mashuhuda
 
Back
Top Bottom