Samaki wa Magufuli wafufua mgogoro wa muungano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Samaki wa Magufuli wafufua mgogoro wa muungano?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Dec 28, 2009.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  waziri Hamza wa zanzibar leo kwenye Tv anasema zanzibar inastahili ipewe share ya 40% kwa sababu sheria inasema hivyo.

  jee huu ni mgogoro mwengine ktk muungano?

  jamaa anasema waziri magufuli alikuwa anatakiwakae na mwenziwe kabla ya kuamua lkn katumia ubabe kwa hio wao watakaa na waangalie cha kufanya
   
 2. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,397
  Likes Received: 3,723
  Trophy Points: 280
  Saidia...Magufuli Pombe kasema nini juu ya hao samaki hadi hawa jamaa waongee hivyo...??
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wazanzibari bwana, chao kinakuwa chao wenyewe wala hawatushirikishi, lakini chetu wanataka asilimia 40? Zanzibar kuna watu wasiozidi milioni moja, bara tuna watu milioni 40 halafu watake asilimia 40? Hivi hawa siyo wachawi kweli?
  Ninachojua mimi ni kwamba watanzania wote walitangaziwa kuomba hao samaki iwapo wanawahitaji, sasa wenyewe hawakuomba, wanataka wapelekewe? Wao ni akina nani hadi tuwabembeleze hivyo? Sometimes huu muungano ni kero tupu. Uvunjike tu wala hautusaidii. Nichagueni mimi niwe Rais ili niuvunjilie mbali huo muungano.
   
 4. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Vipi wasiombe kulipia 40% ya storage charges!? Wazanzibari bwana!
   
 5. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,397
  Likes Received: 3,723
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa wala siwaelewi....... yaani wao kulalama tuuu....... hiyo storage charge hawaizungumzii kabisaaaa.....!!!!! Mafuta wanataka 100%
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hawa wamezungukwa na maji kila upande, na chakula chao cha kila siku ni samaki, lakini hawaridhiki hadi wawapate hao wa makufuli...huu ni utoto dizaini...huh!
  Au watu wa pwani nielezeni, jodari ni mtamu kuliko CHANGU?
   
 7. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hapana sio utoto wala njaa. kutokana na kumsikiliza bwana hamza waziri wa zanzibar kuna sheria inayozungumzia kuhusu masuali ya bahari kuu ambayo inasema kuwa mgawo wowote wa mali za bahari kuu uwe 40 to 60.

  na masuali hayo kwa vile sio mambo ya muungano kwanza ilipaswa mawaziri wawili wa Tanzania yaani Tanganyika na zanzibar wakae waongee ni jinsi gani ya kufanya na sio waziri mmoja ajifanye kuwa ana nguvu za maamuzi dhidi ya mwengine.


  nnachokiona ni zanzibar sasa wanatafuta bifu, na hapa wamekamata kipengele cha sheria inayohusiana na bahari kuu.

  huu moto naona umeanza kuwaka tena
   
 8. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Omba Mungu Muungano udumumu ili muendelee kunufaika na vya Bahari Kuu lakini ukivunjika leo tunarudisha mipaka-Please ielewe mipaka ya Tanganyika yako katika Bahari ya Hindi!!!!! Watu wanachojivunia ni Tanzania na siyo Tanganyika na Tanzania haiwezi kuwepo bila nchi Zanzibar. Hivi hujafahamu tu wale wa Maandalizi (Nursery)wanafahamu hivyo.
   
 9. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Watanganyika ni waroho sana, samaki, mafuta kila kitu wanataka kula wao tuu.Muungano uvunjike, wazenji hatutaki miungano ya kizushi zushi!

  Watanganyika anzeni kampeni za kuwapigia kelele viongozi wengu wavunje muungano, hauna faida si ndio mnavyo dai?

  Hata Pinda alijikaza kisabuni bungeni kudai ukivunjika Zenji itasaga mawe, sasa anasubiri nini?
   
 10. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  naomba kufahamu,
  Eneo la bahari ambalo ni sehemu ya Zanzibar linafikia asilimia 40?
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mimi nashauri wapewe samaki woote meli nzima kama watahitaji!binafsi wazenji nimeanza kuwachoka,because THEY ARE TOO DEMANDING
   
 12. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mkuu Geoff hivi mtu kudai haki yake kisheria ni kosa ? jee ikiwa kweli ziko sheria ambazo zinatoa muongozo wa kuendesha mambo ya mungano na kuna kundi moja kwa ubabe linafanya litakavyo kwa kujiona wao wana eneo kubwa la ardhi na watu wengi na kukiuka sheria liachwe? jee huu ndio utawala bora ?

  kwa nn Tanganyika inavyoibinya Zanzibar hamsemi kitu? kuna mengi ambayo wazanzibar wamekula kobis ila sasa naona mambo yatakuwa mambo.

  kwa muelekeo huu tutafika kwa haraka tunapopataka.

  hewalla bwana imeisha zama zake, yakhe wankanyaga yakhe npisha npumue ipia imeisha zama zake.


  sasa tunaenda inavyotaka Tanganyika. Tunataka watu waelewe Tanganyika sio Tanzania kama wengi walivyozoea
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Walianza kumalizana na kushikana uchawi wenyewe kwa wenyewe sasa wameshaeneza sumu mpaka bara.
  Nilishasema kuwa ktk kipindi hiki kuna jambo tena la siri linaendelea kupangwa huko zenji kama tusipokuwa makini na hawa wazee wa chaza watakuja na kitu ghafla na tutashindwa pa kutokea.
  Muungano kwao si mali kitu tena kwani nje ya muungano wanaweza kutengeneza usultani wa kutawala milele visiwani. hawapendi kupokezana madaraka hawa.
  Yangu macho
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  UNAWEZA KUTUSAIDIA KITU KIMOJA KAKA...!tunaomba wewe au INVISIBLE mui-upload sheria ya muungano hapa!...tunaweza jadili kwa hoja za msingi
   
 15. Bernard Rwebangira

  Bernard Rwebangira R I P

  #15
  Dec 28, 2009
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mbona sikuwai kuwasikia toka siku wamekamatwa samaki hawa? iweje leo? ama kweli mchuzi mtamu jaman teh, teh, teh

  bila shaka wako tayari kulipia na gharama za utunzaji kwa 40%, au sio ndugu zetu?
   
 16. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Halafu Magufuli alisema samaki wataliwa na watanzania sio kuuzwa ila ni zile taasisi zilizopendekezwa yaani magereza, shule, mahospitali n.k au wao Zanzibar sio Watanzaniia mbona hawakupeleka hayo maombi yao basi? Au ndio hivyo kutafuta choko kila kukicha kwa kisingizio cha Muungano?

  Walipokamatwa hawakusema, waliposemekana watauzwa hawakusema, kesi iko mahakamani wachangii hata mawazo hata kutoa sifa kwa Magufuli kwa kazi kubwa aliyofanya ya kukamatwa kwa hizo samaki, Taasisi zinazotaka samaki wa bure leteni maombi na muda maalumu umetolewa hatujasikia taasisi za Zanzibar zimepeleka maombi ndio kwanza nasikia wanataka mgao wa 40% kama nani? Zanzibar au Taasisi iliyopo Zanzibar au watanzania wa visiwani au tena ni masuala ya Muungano. Mmh mimi sielewi.
   
 17. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  hata bado hamjawachoka, just wanabeep tu. ila wakipiga hapo lazima muamue kupokea au kuzima simu kabisa.

  kwa kweli wazanzibari wanaona huu muundo unahitaji serious discussion sasa kila wanapopata nafasi hutuma hio message. ukweli zanzibar hawahitaji hao samaki na hasa walivyokuwa wamekaa kwenye mafriji muda wote huo. kwao samaki sio issue ndio mboga yao kuu, ila kwenye neno kuna neno tena nene
   
 18. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wewe kwali ni mtu wa pwani unafahamu malengo yetu huko visiwani, JK anakimbia kujadili muungano.

  Sasa tunatumia sheria hizo hizo zilizopo, hadi museme sasa muungano basi!
   
 19. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wadanyika wametaka Zenji ipeleke ombi la kuomba samaki kama vile mtoto yatima, wakati ni haki yao kikatiba kupewa kitoweo...teh teh teh!
   
 20. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #20
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Huu Muungano una kero kweli kweli, ningekuwa na uwezo ningeuvunjilia mbali ili nchi ile cha kwao. Naanza kuona kama vile Mtikila alikuwa sahihi kudai kuwepo kwa taifa la Tanganyika ambayo ingekuwa ni njia nzuri ya kuelekea kuvunja muungano huu.

  Baadaye hata Tabora nao watasema ilikuwaje samaki hao waishie Dar tu wakati Tabora nayo ni saehemu ya Tanzania? Hili dai la kutaka mtu atoke Zanzibar aje Dar kujadili swala la matumizi ya samaki wale, kitu ambacho kinaweza kutolewa maamuzi na mtu mmoja kama ilivyotokea ni kuonyesha jinsi gani tunavyopenda kutumia muda na raslimali za serikali vibaya.
   
Loading...