Samaki wa bure

Icon Special

JF-Expert Member
Mar 14, 2019
257
230
Niliwahi kusikia kuwa maji na mafuta havichangamani, na pia mafuta huwa yanaelea juu ya maji.

Basi jana mimi nikaamua kupaka mafuta mengi tu miguuni kisha nikaingia baharini ili niweze kutembea juu ya maji maana nilihisi ningeelea na kuweza kufanya chochote.

Sikumbuki nini kilitokea lakini nilijikuta nimelala mchangani watu wakiwa wamenizunguka huku wakisema niwashukuru sana wavuvi.

Nadhani watakuwa wamenipa samaki wa bure.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom