Samaki sio wa kuokota Kama senene/ kumbikumbi

karue

Senior Member
Oct 31, 2018
191
347
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri.
Kuna hii tabia ya watu wa mikoani ambapo hakuna ziwa Wala bahari Wana tabia ya kuagiza vitu utadhani vinakwenda kuokotwa tu

Unakuta mtu anakwamba ukirudi kutoka Mwanza naomba uniletee samaki na dagaa kwani wa uko ni watamu Sana
Pengine hata shilingi mia moja hajakupa

Maisha ya 1990 siyo sawa na maisha ya 2000, tubadilike ukitaka kitu kutoka sehemu fulani toa pesa uletewe

Ni Mimi Karue kutoka Bugolola Ukerewe
 
Kaka umeamua kuja kunitangaza JF kuwa nimekuagiza sangara.
Ngoja uje home hautakula michembe yetu🚶‍♂️
 
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri.
Kuna hii tabia ya watu wa mikoani ambapo hakuna ziwa Wala bahari Wana tabia ya kuagiza vitu utadhani vinakwenda kuokotwa tu

Unakuta mtu anakwamba ukirudi kutoka Mwanza naomba uniletee samaki na dagaa kwani wa uko ni watamu Sana
Pengine hata shilingi mia moja hajakupa

Maisha ya 1990 siyo sawa na maisha ya 2000, tubadilike ukitaka kitu kutoka sehemu fulani toa pesa uletewe

Ni Mimi Karue kutoka Bugolola Ukerewe
Hawana tofauti na wanaume wa Dar !! Mikoa mingine wanaiona ni kijijini, ukisema unakwenda kumtembelea anakuagiza vyakula kama mahindi,maharage na hata kuku,yeye akija kukutembelea haji hata na kg moja ya sukari !!!
 
Hii mada ni ndogo ila nimeitunuku kuwa mada bora ya mwezi.
Mtu ukiwa mkoa fulani ukiwajulisha ndugu na jamaa kuwa unaenda mkoa wao basi watakuagiza bidhaa zinazopatikana huko lakini hela hawakutumii na ukijiongeza kununua ukitegemea wakupe hela ukifika ujue imekula kwako.
Hizo bidhaa hata kama zipo nyingi kiasi gani bado haziwezi kupatikana bure bali kwa pesa nafuu tofauti na maeneo mengine.
 
IKIKUPENDEZA wapelekee,inajenga na kudumisha undugu,ujamaa,urafiki na mahusiano
Si vibaya pia kuwaeleza mfuko hauruhusu.
Binafsi hua siombwi ila naletaga na kugawa kwa majirani Bila kugombea na kwa hela yangu.
Na enjoy Hali hii
 
Huu usawa hauki sawa
 
Hawana tofauti na wanaume wa Dar !! Mikoa mingine wanaiona ni kijijini, ukisema unakwenda kumtembelea anakuagiza vyakula kama mahindi,maharage na hata kuku,yeye akija kukutembelea haji hata na kg moja ya sukari !!!
Kabisa kabisa
 
Hii mada ni ndogo ila nimeitunuku kuwa mada bora ya mwezi.
Mtu ukiwa mkoa fulani ukiwajulisha ndugu na jamaa kuwa unaenda mkoa wao basi watakuagiza bidhaa zinazopatikana huko lakini hela hawakutumii na ukijiongeza kununua ukitegemea wakupe hela ukifika ujue imekula kwako.
Hizo bidhaa hata kama zipo nyingi kiasi gani bado haziwezi kupatikana bure bali kwa pesa nafuu tofauti na maeneo mengine.
Nashukru kwa kulitambua ilo
 
Juzi watu wamesikia nipo mtwara kila mtu ananiambia nimletee eti korosho utafikiri kule zinapatikana bure wakati robo kilo ni Tsh.10,000/= bei ambayo hata hapa Dar uwa ni hiyo hiyo katika ma super markert na mtaaani.Ebu tuache hizo tabia.
 
Sikuhizi aidha hakuna tofauti au kuna tofauti ndogo sana ya bei ya Samaki na vyakula kati ya mijini / jijini na vijijini.

Pia uhitaji wa vitu hivyo ni mkubwa na wafanyabiashara wamekuwa wengi sana

Maisha yamebadilika kwakweli, tujiongeze.
 
Dar ukitaka uheshimike kama mkuu wa Kaya nenda umewafungashia chakula ama kwa hakika watakulamba miguu
 
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri.
Kuna hii tabia ya watu wa mikoani ambapo hakuna ziwa Wala bahari Wana tabia ya kuagiza vitu utadhani vinakwenda kuokotwa tu

Unakuta mtu anakwamba ukirudi kutoka Mwanza naomba uniletee samaki na dagaa kwani wa uko ni watamu Sana
Pengine hata shilingi mia moja hajakupa

Maisha ya 1990 siyo sawa na maisha ya 2000, tubadilike ukitaka kitu kutoka sehemu fulani toa pesa uletewe

Ni Mimi Karue kutoka Bugolola Ukerewe
Agiza Ukara kwa bei ya jumla, kisha wakaushe wapelekee nyumbani. Ukifika mpe shemeji awagawie majirani hata mmoja mmoja, inaleta heshima Mjini.
 
Back
Top Bottom