Samaki akimla mtu ndio habari ila mtu akila samaki sio habari hio(copy & paste)

Madihani

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
5,972
6,605
SAMAKI AKIMLA MTU NDO HABARI ILA MTU AKILA SAMAKI SI HABARI HIYO.

NA SHITINDI VENANCE

Kesho asubuhi na mapema ninaratiba ya kwenda centro ya hapa kwetu mbeya ili nikawaone waalimu wa shule ya mbeya sekondali walioswekwa lupango kwa kosa la kumpiga mwanafunzi mithili mwizi.

Kiukweli katika hili mm binafsi siungi mkono kipigo cha kikatili kilichotolewa na walimu hawa kwa mwanafunzi haswa kwa sababu dhaifu inayotolewa kuwa hakufanya kzi ya kiingeleza iliyotolewa.

Licha ya ukweli huu bado hatua zilizochukuliwa dhidi ya waalimu hawa zimekuwa ni zakukurupuka mno na kwa kiasi kikubwa hatua zimetolewa kwa msukumo wa watu katika mitandao ya kijamii badala ya kufata taratibu za kiutumishi na haswa ikizingatiwa kuwa hawa ni wanafunzi wa vyuo vikuu na walikuwa katika mafunzo kwa vitendo.

Ukiwa katika mafunzo unakuwa chini ya uangalizi maalumu na nimajukumu ya yule unayekuwa chini yake kukukosoa na kukurekebisha pale unapokwenda ndivyo sivyo.
Kwamaana kuwa vyuo vikuu na wakufunzi ndio walitakiwa kuchukua hatua za kitaaluma dhidi ya wanafunzi hao ikiwemo kurudia mafunzo kwa vitendo.

Lakini cha kushangaza wanaochukua hatua dhidi ya wanafunzi ni waziri wa mambo ya ndani na waziri wa elimu jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa kawaida na wakitaaluma

RAI YANGU
swala hili lisiendeshwe kimihemko na badala yake tufate utaratibu wa kitaaluma ili kuweza kushughulikia suala hili badala ya kutumia mihemko na mashinikizo ya mitandaoni.

Elimu ya juu na vyuo vikuu viwe huru katika maamuzi yake na hatua za kitaaluma ndizo zionekane kutawala katika sakata hili badala ya kuwaachia wanasiasa kufanya siasa katika hili

Tuwape hakiyao ya asili ya kusikilizwa waalimu haw waliohusika na sakata zima haswa wale ambao mpaka sasa wameshapewa kila aina ya hukumu kwani wameshaswekwa ndani na wakati huohuo wameshafukuzwa vyuo hata kabla ya kusikilizwa na bodi za vyuo vyao.

MWISHO
Elimu ni kumpa mtu maarifa ya jambo fulani kama hakuelewa hafungwi wala kufutwa kwenye mfumo wa elimu.

ALIYEMTOA MTU MACHO KAPELEKWA MAHAKAMANI LAKINI MWALIMU ALIYEPIGA VIBAO AMESHAHUKUMIWA TAYALI.

TUNAHITAJI KUJIFUNZA MENGI KUPITIA SWALA HILI.

SHITINDI VENANCE
VOICE OF VOOICELESS
0759704444
 
tatizo nyie walimu hamjui we kimekupeleka kupiga au mshahara......
 
Mwalimu andaa
1, scheme of work
2. Andaa andalio LA soon
3, kuwa na lesson notes
4, kuwa na bank of question

Baada ya hapo
ingia darasan fundisha toa mazoezi ikifka muda wa kuazibu acha hizo mambo ondoka huwezi kukosa mshahara kisa tuu haukuazzibu Toto la MTU mana ukiwa unaadhibu ndio ibilisi anapo tokea unapiga Toto harafu linakujibu hovyo hapo unaweza kupiga zaid ya msigwa

Na nyie wanafunzi mnao enda kwenye mafunzo bila vitendo hakuna marks zinazo tolewa kwa kupitia kipengere cha kuazibu hiko hakipo epukeni ibirisi

Na serikali kuna Mwl alipigwa na Afsa takukuru hatuja sikia hata kulaani hasa mawaziri wote hapa Ndalichako mwalimu wako alipigwa Tena kwenye uhakiki ukabaki kimyaaaaa

walimu jitahidini muombe kuhudumiwa na wizara moja sasa ona Jana Simbachawene katoa maagizo, Ndalichako nae katoa maagizo, Mwigulu nae katoa maagizo sasa huelewi Mwl anahudumiwa na Nani na wizara gani Nani atamaliza swala la hawa walimu ipi mipaka ya kila mmoja kwa Mwl

Chama cha walimu nyinyi ndio mkae kimyaaaaa
 
Back
Top Bottom