Samahani wenye nchi, je siku hizi VETTING hazifanyiki kabla ya teuzi?

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,193
6,381
Habarini wanajamvi, kwanza kabisa niwapongeze wale ambao hawalali usiku na mchana kwa kazi kubwa na nzito ya kizalendo kuhakikisha Taifa letu lipo salama kabisa.

Siku za karibuni kumetokea utenguzi wa teuzi mda mchache sana baada ya mhusika kuteuliwa, mpaka sasa yameshatokea kama matukio 3 au 4 hivi. Sababu ni kinachoonekana ni makosa katika uteuzi, lakini kwa uelewa wangu mdogo teuzi serikalini huwa kuna utaratibu unaojulikana kama Vetting ambao kwa ufupi ni kuangalia kama mhusika anafaa kwa hiyo nafasi, na utaratibu huo hufanywa na Usalama wa Taifa. Sasa ninachoshangaa inakuaje ndani ya mda mfupi teuzi hizo 3 zinaonekana kama hazikufanyiwa huo utaraibu au haikuanyika viuri au sijui ilikuaje. Nakubali kuna nafasi ya makosa ya kibinadamu lakini mara 3 ni nyingi ndani ya kipindi cha miezi 6, na hii ya mwisho mtu kaingia mpaka Ikulu kimakosa, jambo ambalo kwa uelewa wangu mdogo ni Hatari Kiusalama.
 
Vetting makini ilikuwa ni kipindi cha J Nyerere hadi Mkapa. Kwa sasa ni self vetting ya Mkulu. Na hata huko kwa wenye kufanya vetting kama una mkono mtupu hupati kitu. Ndio maana unaweza kushangaa ma-DC wengi wateule walishajua wameteuliwa na wengine walidiriki hata kubadili miondoko. Mimi nawajua watatu waliojua ni maDC na wilaya zao. Mmoja anakuja wilayani kwangu. Hivyo kifupi VETTING siku hizi ni utashi wa Mkulu au jitihada za anayetaka kuteuliwa!
 
Vetting kwa sasa ipo hadi dakika ya mwisho,napongeza sana kwamba rais yupo macho muda wote,maana mtu waweza kugundua dosari,inamaana uogope kutumbua kuwa utaambiwa hukuwa umepitia vilivyo profile ya mteuliwa?hiyo si kweli,ni kwamba watu wakiteuliwa wajue kama walivyoteuliwa ghafla wanaweza tumbuliwa ghafla.
 
Vetting makini ilikuwa ni kipindi cha J Nyerere hadi Mkapa. Kwa sasa ni self vetting ya Mkulu. Na hata huko kwa wenye kufanya vetting kama una mkono mtupu hupati kitu. Ndio maana unaweza kushangaa ma-DC wengi wateule walishajua wameteuliwa na wengine walidiriki hata kubadili miondoko. Mimi nawajua watatu waliojua ni maDC na wilaya zao. Mmoja anakuja wilayani kwangu. Hivyo kifupi VETTING siku hizi ni utashi wa Mkulu au jitihada za anayetaka kuteuliwa!
wewe ni mwongo!
 
Ukiona mambo kama haya yanatokea ujue kuna tatizo kati ya anaeteua na wanaofanya vetting! Nasema hivi kwa sababu vetting yeyote haiwezi kuruhusu haya!
 
Mtu aliye na uwezo wa kuropoka hadharan huwez kutulia kuwaza hata akiwa peke yake. Binadam tunawaza mabaya mengi kuliko tunayoyatamka.

Mwalim mkuu wa fasih aliwah kusema , yamjazayo mtu ndio yamtokayo. Ukiona mtu anakurupuka kuongea jua na moyo wake unarukaruka kuwaza hovyo hovyo aka unakurupuka kuwaza!!
 
Halafu sasa naona wanajeshi wengi wanapewa nafasi hizo za uDC na uRC wengine wastaafu na wengine inservice
13507101_10209678182540634_7395539781362859063_n.jpg
 
wewe ni mwongo!

Ndugu/Dadangu, mimi si mwongo maana huwezi kuthibitisha uongo wangu. Mimi ninakueleza ninajua maDC 3 all are my friends walijua ni wateule before na wilaya zao. Nikiwataja hapa si fare kwao na kwangu. Ndio msingi wa hoja yangu kuwa real vetting ilikuwa kipindi cha JK1.
 
Kichekesho walishateua mkurugenzi wakasitisha uteuzi ndani ya saa 24 bila kkutoa sababu yoyote. Bora Kitwanga walisema ni pombe hawa wengine nadhani ni mzimu tu umekataa.
 
Back
Top Bottom