Samahani Rais Magufuli kwa kukosa kura yangu Oktoba 2020

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,210
12,913
Mh. Rais naomba kukuomba radhi kuwa kura yangu yamkini usiipate happy October utakapo fanyika uchaguzi mkuu.

Mh Rais, Juzi wakati narudi nyumban majira ya saa 22:00 nilikutana na vibaka na wakafanikiwa kunipiga panga 2-3 kichwani huku wakichukua kila kitu nilichonacho ikiwemo na wallet iliyokuwa imebeba kitambulisho cha kupigia kura ambacho licha ya kuwa na matumizi mengine lakini kubwa ilikuwa kura yako hapo October.

Nimechukua hatua ikiwemo kureport Police Tabata na tayari nina RB japo Sina hakika kama kwa muda uliobaki nitafanikiwa kupata kitambulisho changu na nikakitumia ipasavyo.

Kwa hayo machache Mh Rais nakutakia ushindi wa kishindo hapo October kwenye uchaguzi mkuu.
Ahsante
 
Wewe unapigwa panga na wezi waliotapakaa kutokana na serikali ya magu kushindwa kusimamia usalama wa raia wake kikamilifu halafu unamtakia magu ushindi?! Kama hata baada ya kupigwa mapanga bado huoni tatizo la serikali hii, je ujinga wa watanzania utakwisha lini Mungu wangu?
 
Wewe unapigwa panga na wezi waliotapakaa kutokana na serikali ya magu kushindwa kusimamia usalama wa raia wake kikamilifu halafu unamtakia magu ushindi?! Kama hata baada ya kupigwa mapanga bado huoni tatizo la serikali hii, je ujinga wa watanzania utakwisha lini Mungu wangu?
Mimi nimejaribu kumsoma kwa makini mstari kwa mstari ili nimwelewe vizuri anachoandika, nikashindwa kukipata.

Nikarudi mwanzo wa mada yake na kusoma katikati ya mistari, bado namwona kama juha fulani baada ya kujiridhisha kwamba andiko lake hata 'fasihi' hailielezei ipasavyo!

Nikaamua nimpe ushauri huu:

Kesho asubuhi ikiwezekana afunge safari kwenda Dodoma akaonane na mhusika na amweleze yote yaliyomsibu. Aombe msako mkali ufanyike kuwapata hao vibaka. Hili ni mhimu kufanyika vinginevyo watasingiziwa wapinzani kwamba ndio waliofanya hujuma hii ya kumkosesha kura mkuu.
 
Kwani hao wezi shingo hawakuiona mpaka wamepata tabu yakukupiga kichwani, alafu unakuja kuwaanika huku.
 
mimi nimemwelewa vizuri mtoa mada, pamoja na ukweli kuwa anapaswa kuwahi hospital ya mirembe kurekebisha dishi lake ambalo limeyumba ila....

ila ni kwamba anazungumzia vizuri kuwa pamoja na ufalme tunaomtukuza nao Mh Rais Magufuli ila suala la ajira limemshinda kwa sera zake za uchumi kuua sekta binafsi inayoajiri 90% + ya able bodied people!! na hivyo kuzalisha ajira mpya ya matapeli na vibaka na kuongezeka kwa soko la mapanga!!

utitiri wa wagombea kura za maoni ni ujumbe tosha kuwa vyuma vimekaza ajira hakuna na kuharibika kwa uchumi wa mamilioni ya watu ambao ni matajiri wa zamani ambao wamefilisika na sasa wanaishi kishetani!!
 
Back
Top Bottom