Kupeleka chakula kwa mwenzako wakati wewe una njaa ni wema au unafiki?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,864
Hivi majuzi niliona mahala na kusikia kwingineko kuwa Tanzania imepeleka Shehena za Mahindi ya Msaada kwa Waathirika wa Kimbunga Freddy huko nchini Malawi kama sehemu ya kuonyesha ujirani mwema na kupata Thawabu zaidi kwa Mwenyezi Mungu.

Sasa nami GENTAMYCINE nauliza je, kutoa Msaada wa Chakula kwa Jirani yako mwenye tatizo (njaa) wakati hata wewe pia kwako kuna njaa tukuka katika baadhi ya maeneo, ni kutafuta Thawabu kwa Mola au kuonyesha Unafiki?

Nitashukuru nikielimishwa tu zaidi.
 
Hivi majuzi niliona mahala na kusikia kwingineko kuwa Tanzania imepeleka Shehena za Mahindi ya Msaada kwa Waathirika wa Kimbunga Freddy huko nchini Malawi kama sehemu ya kuonyesha ujirani mwema na kupata Thawabu zaidi kwa Mwenyezi Mungu...
Mahindi karibu yote yanayosagwa Dar yanatoka Malawi na Zambia sasa sisi kuwapelekea mahindi ni kituko
 
Hiyo ndio moja wapo ya PROPAGANDA kwa Nchi Yetu na Sisi kwa Nchi Kuonekana kuwa Tunajari hata Tukipata Matatizo Tuonekane Kwa Ujirani Mwema,Hasa Kimataifa kwa Nchi ya TZ.
 
Hivi majuzi niliona mahala na kusikia kwingineko kuwa Tanzania imepeleka Shehena za Mahindi ya Msaada kwa Waathirika wa Kimbunga Freddy huko nchini Malawi kama sehemu ya kuonyesha ujirani mwema na kupata Thawabu zaidi kwa Mwenyezi Mungu...
Ni Baraka, Hata yule Tajiri aliambiwa uza mali zako zote kisha unifwate, Ndio maana Mungu Kaachilia mvua
 
Itoshe kusema HANGAYA anajua kujipendekeza,ukiachana na hayo mahindi na pesa kedekede kwa malawi, nimeshangaa zaidi kuona eti Tanzania inatoa Bil.2 kwa Turkey kama msaada, kha!!!
 
Kuna watani zako fulani wana msemo kuwa mwenye njaa hamponyeshi mwenye njaa mwenzake, yaani huwezi kupeleka uponi kwa mwingine kwa kuwa nawe huna chakula.

Watu wameshangaa kitendo hicho na wanadai huenda kukawa na upungufu wa chakula hicho na unga ukapanda bei
 
Hivi majuzi niliona mahala na kusikia kwingineko kuwa Tanzania imepeleka Shehena za Mahindi ya Msaada kwa Waathirika wa Kimbunga Freddy huko nchini Malawi kama sehemu ya kuonyesha ujirani mwema na kupata Thawabu zaidi kwa Mwenyezi Mungu...
Inategemea jirani yako kapatwa na janga gani, kuna suala la njaa, pia kuna suala la njaa +janga, huyu ni lazima umuokoe maana amekutwa na vyote viwili kiutu ni lazima umsaidie, ila nyie msio na utu wala kupima mambo na jinsi mlivyo na maroho mabaya toka kuumbwa kwa dunia hamuwezi kumsaidia mtu, japokuwa unaona kabisa fulani kaelemewa.
 
Back
Top Bottom