Samahani kama kuna nitakaowakwaza ila nadhani hili Jambo lisiwe la Kuzoeleka kwani linaleta ' Usumbufu ' mkubwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,365
2,000
Najua kuwa kuna Misiba ya Watu ambao huwa tunawapenda huwa inatuuma na kutugusa sana kwa kila hali hasa kutokana na ule umuhimu Wao Kwetu hasa pale walipokuwa Hai na yale mema ambayo walikuwa wakifanya Kwetu au katika Jamii nzima.

GENTAMYCINE leo nasemea tu Suala moja la Utaratibu hasa wa Watu pale Mwili wa Mpendwa Wao ukiwa unapita. Kuna Msiba Mmoja nauona ambao kwa Ratiba yake iliyokuwepo mpaka hivi sasa Saa 8 Mwili ulitakiwa zamani sana uwe umeshafika ulikokusudiwa kwa ajili ya Kuhifadhiwa ila Ratiba hiyo imeshindikana kutokana na Watu Kuuingilia hali iliyofanya icheleweshe kila Kitu na kusababisha Usumbufu kwa Wafiwa na hata Wageni wengine walioko katika Msafara huo.

Nadhani kungekuwa na utaratibu ' Maalum ' kutoka katika Kamati za hii Misiba kwamba kama wanajua Wapendwa Wao walikuwa wakipendwa mno na Watu basi wangekuwa wanaweka tu Utaratibu fulani wa Miili ya Marehemu hao kuwekwa sehemu moja ili Watu waage kisha ratiba zingine ziendelee na kusiwe na Ucheleweshwaji wowote huko njiani hali ambayo inasababisha Foleni zisizo za lazima kwa Watu wengine ambao nao wanaendelea Kujenga nchi yao kama vile ambavyo hao Marehemu nao waliijenga nchi.

Kwanza ni HATARI sana pale Msiba ukiwa katika Msafara wake mkubwa Kuingiliwa tena na Watu walioko pembeni kwani kunaweza pia kukatokea ' balaa ' la Mtu / Watu ' Kugongwa ' au hata ' Kujeruhiwa ' hivyo ikawa ni kuzidisha tu matatizo kama si usumbufu.

Ila lawama zangu kubwa na nyingi nazipeleka kwa Kamati za Misiba na Ulinzi na Usalama za hiyo Mikoa ambayo Watu hawa Maarufu wanaishi au wanatokea. Kama Ratiba tayari imeshapangwa hakuna tena haja ya Kuiharibu kwasababu tu kuna Watu wamesimama barabarani na wengi Wao wakiwa hadi wanaingia barabarani Kuzuia Gari na kusababisha Ucheleweshwaji wa Mwil kufika kule ambako umekusudiwa na kwa wakati ( muda ) fulani.

Tukumbuke kuwa wenye ' Uchungu ' na Marehemu siyo wale tu waliojipanga Barabarani huku wakiwa wanalia, wamebeba Maua, Majani na Kutandika khanga Barabarani bali pia kuna wale ambao nao wamechukuwa muda Wao wamesafiri umbali mrefu ama kwa Magari au Ndege kuweza Kuusindikiza Mwili ( Marehemu ) hivyo kwa Kiasi fulani nina uhakika kuwa hata Wao ' wanakwazika ' kwa namna moja au nyingine kwa hii ' tabia zoeleka ' ya Kuingilia Misafara ya Mazishi ya Watu Maarufu, Wakubwa na Mashuhuri nchini.

Ni kweli kabisa kwamba hawa Marehemu huwa tunakuwa tunawapenda sana na mno ( kama vile ambavyo hata Mimi GENTAMYCINE ) nawapenda na nawalilia ila ' Concern ' yangu Kubwa tu ni huu ' Utaratibu ' wa Kuingilia Misafara hovyo wakati tayari kuna muda ' Maalum ' unakuwa umeshapangwa kwa Mwili na Waombolezaji kuweza kufika Kijijini ili kupisha ratiba zingine kuweza kuendelea.

Sasa kama leo tu Safari ya Kilometa 39 kutoka Uwanjani KIA hadi Kijijni kwa Marehemu ambayo ilitakiwa ichukue takribani Saa Moja au Mawili tu kwa Msafara huo Kuingiliwa na Watu hovyo na mara kwa mara barabarani sasa umecheleweshwa kwa takribani Masaa 5 kama siyo 6.

Tunaochelewesha hii Misiba humu Barabarani tukumbuke kuwa tunawatesa pia na Wajane, Ndugu, Jamaa na Marafiki wengine waliopo katika Misafara kwa Kuzidi Kuwachosha zaidi njiani na hata kuwazidishia Majonzi japo wanaweza wasiseme ila kimoyomoyo ' wanakwazika ' sana tu. Kuna Watu wapo katika hayo Magari ya Misafara labda wanaumwa au wengine wameshikwa na Haja na kutoka katika Misafara Kwao inakuwa ngumu je hapa kwa Sisi Kuiingilia hovyo na mara kwa mara hii Misafara hatuoni kama tunawapa nao Usumbufu wa kilazima na usiotarajiwa?


Naomba radhi kama kuna nitakaowakwaza kwa huu Uzi wangu ila dhamira yangu GENTAMYCINE ni njema na nzuri tu japo kwa sasa Mtu unaweza usione kwakuwa tu bado tukio zima linaendelea ila kwa Jicho la mbali zaidi nadhani sasa kunahitajika Elimu hasa kwa Watu namna ya Kuikabili Misiba hii mikubwa na ya Watu maarufu ili kutoleta Usumbufu na kusababisha upotezaji mkubwa wa muda na kuharibu Ratiba ambazo huwa tayari zinakuwa zimepangwa kwa Kuzingatia mambo mengi sana.

Tujifunze kuwa Wastaaabu na Kufuata Utaratibu ili tusiwakwaze na wengine.

Nawasilisha.
 

Roman Empire

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
623
1,000
Unaweza kufikiria unapendwa Lakin ukapata matokeo tofauti na matarajio yako. Tuache utani mengi alipendwa na watu wa kijiji kwake. Sio kwa umati uliosimama barabaran kuanzia machine tools. Watu watu wa protocal wajipange kwa kesho wasije kuzika na tochi
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,365
2,000
Mkuu kuna watu wana imani juu ya Maiti, kwamba wakigusa jeneza wanapata baraka, yaani hao ndio wasumbufu. Elimu itolewe kwa kweli kuanzia makanisani na misikitini

Kuna Kundi Kubwa sana la Watu pale KIA njia panda walihojiwa wakasema huku wakijiapiza ' Mubashara ' kabisa kuwa wanaenda na Msafara hadi kwa Marehemu Kijijini lakini cha Kushangaza wakati Msafara ulipoongeza Kasi na Wao safari zao ziliishia pale pale japo kuna baadhi ' Wabishi ' nimewaona wamekodi ' Bodaboda ' na ' wameliunga ' hadi Kijijini kwa Marehemu.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,365
2,000
Unaweza kufikiria unapendwa Lakin ukapata matokeo tofauti na matarajio yako. Tuache utani mengi alipendwa na watu wa kijiji kwake. Sio kwa umati uliosimama barabaran kuanzia machine tools. Watu watu wa protocal wajipange kwa kesho wasije kuzika na tochi

Na Mimi nililitegemea kwamba kama Kamati Kuu ya Mazishi ilijua kabisa kuwa huo Mkoa na hasa huko Kijijini ndiyo ' Stronghold ' ya Marehemu kwanini hawakufanya ' anticipation ' ili waweze Kujipanga zaidi hasa katika suala zima la Ratiba na Kukabiliana na huu Uwingi wa Watu unaoonekana?

Kuna muda nilianza Kuogopa kuwa huenda kungekuwa na ' Stampede ' ambayo ingeweza Kuhatarisha Maisha ya Watu hasa wale waliokuwa wamejipanga Barabarani na wengine wakikimbia na Msafara huku wengi wao wakiwa ni Wanawake ( akina Mama ), Watoto na Wanafunzi baadhi ila nashukuru Mungu kwamba hakuna ' dhahama ' ya namna hiyo iliyotokea.
 

Roman Empire

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
623
1,000
Na Mimi nililitegemea kwamba kama Kamati Kuu ya Mazishi ilijua kabisa kuwa huo Mkoa na hasa huko Kijijini ndiyo ' Stronghold ' ya Marehemu kwanini hawakufanya ' anticipation ' ili waweze Kujipanga zaidi hasa katika suala zima la Ratiba na Kukabiliana na huu Uwingi wa Watu unaoonekana?

Kuna muda nilianza Kuogopa kuwa huenda kungekuwa na ' Stampede ' ambayo ingeweza Kuhatarisha Maisha ya Watu hasa wale waliokuwa wamejipanga Barabarani na wengine wakikimbia na Msafara huku wengi wao wakiwa ni Wanawake ( akina Mama ), Watoto na Wanafunzi baadhi ila nashukuru Mungu kwamba hakuna ' dhahama ' ya namna hiyo iliyotokea.
Kesho wajipange kweli kweli kupeleka mwili kanisani na safari ya kwenda kuzika kijiji watu watakuwa wengi sana
 

Njemba Soro.

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
1,623
2,000
Hapo kwenye kushikwa na haja umesema kweli kabisa..... tulisafirisha mwili kutoka dar kwenda kibosho huko aisee ile kukaribia nyumbani kumbe watu wamejazana barabarani wakashusha jeneza wanatembea nalo taratiiiiibu..... halafu marehemu ni broo wangu. Nimeshuka kwenye gari ili nikojoe migombani aisee alikuja dada mmoja kunirukia eti analia nimefanana na broo hajui kama nimechoka na nimebanwa haja..... nilimwangalia vibaya hadi akajishtukia halafu sikuongea naye na alikuwa mtoto wa shangazi. Baadaye nilimwambia kwa nini nilichukia tukasameheana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom