Salva Rweyemamu wa IKULU aanzisha gazeti

Tunashukuru sana kwa nondo hizi. Tunaomba muendelee kuzidondosha, wakituibia wajue kuwa tunafahamu. 2005 ni tofauti sana na 2010 mbinu walizotumia 2005 sidhani kuwa zitawavusha 2010, itabidi wabuni zingine

Sasa suala hapa nikuwaumbua wasiendelee kutuibia au wawe wanabuni mbinu mpa kutuibia?
 
Ameniahidi kumchota kila muandishi wa habari Tz mpenda fedha na tayari wengi makanjanja washakubali.
Makanjanja hao wako chini ya Kanjanja wewe!! kwa hiyo umeamua kuwa kanjanja ili ujengewe nyumba na kununuliwa gari?
 
Ee Mungu tunakuomba utuepushie vikombe hivi vya JK na CCM, Waja wako tunateseka katika hii nchi uliyotupatia huku wezi wachache wenye tamaa wasiotii amri yako inayosema Usiibe na usitamani wakiendelea kututesa. Tunakuomba e mola siku ukirudi hapa duniani hebu ukatulipie na kuzidi kwa maovu yao na hila walizotutenda na wanazoendelea kututenda. Sisi baba tunaendelea kuwasemehe kwani ulisema sameheni 7 mara 70. Mungu uliyemkuu utuzidishie Amani, Upendo na umoja kwani ndio utajiri pekee uliobaki kwetu sisi waja wako. AMINA.
 
Mkuu Wild Card, kwa sasa Mbwambo&Ulimwengu are speaking 2 different languages na kina Shoo na mwenzie Salva as far as house style is concerned ktk uendeshaji wa media house. Raia Mwema wanacriticise govt. wazi wazi ktk yale yasiyo ya maslahi kwa nchi wakati Shoo na mwenzie Salva ujio wao ni wa kuipamba serikali ya Chama Chawala!!
 
Kwa jinsi ninavyoifahamu Tanzania, hili mbona la kawaida tu?

Kama mwataka kuongelea ufisadi, zungumzieni wale wenye personal banks at their residences, wana strong rooms. Akitaka kwenda Geneva anaingia ndani kule, anachukua Swiss Francs. Akitaka kwenda Munchen, anachukua Deutsche Marks, etc., etc., etc.

Wazungumzieni hao. Wanapataje hizo fedha? Hao akina Shoo na Salva ni dagaa kwenye bahari ya mafisadi. Watafuteni mapapa wenyewe.
 
Ni kipindi cha serikali ya CCM kugawa mafweza ya wananchi kwenye vyombo vya habari -- hasa magazeti -- kwa matangazo yatokanayo na budget. Tutaona hata magazeti uchwara yanasheheni matangazo ya speech za mawaziri mbali mbali kuhusu bajeti za wizara zao. Hata magazeti yale yenye misimamo mikali dhidi ya CCm na serikali yake nayo yatabadilisha gia ili wapewe matangazo.

Tutashuhudia mengi katika vyombo vya habari -- jinsi vitakavyolazimishwa kuinama chini kabisa bila aibu kwa ajili ya kupewa fedha za wananchi zinazosimamiwa na serikali ya CCM! Ni kipindi ambacho magazeti yatashangaza wasomaji wake!!!!!

Madhambi ya mawaziri kuhusu utafunaji wa fedha katika wizara zao hayataandikwa kamwe hata yakigunduliwa na gazeti -- kwa ahadi ya matangazo ya biashara!

HII NDO TANZANIA YETU.[/QUOTE

GREAT PITY

mix with yours
 
Kuanzishwa kwa gazeti siyo tatizo iwapo tu gazeti hilo siyo la kuwalinda mafisadi na maadui wengine wa uma wanaotumia nafasi zao kuididimiza Tanzania kwa faida yao binafsi, ndugu, jamaa, marafiki au kundi lao!
 
Ushauri wangu, tukishirikiana kutambua magazeti husika, tunahimiza na kuwafahamisha wananchi wasiopenda habari za kupikwa ili kumpamba mtu fulani wayakatae magazeti haya. Tuone kama yatauzika namna hiyo. Waambie waulize kilichotokea kwa gazeti la rai lilivyokuwa linauza kama njugu, lakini kitendo cha kununuliwa na kuanza kuandika habari zilizotengenezwa, wasomaji wengi makini wa wakati huo hawataki hata kuliona. Na nadhani reputation yake imepotea siku hizi si kama zamani. Kwa hiyo ndugu zangu, mapambano yanaendelea, wanafanya na sisi wapenda haki na ukweli tunafanya tusiishie kusema tu!
 
Back
Top Bottom