Salva Rweyemamu wa IKULU aanzisha gazeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salva Rweyemamu wa IKULU aanzisha gazeti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Informer, Jun 14, 2010.

 1. T

  The Informer Senior Member

  #1
  Jun 14, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hodi JF,

  Kuna taarifa za uhakika kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu, pamoja na business partner na rafiki wake wa siku nyingi, Dk. Gideon Shoo, wameanzisha gazeti la kila wiki la Kiswahili, TAFAKARI, ambalo linalenga uchaguzi mkuu ujao.

  Hivi sasa inaelezwa kuwa kuna amri ya Ikulu kuwa Idara ya Habari, Maelezo, isitishe kusajili magazeti mapya eti mpaka sheria mpya ya Habari itakapopitishwa. Ni wazi hii ni mbinu ya kudhibiti media kwenye uchaguzi mkuu.

  Hivi sasa Salva na Shoo wamekodi gazeti hilo la TAFAKARI kutoka kwa mmiliki wake halisi ili waliendeshe kwa muda kwenye kipindi hiki cha mavuno cha kuelekea uchaguzi mkuu.

  Lengo la kuanzisha gazeti hillo ni kupata matangazo ya Bajeti za wizara za serikali kwenye Bunge linaloendelea sasa ili wavune at least 300 million shillings za matangazo.

  Pia, gazeti hili linategemea kupata matangazo mengine zaidi kutoka serikalini na msaada wa system kwa makubaliano kuwa litakuwa linaandika habari za kumpamba Rais Jakaya Kikwete na chama cha CCM ili wapate ushindi wa kishindo 2010.

  Watu walio karibu na 'wajanja' hawa wawili wanasema kuwa lengo haswa ni kwa Salva na Shoo kuvuna pesa za matangazo ya bajeti na uchaguzi mkuu kwa kupitia mgongo wa kumsaidia JK na CCM.

  Inasemekena kuwa gazeti hili linaendeshwa kutoka ofisi iliyopo Sinza, Dar es Salaam, na lina idadi chache sana ya waandishi wa habari na wafanyakazi wengine. Salva na Shoo husemekana kuwa nao wanasaidia kuandika baadhi ya makala kwenye gazeti hilo.

  Pamoja na kuwa na waandishi wachache mno, bado uongozi huo unachelewa kuwalipa mishahara yao na huenda kukawa na matatizo makubwa zaidi pesa za matangazo ya bajeti na uchaguzi zitakavyoanza kumiminika. Gazeti hili limejipa mategemeo makubwa ya kupata matangazo serikali kwa kujinadi kuwa ni "Special Project" ya kuhakikisha ushindi wa Kikwete na CCM kwenye uchaguzi wa 2010.

  Ikumbukwe kuwa Salva na Shoo zamani walikuwa wakurugenzi wa Habari Corporation inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai na mengineyo kabla ya kuuza kampuni hiyo kwa mbulushi Rostam Aziz -- yule mbunge wa Igunga anayehusishwa na Richmond, Kagoda, import support, kashfa ya kodi kwenye uagizaji mchele, mbolea, pembejeo, n.k.

  Salva na swahiba wake, Shoo, wana kampuni ya Public Relations inayoitwa
  G&S Media Consultancy. Hii kampuni ndiyo ilifanya kazi ya kuitangaza kampuni ya kitapeli ya Richmond Development Company LLC kupitia vyombo vya habari wakati ilipoingia Tanzania kufanya upigaji.

  Katika mradi huu, Shoo ndiyo yuko front na Salva anaonekana kujificha kwa mbali asionekene kuhusika moja kwa moja.

  Kweli nchi hii wajinga ndiyo huliwa!

 2. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huu ni mfululizo wa madudu ya utawala wa JK. inasemekana pia mtoto wake anamiliki gazeti linaloitwa Jambo Leo. Nalo limeanzishwa kwa madhumuni hayo hayo ya kumpigia debe JK ili aendelee kupeta tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano licha ya udhaifu mkubwa aliouonyesha mpaka sasa. Ee Mungu, ikiwezekana tuepushie 'kikombe' hiki.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako informer.

  Mkuu habari nzito lakini inatia shaka kwasababu kila sehemu kuna neno inasemekana limejirudia mara nyingi kiasi kwamba inatia shaka uhakika wa habari yenyewe.
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tunashukuru sana kwa nondo hizi. Tunaomba muendelee kuzidondosha, wakituibia wajue kuwa tunafahamu. 2005 ni tofauti sana na 2010 mbinu walizotumia 2005 sidhani kuwa zitawavusha 2010, itabidi wabuni zingine
   
 5. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  salva stop t please
  z part of ya job?
  y dont u gve the tender to pipo waliokwenye industry....?
  bt sidhani km ni idea nzuri ya kujiingiza kunako magazeti babu
  z beta for u kufanya yanayokuhusu bwana achana na kukuru kakara za kuchupia peas mwisho wa siku utashusha p yako!!!!

  pooe na majukumu baba bt pleeeeessssss rudi kwenye mstari b4 aujapotea!

  ol da best n may god bless u.....:sick:
   
 6. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  na kumbuka lolote unalofanya katika dhamana ulionayo ina madhara kwa wanawake,watoto na vikongwe.....tanzania kwa ujumla

  b wise n act for da well being of tanzania.stp thk for yaself

  kuwa mtu n dont ride wheel where u thk wthot concerning tanzanians!!!!1
  kua mtu pleeeeeeeas .........utaumbuka miuda si mrefu.....
   
 7. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ndio maana hii imeitwa tetesi. Naamini kuna watu watakuja na nondo za kuthibitisha hili.
   
 8. T

  The Informer Senior Member

  #8
  Jun 14, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna tetesi zaidi pia gazeti la TATHMINI ambalo linasemekana kumilikiwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, ambaye pia ni waziri kivuli wa fedha nalo limepokea mamilioni ya shilingi kutoka serikani kupitia tangazo la bajeti.

  Nimelinunua leo hili gazeti na kweli lina kurasa nyingi za matangazo ya bajeti. Hapa swala la
  CONFLICT OF INTEREST halileti utata?
   
 9. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kaaazi kwelikweli, haya twende!
   
 10. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  tUTASIKIA MENGI MWAKA HUU
   
 11. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu Salva ni mtu rubbish tuu.

  Mi nashangaa sana, Ikulu ya karne ya 21 haina at interactive website, haina njia ya wananchi ku-access key information about the executive and decision it makes. Eti Director of Presidential Communication. Upuuzi mtupu, aitwe ka-spokesman tuu because that is all he seems to be doing. Where is the innovation?

  Where is the efficiency and transparency that is required by the principles of good governance. Nani anaemjua huyu mtu mumuite hapa aje atueleze wananchi what it is that we pay him for?
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  Jun 14, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mmh,haya,kumbe lao!mbona halina mvuto!
   
 13. G

  Godwine JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  haya wakuu mambo yameanza
   
 14. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hakuna hata maadili ya uongozi ndio Jakaya huyo.
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni kipindi cha serikali ya CCM kugawa mafweza ya wananchi kwenye vyombo vya habari -- hasa magazeti -- kwa matangazo yatokanayo na budget. Tutaona hata magazeti uchwara yanasheheni matangazo ya speech za mawaziri mbali mbali kuhusu bajeti za wizara zao. Hata magazeti yale yenye misimamo mikali dhidi ya CCm na serikali yake nayo yatabadilisha gia ili wapewe matangazo.

  Tutashuhudia mengi katika vyombo vya habari -- jinsi vitakavyolazimishwa kuinama chini kabisa bila aibu kwa ajili ya kupewa fedha za wananchi zinazosimamiwa na serikali ya CCM! Ni kipindi ambacho magazeti yatashangaza wasomaji wake!!!!!

  Madhambi ya mawaziri kuhusu utafunaji wa fedha katika wizara zao hayataandikwa kamwe hata yakigunduliwa na gazeti -- kwa ahadi ya matangazo ya biashara!

  HII NDO TANZANIA YETU.
   
 16. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,753
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280

  Angalia hayo maneno niliyo underline hapo juu,ila ahsante kwa taarifa!
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  The Informer, asante kutuinform,
  naomba twende nyuma na mbele, tutizame upande mmoja wa shilingi na kugeuza na upande wa pili,
  Salva kitaaluma ni mwandishi, kwa sasa ameajiriwa na Ikulu, hiyo hainyimi fursa ya kufanya biashara nyingine yoyote ikiwemo kumiliki gazeti, hata kituo cha redio na TV au hata kufuga kuku.

  Conflict of interest itakuja pale tuu atakapoitumia fursa ya uwepo wake Ikulu kulipatia gazeti lake matangazo kwa kutumia undue influence. Lakini kama anamili gazeti na Dr. Shoo, gazeti linafanya vizuri, linatafuta matangazo serikali na kwingineko, linapata what is wrong?.

  Kama uwepo wa Salva ikulu amegundua magazeti yaliyopo hayaifagilii serikali ya JK, hawayaelezi mazuri ya serikali ili wananchi waielewe vizuri serikali yao na kuipenda na kuendelea kuichagua, hapo tayari Salva ameshaona ombwe kwenye magazeti yaliyopo. Hivyo uamuzi wa kuanzisha gazeti mahsusi kuziba ombwe hilo, hii ndio inaitwa tarning the problems into opportunities!. Bado sioni tatizo hapa hata Salva pia akiandika.

  Salva kama Mtanzania mwingine yoyote, ana uhuru wa kuwa mjasiliamia, tatizo ninaloliona hapa ni the deviding line between kulitumia gazeti lake kwa maslahi ya binafsi ya uwepo wake ikulu, dhidi ya maslahi ya umma kupata habari ni very thin, ndio maana Mkapa alifanya biashara akiwa ikulu and he broke no law, ndivyo afanyavyo Salva, he broke no law, na hata muungwana alivyowanunua majirani zake pale regent na kujijengea kaikulu kadogo, he break no law, etc etc, issue iwe only on morality.
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  The informer... yaani umeshalipa PROMO hili gazeti

  DN
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Salva na Dr Shoo hawaivi tena na akina Jenerali/ Mbwambo? Wangeliimarisha tu RaiaMwema au?
   
 20. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,184
  Trophy Points: 280
  Hatutalinunua kamwe, wacha wapeane hayo madili ya matangazo.
  Walala hoi tumekataa kupelekeshwa kama gari bovu. [QUOTE=The Informer;951329]Hodi JF,

  Kuna taarifa za uhakika kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu, pamoja na business partner na rafiki wake wa siku nyingi, Dk. Gideon Shoo, wameanzisha gazeti la kila wiki la Kiswahili, TAFAKARI, ambalo linalenga uchaguzi mkuu ujao.

  Hivi sasa inaelezwa kuwa kuna amri ya Ikulu kuwa Idara ya Habari, Maelezo, isitishe kusajili magazeti mapya eti mpaka sheria mpya ya Habari itakapopitishwa. Ni wazi hii ni mbinu ya kudhibiti media kwenye uchaguzi mkuu.

  Hivi sasa Salva na Shoo wamekodi gazeti hilo la TAFAKARI kutoka kwa mmiliki wake halisi ili waliendeshe kwa muda kwenye kipindi hiki cha mavuno cha kuelekea uchaguzi mkuu.

  Lengo la kuanzisha gazeti hillo ni kupata matangazo ya Bajeti za wizara za serikali kwenye Bunge linaloendelea sasa ili wavune at least 300 million shillings za matangazo.

  Pia, gazeti hili linategemea kupata matangazo mengine zaidi kutoka serikalini na msaada wa system kwa makubaliano kuwa litakuwa linaandika habari za kumpamba Rais Jakaya Kikwete na chama cha CCM ili wapate ushindi wa kishindo 2010.

  Watu walio karibu na 'wajanja' hawa wawili wanasema kuwa lengo haswa ni kwa Salva na Shoo kuvuna pesa za matangazo ya bajeti na uchaguzi mkuu kwa kupitia mgongo wa kumsaidia JK na CCM.

  Inasemekena kuwa gazeti hili linaendeshwa kutoka ofisi iliyopo Sinza, Dar es Salaam, na lina idadi chache sana ya waandishi wa habari na wafanyakazi wengine. Salva na Shoo husemekana kuwa nao wanasaidia kuandika baadhi ya makala kwenye gazeti hilo.

  Pamoja na kuwa na waandishi wachache mno, bado uongozi huo unachelewa kuwalipa mishahara yao na huenda kukawa na matatizo makubwa zaidi pesa za matangazo ya bajeti na uchaguzi zitakavyoanza kumiminika. Gazeti hili limejipa mategemeo makubwa ya kupata matangazo serikali kwa kujinadi kuwa ni "Special Project" ya kuhakikisha ushindi wa Kikwete na CCM kwenye uchaguzi wa 2010.

  Ikumbukwe kuwa Salva na Shoo zamani walikuwa wakurugenzi wa Habari Corporation inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai na mengineyo kabla ya kuuza kampuni hiyo kwa mbulushi Rostam Aziz -- yule mbunge wa Igunga anayehusishwa na Richmond, Kagoda, import support, kashfa ya kodi kwenye uagizaji mchele, mbolea, pembejeo, n.k.

  Salva na swahiba wake, Shoo, wana kampuni ya Public Relations inayoitwa
  G&S Media Consultancy. Hii kampuni ndiyo ilifanya kazi ya kuitangaza kampuni ya kitapeli ya Richmond Development Company LLC kupitia vyombo vya habari wakati ilipoingia Tanzania kufanya upigaji.

  Katika mradi huu, Shoo ndiyo yuko front na Salva anaonekana kujificha kwa mbali asionekene kuhusika moja kwa moja.

  Kweli nchi hii wajinga ndiyo huliwa!

  [/QUOTE]
   
Loading...