Salva Rweyemamu tuambie ukweli wako TUMAINI LILILOREJEA limekwenda wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salva Rweyemamu tuambie ukweli wako TUMAINI LILILOREJEA limekwenda wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dumelambegu, Mar 12, 2011.

 1. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,

  Mmojawapo ya wanamtandao waliomfikisha Kikwete hapo alipo ni Bw. Salva Rweyemamu. Huyu jamaa alitumia kalamu yake kwa nguvu zake zote kumpamba kikwete na bila aibu ndiye aliyeongoza jopo la waandishi wa habari waliomchafua Mzee mwenye rekodi ya kutukuka Mhe. Salim Ahmed Salim.

  Alitumia gazeti maarufu wakati huo la RAI kuwadanganya watanzania kwamba Kikwete ni TUMAINI LILILOREJEA!! Kama kawaida ya kikwete, hakuna mwanamtandano hata mmoja ambaye yupo kijiweni hana kazi. Wote wamepewa vyeo vikubwa bila kujali wana uwezo au hawana.

  Najua Salva ni msomaji wa mtandao huu wa JF. Sasa nataka atueleze kwa moyo wa dhati kabisa, je tumaini lililorejea mbona hatulioni!!! Limeenda wapi?? Au ni yeye na wanamtandao wenzie ndiyo pekee wanaoliona!
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa swali lako alieleweki; ilo tumaini unalosema halionekani,inategemea umemlenga nani, kama ni Salva na wenzake wachache, hao utajiri walioibuka nao katika kipindi hiki, hawakuutarajia kabla ya JK kuingia madarakani.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Na tuko makini sana na hilo gazeti la RAI na pumba zake. Halitaheshimika tena. Linadharaulika mtaani kuliko inavyodharaulika CCM ya JK
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,606
  Likes Received: 3,908
  Trophy Points: 280
  They had clear goals what they want!!! LOL! they dont even ashamed of their deed.

  These guys are criminals..they are worse than all those we know
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Alichokuwa anatafuta tayari amekipata. Anakula kuku kwa mrija pale Magogoni. Sasa unataka akueleze nini tena!?
   
 6. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Inaonekana wewe hukumuelewa vizuri, yeye alikuwa anafanya kazi maalum kwa makubaliano maalum na alifanikiwa kazi yake na kapata ujira wake. hapo alipo ndipo yawezekana aliahidiwa kuwepo mara baada ya kazi yake, yawezekana alijua anadanganya lakini yeye hakujali, labda alisema shauri yake atakaye danganyika mimi bora nimtumikie kafiri nipate ujira wangu na siku zisonge mbele.

  Tabu anayoweza kupata ni kukosa pa kuishi baada ya hii awamu yako ya kifahari! kama unavyojua madhara ya umaskini yapo wazi Tanzania, Dar es Salaam unaweza kuibiwa side-mirrow ya gari na kuuziwa na mwizi na hauna pa kwenda! hakuna serikali, kila mtu anajua ukiibiwa nenda Gerezani utapata mali yako uinunue tena! hayo ni madhara ya kuwepo tabaka la maskini waliokata tamaa. Huwezi kuwa na amani wakati umezungukwa na watu waliolala njaa, ambaye yupo tayari kukuchoma kisu kwasababu ya simu au saa kwa ina thamani kubwa sawana roho yako, ndio maana Mwl. alisisitiza kugawa kilichopo kwa haki ili kila mtu apate.

  wakati tunasoma sisi enzi za Mwalimu Shule za Serikali ndio zilikuwa bora, Seminary zilikuwepo lakini zilikuwa zinachuana na shule za serikali ngoma droo, leo shule ambayo ndiyo msingi wa ustawi wa taifa lolote viongozi wanapereka watoto wao shule nzuri za kulipia bei juu za serikali wameziuwa, mtoto wa maskini hato pata elimu bora tena.

  Taifa limevurugika.
   
 7. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  hakuna TUMAINI LILILOREJEA bali ni balaa tupu kwa nchi. naamini wote waliompa kura kikwete ambao wanaweza kuangalia vitu 'objectively' naamini mioyoni mwao mwanajuta na kutamani mungu afanye miujiza ili kuinusuru nchi katika kila sector
   
 8. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  ule ulikuwa usanii tu!
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Hapana, aliyeandika kuhusu tumaini lililorejea ni Bagenda si Salva
   
 10. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  sawa ila hata Bagenda na Salva nachelea kusema kuwa hamna tofauti, wamecheza pamoja, wametoka kijiji kimoja(RUBYA), wamesoma shule moja, wamekuja Dar wakalitumikia gazeti moja. Wote lao moja, kuliangamiza taifa ili wafukuze njaa zao!
   
 11. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mzee unadata.....
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Si hivyo tu: Ni Salva aliyeondoa hata makala katika gazeti la Mtanzania Jumapili ambayo ilikuwa inamshabulia Kikwete. Makala iliandikwa na Badra Masoud ambaye wakati huo alikuwa ameachwa katika ndoa yake na Lowassa. Lakini sasa naye ameingia katika mkumbo huohuo. Kwa maneno mengine, amerejewa na Lowassa..
   
 13. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Salva Rweyemamu ambaye amekuwa akipigana kufa na kupona kudai Utanzania wake? Je ni lini alikuwa Mtanzania? Tangu miaka ya 80 alipoanza kuandika katika magazeti na marafiki zake wakubwa Jenerali Ulimwengu ambaye mnafahamu yeye ni raia wa nchi gani, marehemu John Rutayisingwa, na wapambe wake wengi ambao tunafahamu hasa jinsi alivyobebwa hadi sasa yupo pale Magogoni akiziba nafasi za wazawa.

  Sio siri yeye ni swaiba mkubwa sana wa EL na RA wakati anajifanya yuko bega kwa bega na JK hii ngonjera sasa karibu itafika mwisho. Midhali sasa umejiunga rasmi Salva the ball is in your court usiseme kwamba ni uzushi twambie wewe ni raia wa wapi? Maana hata mchezo wa Pwagu na Pwaguzi mnaoucheza na mafisadi unafahamika.
   
 14. n

  n.ngereja Member

  #14
  May 10, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama sio mfuatiliaji hapa c mahali pako
   
Loading...