Salva Rweyemamu amjibu Lipumba juu ya mafanikio ya Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salva Rweyemamu amjibu Lipumba juu ya mafanikio ya Rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kitoto Akisa, Jul 17, 2009.

 1. K

  Kitoto Akisa Member

  #1
  Jul 17, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Juzi kwenye gazeti la mwanahalisi kulikuwa na makala iliyoandikwa na Salva Rweyemamu, ambaye ni mkurugenzi wa habari wa ikulu na mwandishi wa habari wa muda mrefu (alikuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa gazeti la rai), makala ile ilikuwa ni majibu ya Salva kwa Profesa Ibrahim Lipunba ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) juu ya mafanikio ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Majibu haya ya Salva, ambaye katika makala hii alisisitiza kuwa hayo aliyoandika ni maoni yake binafsi na wala haandiki kwa nafasi yake aliyonayo pale ikulu, na hivyo sio majibu rasmi ya ikulu, yalifuatia shutuma zilizotolewa na Profesa Lipumba kuwa Kikwete hajafanikiwa katika kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.

  Katika makala ile Salva ameanza kwanza kwa kueleza kuwa anamuheshimu sana Profesa Lipumba na kwamba miongoni mwa viongozi wote walio katika vyama vya upinzani pengine labda Lipumba ndio angalau anasifa za kuongoza taifa, lakini salva anaendelea kwa kuongeza kuwa pia sio jambo la ajabu kwa Lipumba kusema hoja ya busara na hekima asubuhi na jioni kuongea vitu visivyo na maana na vinavyopingana kwani hivyo ndivyo alivyo. Akianza kuelezea mafanikio ya Rais Kikwete kwa kumlinganisha na Prof Lipumba, Salva alisema, Prof Lipumba ni mgombea urais mzoefu kwa kushindwa kwani aligombea katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 na kushindwa na Mgombea wa CCM Benjamin Mkapa, hali iliendelea kuwa hivyo mwaka 2000 na hata Mwaka 2005 aliposhindwa na Kikwete, katika kuonesha mafanikio ya JK katika hili Salva anasema Kiwete ilikuwa mara yake ya kwanza kugombea urais na alishinda kwa kishindo. Hoja ya pili anayotoa Salva kuonesha mafanikio ya Kikwete ni kuwa, anasema ukimtoa Rais wa kwanza wa Tanzania hayati Mwalimu Nyerere, kiwete ni rais wa kwanza wa Tanzania aliyewezesha kila mtoto anayemaliza darasa la saba anaendelea na sekondari. Hoja ya tatu kuonesha kushindwa kwa Lipumba na kufanikiwa kwa Kikwete, Salva anasema Lipumba ameshindwa kuondosha udini ndani ya CUF na ndio maana CUF ni chama cha pemba tu na hakina mbunge wa kuchaguliwa bara, alkini CCm chini ya Kikwete imeimarika zaidi, na kuthibitisha hili anasema ndio maana sasa CUfF wanatapatapa na kuanzisha operasheni Zinduka na operation Sangara (hii ni ya Chadema), ansema CCM iko imara ndio maana haina haja ya kuanzisha opesheni.

  Salva namalizia kwa kuuliza hivi ni nani aliyefanikiwa kati ya Kikwete aliyechaguliwa kwa zaidi ya 80% au Lipumba ambaye katika chaguzi zote za Rais alizoshiriki hakuwahi hata kuvuka zaidi ya 18%?

  Wanajamvi nawasilisha kwenu tujadili hoja hii ya Salva Rweyemamu

  ===================================


  Profesa Lipumba: Nani kashindwa kazi?

  Na Salva Rweyemamu

  WIKI iliyopita, Mwenyekiti wa muda mrefu wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alikaririwa na gazeti la MwanaHALISI akisema kuwa Rais Jakaya Kikwete "ameshindwa kazi."

  Kiongozi huyo pia alikaririwa akisema kuwa hata chama chake, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshindwa kazi.

  Nianze kwa kutamka kuwa kauli hiyo ya Lipumba haiaminiki kwa sababu siyo ya kweli na nina hakika na yeye anajua kuwa siyo ya kweli. Lakini zaidi ya kutoaminika, kauli hiyo ni ya kusikitisha na yenye kiwango cha juu cha kutowajibika kutoka kwa kiongozi kama Lipumba.

  Kwa sababu ni ukweli usiopingika kuwa miongoni mwa viongozi wote wa vyama vya upinzani, pengine Lipumba ndiye mwenye sifa angalau zinazokaribia zile za mtu anayeweza kufikiriwa kuwa kiongozi wa kitaifa.

  Isitoshe, Lipumba sasa anao uzoefu wa uongozi wa chama cha siasa. Amekuwa Mwenyekiti wa CUF kiasi cha kwamba Mtanzania mwenye umri wa miaka 15 leo na anakaribia kuwa mpigaji kura dhidi ya chama hicho, hamjui mwenyekiti mwingine yoyote wa chama hicho, isipokuwa Lipumba.

  Tatizo ni kwamba Lipumba anaongoza chama kisichokubalika katika sehemu kubwa ya nchi. Anaongoza chama ambacho kwa sababu ya sera zake za udini uliokithiri, kimefanikiwa kujithibitisha kuwa chama cha kikanda – kanda ya Pemba katika Tanzania Visiwani, wala siyo chama cha Zanzibar, bali chama cha Pemba.

  Ni kauli za namna hiyo za Lipumba ambazo wakati mwingine zinamfanya kiongozi huyo wa CUF kushutumiwa kwa kuwa kigeugeu. Mwanasiasa ambaye asubuhi anasema jambo la maana na busara, jioni anasema jambo la ovyo, lisilokuwa na kichwa wala miguu. Kauli hiyo ndiyo kielelezo kizuri zaidi cha tabia ya Lipumba.

  Sasa kutoaminika ni jambo moja. Liko jambo la pili ambalo ni kubwa zaidi kabla ya hata kujibu moja kwa moja hoja pindifu ya Profesa Lipumba. Hili la pili liko katika mfumo wa swali. Na swali lenyewe ni je, nani hasa kashindwa kazi kati yake yeye Profesa Lipumba na Rais Kikwete?

  Tulijibu swali hili kwa ufupi tu kuonyesha kushindwa kwa Lipumba katika uongozi mzima wa chama kisichochagulika. La kwanza ni lazima tukubali kuwa ni kitendo cha kushindwa kwa mtu mwenye elimu, upeo, uzoefu na ujuzi wa mambo kama alivyo Lipumba kutoka chama kama CCM na kuingia chama kama CUF, na bado akaendelea kujiaminisha kuwa anaweza kupewa ridhaa ya kuongoza nchi na Watanzania.

  Inahitaji mtu ambaye hajapata kuishi Tanzania kabisa kufanya uamuzi kama aliofanya Lipumba kuingia chama kisichoaminika kwa sababu ya udini, kisichochagulika kwa sababu ya kutoaminika, na kilichoshindwa kwa zaidi ya miaka 15 sasa kusambaza mtandao wake na ufuasi nje ya eneo dogo tu la nchi hii, yaani Kisiwa cha Pemba. Hili la kwanza. Miaka yote hii, ameshindwa kufurukuta kutoka nje ya Pemba. Sasa nani hasa kashindwa kazi?

  La pili katika kujibu swali la nani kashindwa kazi ni kuangalia historia ya Lipumba na Kikwete katika kusaka uongozi. Lipumba ameanza harakati za kuwania urais tokea uchaguzi wa kwanza kabisa wa vyama vingi mwaka 1995.

  Aligombea mwaka 1995, akashindwa vibaya na Rais Benjamin Mkapa. Akajaribu tena mwaka 2000 akashindwa tena na Mkapa. Akajaribu tena mwaka 2005 dhidi ya Kikwete, anajua kilichompata.

  Sasa nani hasa kashindwa kazi? Huyu ambaye amekuwa mgombea na mshindwa mzoefu wa urais, ama mwenzake ambaye kasi yake ya kupata alichokiwania haihitaji kuelezwa kwa yoyote?

  Tatu katika kujibu swali la nani kashindwa kazi ni kuangalia mafanikio ya Lipumba katika kujenga ushawishi wa CUF kuungwa mkono na Watanzania. Tokea kuundwa kwa chama chake na tokea yeye kuongoza chama hicho, CUF imepata ufuasi wake na wabunge wake kwa asilimia 99.99 kutoka Pemba.

  Katika Unguja, CUF chini ya uongozi wa Lipumba imesusua vibaya mno. Kwa sasa ina kiti kimoja tu katika Unguja kwenye Jimbo la Ngome Kongwe. Huko Bara ndiyo kabisa, ni aibu. Imeshinda viti viwili tu katika miaka yote ya uongozi wa Lipumba. Kimoja cha Kigamboni, Dar es Salaam kilipata kushikiliwa na Frank Magoba kwa kipindi kimoja tu.

  Cha pili, cha Jimbo la Bukoba Mjini wakati wa Wilfred Lwakatare; sasa nacho kimeota mbawa, kama alivyoota mbawa Lwakatare mwenyewe ambaye amekwenda CHADEMA. Hivyo katika eneo zima la Tanzania Bara, CUF chini ya Lipumba haina hata kiti kimoja. Nani hasa kashindwa kuongoza? Bila shaka atakuwa ni mwenye wabunge sifuri Bara.

  Nne, katika kugombea kwake urais, hali ambayo ni rekodi ya Tanzania mpaka sasa, akishindana na Katibu Mkuu wake, Seif Shariff Hamad kwa urais wa Zanzibar, hajapata kuvuka zaidi ya asilimia 10 ya kura zote za urais.

  Sasa nani kashindwa kazi? Huyu anayepiga asilimia 82 katika jaribio lake la kwanza ama yule wa chini ya asilimia 10 miaka nenda, miaka rudi.

  Lipumba ana nini cha mafanikio ya kuonyesha katika miaka yote hii, ukiondoa uvumilivu wa kuheshimika, kwa kweli, wa kubakia katika chama cha upinzani kisichokuwa na dira wala mwelekeo, ama matumaini ya ushindi. Uvumilivu huu, kwa hakika, ni wa kuheshimika.

  Maadamu sasa tumetoa ushahidi kuthibitisha kuwa ni Profesa Lipumba aliyeshindwa kazi na wala siyo Rais Kikwete, sasa tuangalie hoja ambazo Lipumba anajengea tuhuma ya kwamba Rais Kikwete ameshindwa kazi.

  Lipumba anasema kuwa Rais Kikwete ameshindwa kumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar, na kwamba ameshindwa kupambana na matatizo ya sekta za elimu, afya na nishati.

  Kama nilivyosema hapo juu, Lipumba anasema mambo kama vile hajapata kuishi katika nchi hii. Hivi nani asiyejua kuwa ni CUF ambayo imekwamisha kufikiwa Mwafaka wa Zanzibar kwa sababu inakataa kurejea kwenye meza ya mazungumzo ya kumaliza mpasuko huo.

  Kwa hakika, CCM na CUF, zimemaliza tofauti zao kuhusu Zanzibar. Tofauti iliyopo ni jinsi ya kutekeleza yaliyofikiwa; CCM ikisema kuwa makubaliano hayo yaende kwa wananchi kwa kura ya maoni, CUF ikisisisitiza kuwa saini za Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba na mwenzake Seif Shariff Hamad wa CUF zinatosha kuhalalisha mageuzi makubwa kiasi hicho katika mstakabali mzima wa Zanzibar.

  CCM inashikilia kupata ridhaa ya wananchi kwa sababu mageuzi hayo, yatabadilisha mwelekeo mzima wa siasa na Katiba ya Zanzibar kwa kuundwa kwa serikali ya Mseto, CUF inasema saini za Makamba na Hamad zinatosha. Nani asiyeoona nani anafanya usanii hapa?

  Kuhusu elimu, Lipumba haihitaji kukumbushwa kuwa ni Rais Kikwete aliyeleta mageuzi makubwa katika mfumo wa elimu ya Tanzania kuliko mwingine yoyote ukiondoa mwanzilishi wa taifa hili, Mwalimu Julius Nyerere. Leo hii, hakuna mtoto wa Tanzania anayeshindwa kuingia sekondari kama ameshinda mtihani kwa sababu sasa nafasi zinatosheleza mahitaji.

  Tusisahau jambo moja. Shutuma hizo za Profesa Lipumba zilitolewa wakati akizindua "Operesheni Zinduka"- yaani, kwa maelezo yake mwenyewe, dira mpya ya chama cha CUF kuelekea kwenye uchaguzi mkuu mwakani.

  Ishara moja ya kushindwa kwa sera za chama chochote cha siasa ni kuanzishwa kwa shughuli zinazoitwa "operesheni." Chama kina sera inayojulikana, sasa kinahitaji operesheni ya nini? Chama chochote kinachoanzisha operesheni maalum kinakiri udhaifu wa sera zake.

  Kwa hakika kinazidi kuwachanganya zaidi wananchi, na hasa wafuasi wake, kwa kuwalazimisha wachague kati ya kufuata sera za chama chenyewe, ama matakwa ya operesheni maalum inayouzwa kwa wananchi kwa ghiliba kubwa mno. Hapa linakuwa limekuwa suala la kufa ama kupona.

  Chama kinachokwenda vizuri hakihitaji msukumo wa operesheni maalum ya aina yoyote. La kuvunda halina ubani. Operesheni hizo zote, iwe ni Operesheni Zinduka, Operesheni Sangara ni kiini macho, ni ishara isiyopingika ya chombo kwenda mrama.

  Makala hii imeandikwa na Salva Rweyemamu katika nafsi yake binafsi, na wala siyo kwenye nafasi yake rasmi ya Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Rais (DPC). Inaelezea tu mawazo na maoni yake binafsi na wala haiashirii maoni ama mawazo ya Ikulu ama ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  I can't imagine mkurugenzi wa habari ikulu anaweza kuwa na hoja finyu namna hii!!!!!! Hata kijiweni watu wanajenga hoja nzito na constructive compared to this rubbish. This tells me much about the qualifications, understanding and ability of who employed him.
   
 3. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,288
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Salva anasema udini wa CUF ndio umefanya chama hicho kubakia Pemba tu, hivi huko Unguja kuna dini gani tofauti na Pemba? Amakweli Rostam kavuruga kabisa bongo za hawa vibaraka wake!
   
 4. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,372
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kama wanasiasa wetu wako shallow basi na majibu yatakuwa ya hovyo hovyo...
   
 5. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Pia Salva amesahau kusema Lipumba anagombea bila kuiba kura, bila kuwa na jeshi la polisi linalopiga mabomu wapinzani, bila kuwa na propaganda za RTD, bila kuwa na miundombinu ya CCM waliyopora kwa wananchi wa Tanzania na bila kuwa na support ya mafisadi.
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Pole sana salva. Nakusikitikia kwa majibu yako ya ovyo ovyo kwa jamii.

  Nipo tayari kwa lolote.
   
 7. K

  Kitoto Akisa Member

  #7
  Jul 17, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri amesahau pia kuwa Kikwete hakuanza kampeni za kuwania kuingia ikulu mwaka 2005, labda tumuulize, je anajua Ben Mkapa alishindana na nani katika ile hatua ya mwisho ya kutafuta uteuzi wa CCM kwa nafasi ya Rais, inawezekana hata hili amesahau pia. Sijui ni kusudi au anafumba tu macho, tumkumbushe pia ripoti ya REDET juu ya umaarufu wa JK ulivyoshuka!
   
 8. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Hivi unataka tuamini hicho unachokifikiria wewe au unataka tujadili hoja za Salva, kama unataka tujadili hoja za salva bandika hiyo makala na si hizo hisia zako, unadhani hatujasoma au unataka kuwakusanya wavivu wa kusoma uwalishe huo upupu.Kama una ubavu ibandike hapa alaaaa!
   
 9. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  lakini wana JF kwanini lipumba asiende kugombea ubunge WETE huko PEMBA mi naona yeye na chama chake huku Bara hoi namuomba akajaribu chakechake, wete au wawi kwani akigombea ubunge hata tabora kwao atakosa he is tired enough politicaly to have a sleep rest in pemba.
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli

  haya hivi huyu Salva anatumia platform gani kutoa taarifa hizi?
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Si Lipumba wala Salva, wote wanacheza tu. Na ninaweza kuandika ki-booklet hapa kwa nini.
   
 12. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Lipumba hakumpatia Salva ile nakala ya barua yake wa RA iliyotundikwa hapa? Labda ingemsadia Salva kukaa kimya badala ya kuendelea kuchafua jamvi
   
 13. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #13
  Jul 17, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  how can some ikulu PR be objective? tell me where that has ever happened on earth?
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ukiona watu wanaanza kumsakama Lipumba ujuwe mizinga ya zinduka imeanza kufanya kazi ,kikweli kweli na karibuni wakishashindwa na matangazo watatuma majeshi kwenda kuwapiga wafuasi na kuwakamata viongozi wa CUF ,ila CUF hapo ndipo inapopatafuta kwa udi na uvumba.
   
 15. Mukuru

  Mukuru Member

  #15
  Jul 18, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatukutegemea majibu tofauti kutoka kwa Salva...afterall unamtetea mwajiri wako. Tatizo ni pale Salva anaposhindwa kuja na nguvu ya hoja na kujibu maswali magumu kwa majibu mepesi mepesi. Labda ana woga asije akafurushwa na tajiri yake....Salva anazingatia usemi kuwa MTUMIKIE KAFIRI UPATE MRADI WAKO. Ukweli anaujua lakini yuko tayari kuupindisha ili tajiri yake aendelee kumpa makombo.
   
 16. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Chochote anachosema ama anachoandika Rweyemamu ni tamko rasmi la Ikulu kwa wakati huu labda mpaka hapo atakapojiuzulu ama kuachia nafasi aliyonayo.
  Na kama hayo ndiyo majibu ya ikulu kuhusu hotuba za Lipumba basi kuna kazi kweli kweli katika ofisi husika huko Ikulu.

  Majibu aliyotoa Rweyemamu yanasikitisha kwani hata mwanangu wa miaka sita angekuja na majibu mazito kuliko hayo.
   
 17. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa nini mwanakijiji asiwe mwandishi wa ikulu? Salva uwezo wake wa kuchambua mambo ni shallow mno. Kama angeacha siasa awe objective mbona kuna mambo mengi ya kuandika kwa kujenga hoja nzito tu? Asilimia 99% ya barua ni political na personal attacks. Mafanikia pekee ya Kikwete kama rais aliyotaja ni wingi wa watoto kuingia shule za sekondari (hajasema lolote kuhusu quality of education, miundombinu ya shule, maslahi ya walimu, nk.)

  Yaani yeye Salava ushindi wa CCM ndio mafanikio ya Kikwete? Nadhani alitakiwa kuonyesha ushindi wa CCM ni dhamana aliyopewa Kikwete kuwaletea wananchi maendeleo na ndio dhana nzima ya ushindi na mafanikio hiyo. Ushindi wa CCM (kisiasa) si mafanikio ya kimaendeleo ila ni nyenzo ya kufikia hayo mafanikio. Salva ameshindwa kutofautisha kati ya process na achievements! Hana uwezo wa kazi anayoifanya, ndio maana kaogopa kuongea kwa capacity ya wadhifa wake.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Jul 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh! ama kweli taifa lka NDIVYO TULIVYO kaaazi kweli kweli..
  Yaani mkurugenzi wa habari IKULU anaweza kuzungumza JIBU la hojalikaitwa ni binafsi na yasichukuliwe kama ni majibu ya IKULU!..
  Hivi Kikwete ni wakati gani anaweza kuzungumza mawazo yake binafsi, au mkurugenzi wa wiizara anaweza kuzungumzia jibu la swala linalohusiana na wizara yake lisiwe jibu la wizara..
  Jamani nipeni somo hapa maanake nashindwa kabisa kuunganisha..hayo majibu ya Ikulu yatakuwa na tofauti gani vile!. Kama yeye ni mkurugenzi wa IKULU hutakiwi kabisa kuzungumza maswala nyeti kama haya bila idhini ya Ikulu.. ndio kazi aloajiriwa KUSEMA kwa niaba ya IKULU..ni bora aseme No comment kuliko kuiweka Ikulu kati ya mawazo yake na yale ya Utawala..
   
 19. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0


  MKJJ anafaa huku huku alipo

  kule hakumfai kwani kuna ma SNOBS ile mbaya

  hata salva mwenyewe nadhani unajua kama hajakubalika

  Kwanza si Mtanzania

  pili shule yake ndogo

  tatu hapendwi na waandishi toka mirengo yote

  Nnne he;s narrow minded piece of twat ndio maana mpaka leo Ikulu haina website
   
 20. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nadhani tatizo kubwa hapa sio Salva bali ni Saidi Kubenea. Unapoona gazeti "machachari" linatoa makala binafsi za msemaji wa Ikulu tena kwa wazi kabisa na kutumia jina lake tofauti na hapo mwanzoni walipokuwa wanatumia majina kama "na mwandishi wetu" ama "saidi kubenea" basi ujue hali ni mbaya sana....

  Salva anatekeleza wajibu wake....Kumtetea mwenye IKULU kwa wakati huu. Inawezekana baadaye ikambidi amtetee Lipumba endapo "kura zitatosha kwa mujibu wa wanaohesabu na sio wapiga kura"

  Huyu HERO wetu naona ameshaanza kuingia mkenge wa kulimaliza gazeti lake.

  omarilyas
   
Loading...