Salva kuondolewa Ikulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salva kuondolewa Ikulu

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Zak Malang, Apr 9, 2009.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF -- kuna tetesi kwamba Salva Rweyemamu,Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu huenda akahamishwa na kupewa kazi nyingine. Hivi sasa Salva kaenda likizo ya muda usiojulikana, na kwamba likizo hiyo inaambatana na "masomo" huko n'gambo.Fuatilieni tetesi hizi.

  Inasemekana Salva aliukwaa wadhifa hapo Ikulu kutokana ushawishi mkubwa wa swahiba wake --Rostam na na EL, na inadaiwa jukumu lake kubwa lilikuwa ni kushughulikia kuzifunika kashfa za Richmond na Kagoda.

  Baada ya kuukwaa wadhifa huo hapo Ikulu mara moja akahodhi kazi ya usemaji wa Rais na kupachikwa jina la "Alfred Mutua" wa Tanzania, kazi ambayo ilionekana baadaye alinyang'anywa baada ya kuwa msemaji wa kila wizara.
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duh kuna kaukweli flani ndani yake....wazee wa DATA watashuka.
   
 3. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Leteni data za ukweli, tusijadili tetesi tu.
   
 4. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tupo sebuleni tunasubiri leteni chakula huku!!!
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Tetesi Tetesi Tetesi Tetesi Tetesi Tetesi Tetesi Tetesi...too much! Baadaye Tetesi Tetesihugeuka nakuwa uzushi ama ushuzi!
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Hapo hizo fact zako hazijakaa sawsawa angalia timing ya yeye kupewa kazi hiyo na vurugu za Richmond na Kagoda. Huyu bwana alipewa kazi hiyo kama zawadi baada ya utumishi ''uliotukuka'' wakati wa kampeni ya mkulu.

  Hii kali unajua kama amechukua likizo ya masomo sasa tetesi ipo wapi tena hapo? Maana ni kama ulianza na jibu halafu mwisho ukauliza swali.

  N.B wakati anakuwa mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, wizara hazikuwa na utaratibu mzuri wa mawasiliano ya umma, hivyo sehemu ya kazi yake pia ilikuwa ni kuanzisha/kusaidia kuanzisha utaratibu huu katika wizara, nadhani hii ndio sababu iliyomfanya aonekane kama msemaji wa kila wizara.
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Burn:

  1. Inawezekana alipewa hiyo kazi kutarajia kwamba endapo hizo kashfa mbili zingelipuka, angetakiwa kusimamia moto wake. Walikuwa na wasiwasi mkubwa kulipuka.

  2. Likizo -- hata kama ni za masomo -- mara nyingine huwa ni namna ya tu yua kumuondoa mtu ktk wadhifa wake -- na hiki si kitu kigeni.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Huyu na Tido, Badra walifanyakazi "nzuri" sana wakati wa kampeni 2005 kwenye vyombo vya habari walivyokuwa wakiviongoza. Nakumbuka Tido aliihamishia BBC kule Dodoma wakati uteuzi wa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Salva alihangaika sana na Sumaye kwenye magazeti yao.
   
 9. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Mkuu Zak
  Hata kama tunamfikiria mkulu ni kilaza kiasi gani, hii strategy asingeweza kuitumia, kutumia Ikulu ku cover kashfa kubwa hivi..gimme a break. Iwapo Salva angekuwa anatakiwa ku cover Richmond au Kagoda angebakia tu mwandishi wa magazeti kwani huko angefanya kwa uhuru zaidi bila kuwa connected na ikulu kama ambavyo baadhi yao wanafanya na wote hatuna uhakika nani kawatuma.
  Kwa kuwa sijawahi kufanya kazi katika sekta ya umma siwezi kusema kitu kuhusu hilo la masomo lakini napata taabu kuamini kuwa. salva alitafutiwa shule na waajiri wake akasome kwa lengo la kumuondoa kwenye wadhifa wake. Hii ni kazi ngumu sana maana kusoma ni lazima na yeye akubali na pia awe na sifa za hicho atakachosomea sidhani kama hivi unaweza kuvifanya kwenye mazingira ya kumuondoa mtu kwenye madaraka yake.
   
 10. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,078
  Likes Received: 1,724
  Trophy Points: 280
  That is how the state works my dear; it does not follow the conventional logic you might be knowing!
  Those who are luck that they cannot die they are dispatched as such. Similarly one can refer to the experience of Hassan Benseni Kitine (concocted his names as Hassy Bensen Kitine), the former intelligence chief. He was dispatched to Canada in the early 1980s when he became state liability!
  Ni hayo tu ndugu.
   
  Last edited: Apr 9, 2009
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli usiopingika kuwa Salva aliwekwa Ikulu na RA na Lowasa for thieir interest!!! Hatujui kama interest in Salva atoe habari njema kwa ajili ya ku upgrade Jk au kama awe pale ili kummaliza!!! Nia kamili anaijua RA na Lowasa kwa sababu the next president was expected to be Lowasa (after JK's term - whether one or two trems wao wana jibu kamili). Tukumbuke kuwa kila eneo muhimu la nchi (Ministries, Departments and Agencies) RA na Lowasa wali influence ni nani awe hapo kama kiongozi, only for their interests!!!! Salva aliondolewa ikulu lazima kuna a secret behind the move, wao wanaijua mimi siifahamu. Ila tu generally, Salva has been dormant in his post!!!! Arudi tu private akaendelee na kazi huko, pengine RA atamchukua tena kule.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Apr 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Baada ya kina Nguba kupata nafasi ofisi ya Waziri Mkuu na wengine waliokuwa kundi moja kuonekana kukumbukwa Salva alibakia bado Habari Corp. Alipoona kimya aliandika barua moja ndefu kwenda kwa Rostam (ambayo kijiji kina nakala yake); katika barua hiyo Salva aliamua kumtolea uvivu Rostam juu ya mambo kadha wa kadha, lakini mwishoni alilalamika na kuuliza mbona yeye hakukumbukwa kama ilivyokuwa ahadi yao (kina Rostam)... ilikuwa wiki chache baadaye aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais.
   
 13. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mhh shauri zao bana
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Baada ya kina Nguba kupata nafasi ofisi ya Waziri Mkuu na wengine waliokuwa kundi moja kuonekana kukumbukwa Salva alibakia bado Habari Corp. Alipoona kimya aliandika barua moja ndefu kwenda kwa Rostam (ambayo kijiji kina nakala yake); katika barua hiyo Salva aliamua kumtolea uvivu Rostam juu ya mambo kadha wa kadha, lakini mwishoni alilalamika na kuuliza mbona yeye hakukumbukwa kama ilivyokuwa ahadi yao (kina Rostam)... ilikuwa wiki chache baadaye aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais."
  __________________

  MKJJ:

  1. Mzee wetu, hebu tuwekee hapa hiyo barua, and I'm sure it will an interesting reading.

  2. Kuna mwingine mtu wa RA aliyesahauliwa na hadi sasa yuko Habari Corp kama Managing Editor, Muhingo Rweyemamu. Huyu aliwahi kuwaMhariri wa Habari gazeti la Mwananchi na alitimuliwa wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea urais 2005 baada ya kugundulika kumhujumu mgombea mmoja wa Urais – Dr Salim - kwa kuchapisha picha ya kughushi katika gazeti jilo.

  Katika kampeni za JK za 2005 alikuwa ktk msafara wake na ndiyo alikuwa mgawaji wa pesa kwa waandishi. Alitegema kuula U-RC, au angalau u-DC. Hakupata chochote na inasemekana hadi reshuffle ya juzi ya ma-DC alikuwa antarajia kuukwaa.

  Wakati Rosemary Mwakitwange akiwa CEO Habri Corp alimtimua Muhingo pamoja na waandishi wengine – Deodatus Balile na Manyerere Jackton kwa kukosa maadili ya uandishi, lakini baada ya Rosemary kujitoa, RA aliwarudisha.
   
 15. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  mmmmhhh hii kali! Mkuu Mwanakijiji unatisha!
   
 16. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni toleo lingine la wanii wa ikulu,tutaendela kuimba hadi 2010.
   
 17. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa Uongozi wa kupangiana hivi kama umafia,ufalme au uongozi wa kijeshi ni uongozi gani,hivi JK anasikia/anaona maoni yetu hapa JF.Tulishamshauri mara nyingi apangue umangimeza wa RA na EL kwenye uongozi hapa nchini lakini tukaambulia kurudishiwa maDCs wa watu walewale au JK bado ana ubia na hao mafisadi,lakini wana JF tusichoke kushauri kuna siku JK atatuelewa au nguvu ya umma itafanya kazi.Mungu ibariki Tanzania.
   
 18. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #18
  Apr 9, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa Uongozi wa kupangiana hivi kama umafia,ufalme au uongozi wa kijeshi ni uongozi gani,hivi JK anasikia/anaona maoni yetu hapa JF.Tulishamshauri mara nyingi apangue umangimeza wa RA na EL kwenye uongozi hapa nchini lakini tukaambulia kurudishiwa maDCs wa watu walewale au JK bado ana ubia na hao mafisadi,lakini wana JF tusichoke kushauri kuna siku JK atatuelewa au nguvu ya umma itafanya kazi.Mungu ibariki Tanzania.
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Apr 9, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  Maane, Mmaroroi

  ..Rostam na Lowassa ndiyo waliomuweka JK ikulu. suala la Salva Rweyemamu linapaswa kuwa a no brainer.

  ..sijui kwanini wananchi wanakuwa wazito kuelewa kwamba Rostam,Lowassa,na Kikwete, ni kitu kimoja.
   
 20. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35

  Kama ni tetesi na ziendelee kuwa tetesi mpaka hapo itakapokuwa tukio.
   
Loading...