Salum Rashid Hamduni kutoka ACP mpaka CP. Je, ndiye IGP ajaye baada ya Sirro kustaafu?

hapo amepandishwa ili kuipa heshima chombo/mhimili anaoenda kuuongoza, maana haiwezekana akaenda takukuru na cheo kidgo ndani ya polisi kwa kuwa bado atakuwa anawa salute ma ofisa wengine ndani ya polisi wakati tayari ana nafasu kubwa ndani ya chombo kingine, ndo maana akapewa cheo kikubwa ndani ya polisi baada ya igp yeye ndo anafuata kwa sasa ndani ya polisi...inampa heshima kwa ma ofisa wote ndani ya jeshi la polisi kasoro igp..
Si kweli ulivyosema baada ya IGP yeye ndiye anayefuata Polisi kuna makamishna wengine kama kamishna wa intelegensia,kamishna wa utawala,kamishna anayehusika na masuala ya operesheni, kamishna wa upelelezi,kamishna wa Zanzibar,kamishna wa Polisi jamii.

Hao wametangulia kuwa makamishna (seniors) Hamduni atakuwa na madaraka makubwa lakini akikutana nao atawapigia saluti.
 
Makao makuu ya polisi wewe ulienda kufanya nini?
Hii ni JF I'd feki ndio zimetawala, Kuna watu wa Kila aina...unaweza kumtukana member humu kumbe ni Baba yako,Boss wako,Kamanda wako, Waziri wako ama kiongozi yoyote yule wa juu.

Viongozi kama akina Zitto, Mwigulu,Dr Slaa, Mbowe, Mnyika na wengine Wana I'd humu hivyo kwa uzoefu wao usishangae Wana I'd feki za kuingilia jukwaa la MMU.
 
Hamduni aligoma kabisa kupelekeshwa pelekeshwa na Ole sabaya pale Kilimanjaro!
Kuna watu hawakuelewi kabisa ukisema Sabaya alikua "anapelekesha" wanamuona ni mtoto makini wa baba. Hii inatokana na kwamba hata baba mwenyewe hataki kusikia kwamba kuna mahala alifanya vibaya. Wao kwao wanaona huyo ni baba bora kuwahi kutokea, na kwamba hatatokea mwingine kama huyo. Wamegoma kukubali.
 
Sasa mkuu kupanda kutoka ACP mpaka SACP kunahitaji siri gani? Na hiyo siri ni kwa ajili ya nini ?
usipende kuelezea kila kitu hata usivyokuwa na uhakika navyo.

usivyovijua haimaanishi ni siri,na unavyovijua haimaanishi ni haki yako kuvijua..
 
ndio sababu umeambiwa huelewi unachoandika,kama ni vyeo hata hivyo vya jwtz vina siri gani??

Nikianzia na TISS kwanza TISS yeyote yule hata mfagiaji au daktari hatakiwi ajulikane kuanzia mwanzo

JWTZ , Nao pia hawatakiwi wajulikane sababu TISS na JWTZ ni interdisciplinary yaani nao pia ni watu nyeti i.e jeshini hata private tu anaweza kutumiwa na majasusi
 
Pamoja na kuteuliwa kuwa mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa pia bwana Hamdun amepandishwa cheo kutoka kuwa ACP mpaka kuwa CP ikiwa na maana amerukishwa vyeo vya SACP na DCP je ndio IGP ajae baada ya kamanda Sirro kustaafu?

Ngoja tusubiri tuone


Amenyoka sana, Kazi yake ni safi sana! Haki bin haki, Muislam safi kabisa!
 
Nikianzia na TISS kwanza TISS yeyote yule hata mfagiaji au daktari hatakiwi ajulikane kuanzia mwanzo

JWTZ , Nao pia hawatakiwi wajulikane sababu TISS na JWTZ ni interdisciplinary yaani nao pia ni watu nyeti i.e jeshini hata private tu anaweza kutumiwa na majasusi
Rank za jeshi zina siri gani? Mbona zinawekwa mabegani tunaziona? Hata historia ya kupanda rank kwa askari kuna siri gani? Hueleweki unataka kueleza nini?
 
Rank za jeshi zina siri gani? Mbona zinawekwa mabegani tunaziona? Hata historia ya kupanda rank kwa askari kuna siri gani? Hueleweki unataka kueleza nini?

Mabeyo alivyopandishwa cheo mwaka 2015 uliona taarifa yeyote imetolewa ? In short waliopo mtaani hawawajui majenerali wote , vyeo vya jeshi ni nyeti kuna vyeo vya juu hata mashirika ya kijasusi huwafanyia profiling kwenye ripoti za kijasusi
 
Back
Top Bottom