Salum Mwalimu hajui kuzungumza na waandishi wa habari. Akajipange upya

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,017
..Salumu Mwalimu amepoteza nafasi nzuri ya kueleza msimamo wa chama chake na aina ya demokrasia wanayodai kuitetea.

..Fuatilia ktk video clip swali aliloulizwa na majibu aliyoyatoa.

..kosa kubwa analofanya ni kuwasilisha hoja zake kwa UKALI na KUFOKA.

..ajifunze kuwa MTULIVU na ajenge hoja kwa nia ya KUSHAWISHI na kutafuta kuungwa mkono.

..njia anayotumia kuwasilisha hoja yake inawafanya wale wanaomsikiliza wamuone kwamba amekamilika, na hahitaji msaada, au uungwaji mkono wa aina yoyote ile.

..jambo lingine anapaswa kufahamu uwezo wa waandishi wa habari wa Tz. waandishi wetu wanahitaji "kutafuniwa" kila kitu, halafu waripoti. Ni makosa kutegemea waandishi wetu wa habari kufanyia uchambuzi matamshi ya wanasiasa mbalimbali na kutenganisha "mchele" na "pumba."

cc Erythrocyte , tindo, Nguruvi3
 
Huyu bora angerudia tu taaluma yake ya utangazaji channel ten..mbowe alimdanganya ubunge kipindi kile akiripoti mikutano ya oparesheni sangara..akajaa
 
umesikika mkuu , tutalifanyia kazi

..chama lazima kiwe na sekretariat imara inayofanyia utafiti mbalimbali na kuandaa madokezi kwa ajili ya viongozi.

..kosa ninaloliona ni viongozi wa chama kijitokeza kwa waandishi wa habari na kuzungumza bila ya kuwa wameandaa nini wanataka kuzungumza.

..lazima viongozi wazungumze mambo ambayo wananchi wanataka wayazungumze, na kwa namna ambayo wananchi wanapenda kusikia.

NB.

..pamoja na mapungufu niliyoyaona nimependa aliposisitiza suala la HAKI, DEMOKRASIA na MAENDELEO. anachotakiwa ni kutafuta namna ya kuwashawishi wananchi kwamba anazungumza kwa niaba yao, na siyo kwa niaba ya CDM.
 
Mwalimu amefanya kazi nzuri sana kwenye hiyo press conference, amekosea kwenye hiyo sehemu ya swali la mwandishi, kama mwandishi kauliza swali then wewe muulizwa swali unapaswa kujibu swali siyo kuanza kumuuliza mwandishi swali.

Mwalimu lazima ajue kuwa kila mwandishi ana opinion zake katika mambo kadha wa kadha lakini huuliza maswali ili wapate majibu kwa ajili ya kuripoti, kupanua taarifa, kuondoa sintofahamu na kadhalika.

Kwenye hili suali la huyo mwandishi Salum Mwalimu kachemsha, huo ndo ulikuwa muafaka wa kubuild up kwenye kauli ya mnyika, kuleta more awareness ya kauli ya Mnyika kwa watu, na kuifanya kauli ya Mnyika iendelee kuwemo katika news cycle, lakini kwa bahati mbaya au sijui ni uoga wa Mwalimu akaona ayeyushe. Kazingua sana kwa kweli kuhusu hilo swali, alipaswa apigilie nyundo kwelikweli kuhusu hali ya demokrasia n.k
 
..Jiwe alifanya upotoshaji mkubwa kuhusu malengo ya vyama vya upinzani.

..sasa mwandishi ktk swali lake ni kama alikuwa anampa nafasi Salum Mwalimu kupinga upotoshaji wa Jiwe.

..ni bahati mbaya kwamba Salum Mwalimu hakutambua fursa iliyopewa na mwandishi wa habari na kuitumia ipasavyo kwa manufaa ya chama chake.
 
..Salumu Mwalimu amepoteza nafasi nzuri ya kueleza msimamo wa chama chake na aina ya demokrasia wanayodai kuitetea.

..Fuatilia ktk video clip swali aliloulizwa na majibu aliyoyatoa.

..kosa kubwa analofanya ni kuwasilisha hoja zake kwa UKALI na KUFOKA.

..ajifunze kuwa MTULIVU na ajenge hoja kwa nia ya KUSHAWISHI na kutafuta kuungwa mkono.

..njia anayotumia kuwasilisha hoja yake inawafanya wale wanaomsikiliza wamuone kwamba amekamilika, na hahitaji msaada, au uungwaji mkono wa aina yoyote ile.

..jambo lingine anapaswa kufahamu uwezo wa waandishi wa habari wa Tz. waandishi wetu wanahitaji "kutafuniwa" kila kitu, halafu waripoti. Ni makosa kutegemea waandishi wetu wa habari kufanyia uchambuzi matamshi ya wanasiasa mbalimbali na kutenganisha "mchele" na "pumba."

cc Erythrocyte , tindo, Nguruvi3
Jamaa wenu joka kuu la entraprunyuaship anajua kuongea???
 
..chama lazima kiwe na sekretariat imara inayofanyia utafiti mbalimbali na kuandaa madokezi kwa ajili ya viongozi.

..kosa ninaloliona ni viongozi wa chama kijitokeza kwa waandishi wa habari na kuzungumza bila ya kuwa wameandaa nini wanataka kuzungumza.

..lazima viongozi wazungumze mambo ambayo wananchi wanataka wayazungumze, na kwa namna ambayo wananchi wanapenda kusikia.

NB.

..pamoja na mapungufu niliyoyaona nimependa aliposisitiza suala la HAKI, DEMOKRASIA na MAENDELEO. anachotakiwa ni kutafuta namna ya kuwashawishi wananchi kwamba anazungumza kwa niaba yao, na siyo kwa niaba ya CDM.
asante mkuu
 
Hio ni kama presentation tu ya Darasani, kama hujajipanga huwezi kwenda nayo sawa..
 
Waandishi Wa habari wana maswali ya mitego sana ndo maana jiwe huishia kusema MAYALA KIKWETU NI NJAA maana maswali mengine ni sumu

Sasa huyu jamaa siku akikutana na akina Pascal mayala si atarusha ngumi kabisa
 
..Salumu Mwalimu amepoteza nafasi nzuri ya kueleza msimamo wa chama chake na aina ya demokrasia wanayodai kuitetea.

..Fuatilia ktk video clip swali aliloulizwa na majibu aliyoyatoa.

..kosa kubwa analofanya ni kuwasilisha hoja zake kwa UKALI na KUFOKA.

..ajifunze kuwa MTULIVU na ajenge hoja kwa nia ya KUSHAWISHI na kutafuta kuungwa mkono.

..njia anayotumia kuwasilisha hoja yake inawafanya wale wanaomsikiliza wamuone kwamba amekamilika, na hahitaji msaada, au uungwaji mkono wa aina yoyote ile.

..jambo lingine anapaswa kufahamu uwezo wa waandishi wa habari wa Tz. waandishi wetu wanahitaji "kutafuniwa" kila kitu, halafu waripoti. Ni makosa kutegemea waandishi wetu wa habari kufanyia uchambuzi matamshi ya wanasiasa mbalimbali na kutenganisha "mchele" na "pumba."

cc Erythrocyte , tindo, Nguruvi3

Mpaka DOVUTWA ameungana na vyama vya upinzani? kweli vyuma vimekaza...
 
Akianzisha mada na kutoa maoni ya aliyoyasikia mleta hoja huyu huweka nukuu, picha na video kila inapowezekana ili na sisi tusikie wenyewe. Tremendous work, maana kuna jitu linaweza kuandika “Warwanda wana miguu ya chupa na chura za kuning’inia,” ukifungua mada huoni chupa wala chura.

Let me harken back to the substantives.

Kuhusu hulka ya Salum kuongea kwa hamasa na jazba, nadhani ni style tu ambazo hazina madhara, na hata ukiangalia historia zote, distant and contemporary, utakuta hata wa kina Malcolm X na kina Tundu Lissu wanaongea kwa jazba na ujumbe huwa unapata support kubwa duniani.

SALUM MWALIMU amempa ujumbe mwandishi kwamba kama wanaelewa vinavyoendelea na wao wana wajibu wa kuchambua, kufafanua na kupinga uongo wa wazi wazi unaoenezwa na yeyote yule kwenye jamii bila kuwategea mitego wapinzani ndio “wafafanue.”

Donald Trump akiongopa waandishi huwa hawaendi kuwategeshea mic democrats ndio waseme Trump anaongopa, wanachana wao wenyewe waandishi! And nobody on this board knows this better than you, Jokakuu.

Nilimsikia Rais akimjibu Mnyika, demokrasia tunayodai Watanzania ni ya kuandamana na kuvunja maduka, pale pale nikajiuliza hii wapi imetokea hii?

KWA NINI WAANDISHI WA TANZANIA NA WENYEWE WASIANDIKE, WASICHAMBUE, KUFAFANUA NA KUJIULIZA NI MAANDAMANO GANI YA UPINZANI, LINI NA WAPI, YALIVUNJA MADUKA?

Mwandishi vipi huyu?

Statement ni ya Rais. Rais kasema demokrasia tunayotaka sisi ni kuvunja maduka. Kwa nini upinzani ndio uambiwe UFAFANUE kauli ya Rais ???
 
Back
Top Bottom