Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 58,997
- 103,382
Jamani Siasa hizi za kuchimbana mambo ya familia ni kukoseana adabu,mambo ya faragha na familia yabaki kuwa sehemu ya familia.Hali hii inawaumiza watoto ambao hawajui "vita" hivi vya kisiasa.
Niliposikia Mwigulu Nchemba anasema atafanya siasa za kistarabu uchaguzi mdogo Kinondoni,tulidhani wanamaanisha,kumbe ni ovyoo.
Sasa hawa watoto mnaanza kuwaanika ili tu kujibu tuhuma za Wahuni wanaoacha sera na kutukana watu?Tukianza kufukua hayo mambo wengi wataaibika.
Tutaanza kuangalia mahusiano ya kuanzia Raia Namba moja mpaka diwani,tutafukua makaburi na kusema maisha yao kabla ya vyeo vyao,halafu tutasema,hawa kama familia iliwashinda ilikuwaje tumewapa nchi?Haya mambo mengine acheni,mtasababisha watu tuongee halafu Maxence Melo aanze kusumbuliwa
Mkuu barafu nashukuru kwa kuona huu upuuzi. Huwa ninamsikiliza mkuu akiwa jukwaani anasema maendeleo hayana chama, lakini ukifuatilia matendo yake ni tofauti kabisa. Siku ile Lowassa alivyooenda kumtembelea akawa anamwambia Lowassa wewe hukunitukana kwenye kampeni bali wapambe wako na Lowassa akaonyesha kukubali, hali ile ilinikwazwa ile mbaya, kwani najua kabisa hata mkulu alikuwa anapiga pushup kama kejeli kwa huyo Lowassa. Hawa ccm wanajiita ccm mpya mdomoni lakini matendo yao na siasa zao ni za kipuuzi kabisa. Kwanza nilishangaa ccm walipokuwa wanasema watafanya siasa za kistaarabu, nijuavyo ccm wanajua kabisa hawana nyota na kwa sasa hawakubaliki, hivyo mbinu yao kubwa ni siasa za kishenzi kama zinavyoonekana sasa.
Kwa sasa ccm hawana la kuuza jukwaani zaidi ya siasa za majitaka, na pindi watakapoona cdm wanapata watu ni lazima wataanza tena vitendo vya kikatili. Nakuhakikishia kwa siasa hizi haipiti wiki utasikia tayari unyama unaanza. Nawasihi cdm kila kamanda awe na simu ya smartphone ili kurekodi kitendo chochote cha kiharamia kitakachofanyika huku matukio yoyote yakiripotiwa vituo vya polisi ili kuweka kumbukumbu sawa.