Salum Mwalim hakujipigia kura. Je, angeshindaje na alienda kufanya nini kwenye vituo vya kupigia kura?

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Nimetafuta picha ya Salum Mwalim akiwa anapiga kura katika jimbo la Kinondoni sijaiona. Hii inamaanisha hakupiga kura na wakati wanakinondoni wanapiga kura yeye alikuwa anazunguka kwenye vituo.

Jiulize ni kwanini alikutwa kwenye kituo cha kupiga kura wakati yeye sio mpiga kura au wakala au msimamizi katika uchaguzi?
 
Chadema hawataki tuyajadili haya ili wajifiche kwenye chaka vurugu za maandamano
Hatari kubwa kila mmoja ana uchungu na mwanafunzi aliefariki lakini wao wanataka kutuaminisha kama yule mtoto alikuwepo kwenye maandamano haramu na kusahau kama wao pia ni washitakiwa!
 
Id yako inaonyesha wewe ni jinga lao kawaulize wajinga wenzako
 
ninayo ya yule mwandishi.aliyehoji kura zilizoongezwa zimetokea wapi.
Alijibiwaje?
Tuongelee ndugu yetu mpendwa ambaye hakuwa hata na kituo cha kupigia kura alienda kufanyaje kwenye kituo hadi atake kukamatwa na polisi?
 
Mada ya kujadili uchaguzi imepotea
Mada iliopo kwasasa ni kifo cha aquilina.
Na hivi ndio huwa wanataftaga sababu hapo ndio wameipata sasa
M/kiti wao anafahamu kabisa kuwa maandamano yasio na vibali toka serikalini ni marufuku
Sasa kiherehere gani kilichomfanya akaandamane??
Je alishaona kuwa wamezidiwa ktk kura
Je alitaka kujionesha ana machungu saana
Je hakufahamu kuwa kuvunja sheria ya nchi kitu gani kitakacho msibu yeye na wenzie
Yaani kila nikijiuliza haya maswali sipati jibu,

Cha ajabu ukisema haya utaanza kutukanwa kuwa unaleta siasa ktk mwili wa marehem
Hilo jambo la mtu kuuwawa limetuuma saana na hadi sasa maumivu yapo
Lakini tujiulize chanzo hasa ni nini?
JE WASINGEANDANA YANGETOKEA HAYA???
Kama wasimamizi wa uchaguzi waligoma kuwapa fomu mawakala kwanini M/kiti wa CDM asichukue hatua mbadala,hadi aandamane??
Wakuu naombeni ufumbuzi hapo
 
Back
Top Bottom