Saloon za kike Kichaka cha umbea??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Saloon za kike Kichaka cha umbea???

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, May 14, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,605
  Likes Received: 5,780
  Trophy Points: 280
  Kuna kipindi inabidi uamini Mungu yupo hata kama mpagani
  maana ikifika wakati wa mwisho ayupo hutokuwa na hasara
  lakini weye ulieacha kuamini na ukamkuta kiama chake....&&&&

  Kwenu wanandugu fL1 na wengineo jamani..tupeni ufafanuzi kuna
  wanaume yaani wakisikia wake zao kwenda saloon wanahisi kichefu
  chefu..sasa tunaitaji ukweli halisi

  Wapo wanaaoamini saloon ni sehemu ya kufndishia umbea na hivyo
  wanandoa ama wenye wachumba wengi hubeba upashu na kuishia
  nao mwisho wa siku kuutumia kwa waume zao na kuharibu ndoa ama uhusiano
  wao

  wapo wanaoamini kama mkeo mpashu mpashu tu na wengine awaitaji
  kwenda saloon kuja kuanzisha zali..wao kama ipo ipo na kama apana apana

  sasa pengine wengine wamedanganywa sana kwa waume zao wako saloon
  huku wakiwa sehemu za starehe...nakumbuka nikiwa mwanza nilishukia guest moja
  mchana nasikia mwanmke saa nane anasema niko saloon mumewangu yaani ananipendesesha wacha mapaka utafurahi na jamaa anakuwa kama ana hamu kuona
  alivyopendezwa..ninamaana wengi wa wanawake wanaobanwa hutumia saloon
  kama sehemu za kwenda kufanya uharamia wao wa mapenzi.....

  Mwenye uzoefu mtusaidie
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,605
  Likes Received: 5,780
  Trophy Points: 280
  mwingine anachukulia uzoefu kwa wale wajuzi wa mahaba aliwakuta hapo na kuja kumtunza mume ama bfriend
  waanaume wa bongo wanjuliza vipi umepata wapi style hii kusema anashindwa..anyway sijui nasema sijui
  yawezekana wengine huonyeshana hata style wakiwa wanasubiri draya lipate moto

  hamuu hamuu hamuuuu
   
 3. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  huko ndo sehemu ya kila mtu kumwanika mmewe, mara ohoo hajiwezi, mara ohoo mrefu mno, mfupi sijui,mzito, sijui ukitaka kufanya....fanya namna hii, yaani ni kitcheni party ya kishetani huko....kila mtu anataka kuwaonyeshea wenzie kuwa amemkamata vizuri bwanake, anaweza kumridhisha bwanake, anajua sana mambo fulani ya ndoa yale, yeye ni mtaalam hivyo anawapa wenzie ushauri,....wanaowacheka wamama wenzao wasiovaa vitu vya garama ndo kibao, mara fulani hajui kuvaaa, mara fulani anatoka nje ya ndoa, mara fulani hana sura nzuri, mara hajui kuoga, mara sijui maskini kuliko mimi, mara sijui bwanangu ananipa pesa nipendavyo...kila mtu anaongea apendavyo....ndo maana utakuta midomo yao imenyoookaaa hadi imekuwa mirefu hasa wakipakaa wanja mwekundu..kwasababu ya uongo, umbea na unafiki. mtu aliyefanya saloon kama ni mkeo ni wa kuwa naye makini sana, kwasababu amesikia ushauri wa kila aina..na anaweza kuamua kuupractice
   
 4. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,955
  Likes Received: 21,117
  Trophy Points: 280
  na mama zenu nao mnawaweka kwenye hili kundi??maana nao ni wanawake.
  nb:no offence intended
   
 5. k

  kaiya Member

  #5
  May 16, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0  Umejuaje? au unafanya kazi salon?
  BTW. Mbona salon nyingi siku hizi hairdressers ni wanaume kwa hiyo na wao wamo kwenye kundi hili.
   
 6. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Pdidy draya likiwashwa tu unaingiza kichwa, la kusubiria kupata moto linaitwa steamer!
   
 7. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #7
  May 16, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  umeanza na mfumo dume wako....hata vijiweni nako ni vichaka vya umbea.
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wlikufanya nini hawa watu.....maana unaonekana una hasira nao kweli!:angry:
   
 9. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Hii itakuwa saluni ya wapi? mmh! hii kali!!
   
 10. S

  Silvershadow Member

  #10
  May 16, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe Pdidy kama mkeo ana hulka ya umbeya usijumlishe wanawake wote wanaoenda salon.
   
 11. s

  sijafulia Member

  #11
  May 16, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aaaaah.....pole kama nimekchoma kula hiyo kidogo

  WIMBO WA CHAJA YA KOBE......Uburudike na weekend
   
 12. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #12
  May 16, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ....utakuwa mmojawao na wewe...otherwise umetuacha tunajiuliza umeyajuaje yote haya?
   
 13. S

  Silvershadow Member

  #13
  May 16, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumbe "sijafulia" na "pididy" ni mtu mmoja? Sasa yanini basi ujibu kwa jina tofauti na uliloanzishia thread?
  Kuwa shujaa upambane na ukweli badala ya kujificha kwenye majina elfu - kwani unamwogopa nani hapa au mkweo huwa anaingia humu ..hutaki akuone ulivyo?

  Inaelekea unapenda mipasho kama makurumbembe hao hao unaowasema.... Nakutafutia wimbo wa " sanamu la michelini" wa marehemu nasma kidogo ukuburudishe wewe ..
   
 14. C

  Chipyopyo Member

  #14
  May 17, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba niwe shuhuda,
  Mke wangu alikutana na kuwadi saloon hadi leo sitaki kusikia habari za saloon. Ilikuwa hivi:

  Mke wangu kila alipokuwa anataka kupendeza alienda saloon flan kujirekebisha kumbe kuna jamaa linamfukuzia likaanza kufua tilia nyendo zake na kugundua saloon anayotumia then likamtumia kuwadi (wa kike) kule saloon. Wakawa wanayaongea huku nma wapambe wakishindilia misumari.

  At the end mke wangu kauvaa mkenge na pia kisingizio kikawa ni saloon.

  Nilikujabaini hayo baada ya wamama wenye busara kujua kuwa saloon inamuharibu mke wangu wakanitonya ili kuokoa ndoa yangu ingawa walikuwa wameshachelewa.

  Mbaya zaidi, walinichafua sana na busara finyu za wife ndizo zilizomponza leo hii hana pa kujishika

  Hayo ndiyo mambo ya saloon na hiyo ni TRUE STORY
   
Loading...