Salome Makamba: Ajali zinatokana na trafiki kukifanya kitengo cha usalama barabarani kuwa chanzo cha mapato

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,655
2,000
Ajali za barabarani nchini Tanzania hasa kwa madereva wa pikipiki (bodaboda), zinasababishwa na adhabu kutoka kwa askari wa usalama barabarani (Trafiki).

Kauli hiyo imetolewa na Salome Makamba, Mbunge Viti Maalumu leo Jumatatu tarehe 8 Februari 2021, bungeni jijini Dodoma wakati akiuliza swali la nyongeza katika wizara ya mambo ya ndani.

Salome ni miongoni mwa wabunge 19 waliofukuzwa uanachama wa Chadema na Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, kukiri kufukuzwa kwa kukata rufaa Baraza Kuu (BKT), na kuendele kuhudumu kwa wabunge kutokana na kukingiwa kifua na Spika wa Bunge, Job Ndugai

Akizungumza bungeni hapo, Salome amedai tatizo hilo linatokana na trafiki kukifanya kitengo cha usalama barabarani chanzo cha mapato.

Amedai, baadhi ya bodaboda hulazimika kuwakimbia ili kukwepa kutoa faini, hatimaye wengi wao kuangukia katika ajali.

“Tatizo la msingi la ajali za baraarani kwa bodaboda na vyombo vingine vya usafiri, linatokana na kitengo cha usalama barabarani kuwa kama chanzo cha mapato.”

“Watu wanakwepa ma-trafiki, wanakimbia sababu ukikamatwa, hakuna onyo ni faini,” amedai Salome

Amesema, tatizo la kukithiri kwa adhabu za makosa ya barabarani ni dosari zilizopo katika baadhi ya vifungu vya Sheria ya Usalama barabarani ya mwaka 1973.

“Bodaboda siku hizi wanakamatwa kwa kukimbiana na matrafiki, nadhani hii inasababishwa na uzee wa sheria ya mwaka 1973,” amesema Salome.

Akiuliza swali lake la nyongeza, Makamba amehoji lini serikali italeta muswada wa kufanya marekebisho ya sheria hiyo ili kupunguza ajali za barabarani.

“Serikali ni lini italeta mabadiliko ya sheria ya usalama barabarani ili tufungue mjadala wa kuboresha kupunguza ajali za baabarani?” amehoji Salome

Akijibu swali hilo, Khamis Hamza Chilo ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani amesema, muswada wa mabadiliko ya sheria hiyo uko njiani.

“Nimtoe hofu, muswada huu uko njiani, muda wowote tutaleta tuone namna tutafanya mabadiliko ya sheria hii,” amejibu Chilo.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
14,522
2,000
... nakubaliana naye. Kuna makosa ya wazi kabisa na ya makusudi ambayo adhabu/faini haina mjadala. Lakini kuna makosa mengine kwa kweli onyo linatosha. Mfano, porini huko kibao cha 50 kimejificha hakionekani au ghafla umekiona na ukapunguza speed, kwanini isiwe onyo?

Adhabu inaweza kuwa hivi, kwa makosa ya onyo, dereva aonywe na rekodi ziingizwe kwenye system. Akirudia kosa mara ya pili kwa siku ile ile moja, alipie makosa yote mawili maana huyu ni mkaidi.

Halafu hivi vibao vya 50 sometimes vinapotosha; uanweza kukutana na kibao cha 50 lakini kinapoishia sometimes hapaonekani. Wahusika (TANROADS) watimize wajibu wao, kama eneo halitakiwi kuzidisha 50, basi vibao vya 50 viwekwe umbali usiozidi mita 100 toka kibao hadi kibao. Sio kibao cha kuondoa katazo kinaenda kuwekwa km 5 mbele kama sio kutafutiana sababu ni nini?

Hadi sometimes, dereva anakuwa amesahau yuko ndani au nje ya 50; trafiki wanapenda haya maeneo balaa! Kama nia ni njema, msiwatege madereva, waelezeni kwa uwazi kabisa kwa kuweka vibao karibu karibu.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
40,821
2,000
Halafu Kuna watu wanasema bunge linatunga sheria, huku mbunge analialia kuwa ni lini serikali itapeleka mswaada wa sheria ya barabarani ujadiliwe. Nilitarajia nione mbunge ndio anaanzisha mjadala wa jambo kuwa sheria, na sio hiyo ya rubber stamp ya miswaada ya serikali.
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
7,945
2,000
Huyo mbunge yupo sahihi sana, trafiki wanakusanya mapato hawapo pale kuonya, kulinda au kusimamia sheria.

Mfano zile notification form nyuma zina maelekezo kwa mfanya kosa kutakiwa kuonywa kwa kifungu fulani cha sheria au kutakiwa kulipa faini ndani ya siku saba ila hao trafiki wao wanakulazimisha ulipe on the spot, vinginevyo leseni na funguo ya gari halali yao.
 

Stimboti

Member
Oct 16, 2018
39
125
Acha Boda Boda wakamatwe tu ,hujakutana na adha ya Boda wengi wao hawana leseni na wanaendesha rafu sitasahau Boda aligonga gari yangu kwny mataa hawataki kusimama kwny Trafick light ,hawaheshimu sheria .
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
32,030
2,000
Mheshimiwa Salome yuko sahihi kabisa!
54321076.jpg
 

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
570
1,000
Ni hatari wengine wameenda mbali zaidi kwa kutozwa fedha za ushirikino (madereva wa probox ktk barabara ya Kakonko "Kigoma" - Nyakanazi "Biharamulo" ukiongea nao mengi utayapata).

Need intervention
 

Pep

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,230
2,000
Salome wangu anasahau kwamba trafiki wanahitaji pesa ndogo ndogo za ku brashia viatu
 

Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
10,014
2,000
Hakuna watu wapuuzi barabarani kama bodaboda, huyu mh hawajui huyu, kwanza hawanaga leseni, mafunzo, bima, na hawajui hata alama na sheria za barabarani, anaweza akasababisha ajali na akafa yeye wenzake kama una gari ndio kajigongesha wanaweza kukutoa roho kama polisi wakichelewa kukupa msaada. Hawana maana, sasa kama wanasimamishwa kwa nini hawasimami?
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
4,430
2,000
Mbunge wa viti maalumu kupitia chama gani?

Vipi ile kesi ya kumchona nyumba ya Katambi?
 

Nyanidume

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
2,359
2,000
Comments zote nilizozisoma zinatushambulia sisi tu, mh. Salome kaliona hili ni tatizo kaamua kutusemea lakini nyinyi kwa roho mbaya zenu mmeamua kututoa akili! Mnajifanya hamjui jinsi gani mnavyotutendea mkiwa barabarani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom