Salma Kikwete: Sikubaliani na suala la mtoto aliyepata ujauzito kurudi shule

Sheria zetu zinamtambua mtoto ni yule ambaye hajafikisha umri wa miaka 18,
Sheria inasema kuzini na binti chini ya miaka 18 ni tendo la kubaka.
Cha kushangaza tunaendelea kumbana binti aliyebakwa asiendelee na masomo ingawa aliyempa mimba atafungwa miaka 30 kwa kosa la kubaka!!
 
Maelezo ya kwa Nini warudi shule na au wasirudi, bado hakuna mwenye logic!

Kurudi shule Ni kuhamasisha mapenzi shuleni

Kutorudi shule, Ni kuwanyima haki yao ya msingi,

Lipi Bora!
Kuhamasisha ukimwi na kubakwa wanafunzi
 
Ila tuwe waangalifu, wengi si mimba za bahati mbaya, bali utukutu, yaani wengine wataongeza wakiwa huko shuleni, kwani hao uwezi kuwazuia tena kutofanya ngono, na wengi upenda starehe zaidi ya masomo, sita shangaa f4 watoto 3!
Je viwango vya elimu vitakuwaje. Je nidhamu mashuleni itakuawaje
 
Katika uamuzi mzuri wa serikali ni kuruhusu wajawazito warudi shule,huu ni uamuzi mzuri sana.

Kwa sababu kama mjamzito hastahiki kusoma basi na huyo mtoto wa tumboni naye asisome kwa sababu ndio amemfanya mama yake asisome.

Arudi shule asome,mimba sio kikwazo

Serikali inastahiku kupongezwa katika jambo hili,na sio lazima warudi wakitaka warudi wakitaka wabaki nyumbani kulea watoto,muhimu serikali imeweka mlango wazi kwa atakae na huu ndio ustaarabu.
Mnapoteza muda tu hakuna atakayerudi shule. Ni wachache kutoka familia za walioelimika. Idadi kubwa hawatarudi shule hasa vijijini. Hili suala ni kuliacha tu lilivyo ingawa tunashukuru wameruhusiwa.
 
Ila tuwe waangalifu, wengi si mimba za bahati mbaya, bali utukutu, yaani wengine wataongeza wakiwa huko shuleni, kwani hao uwezi kuwazuia tena kutofanya ngono, na wengi upenda starehe zaidi ya masomo, sita shangaa f4 watoto 3!
Je viwango vya elimu vitakuwaje. Je nidhamu mashuleni itakuawaje
Mimi kitu ambacho mpaka leo hakijaniingiaga akilini ni suala la mama kuendelea na shule wakati baba amefungwa gerezani miaka 30! Yaani mama amlee mtoto peke yake miaka yote ya maisha yake, na mtoto akose malezi ya baba. . Wajinga wanashangilia kuwa wamemkomoa mwanaume kumbe ni mateso kwa huyo mzazi wa kike na maisha yaliyojaa msongo kwa mtoto.

Na sijui mtoto anakua anaambiwa baba yako yuko wapi? Na kama ni gerezani alifungwa kwa kosa gani? Kama kosa la baba yake lililomfanya akafungwa miaka 30 ni kumzaa yeye, sijui huyo mtoto kama atajiona ana thamani!!! Yaani baba kunizaa mimi ilikuwa makosa?? Kwa hiyo sikutakiwa kuzaliwa??? Inafikirisha sana.

Na kama lengo ni kuzuia mimba kwa nini isiwekwe sheria hata ya mtoto wa kike kufungwa au kupewa adhabu yoyote? Baba afungwe miaka 30 lakini mtoto wa kike waweke hata miaka mi3 tu inatosha. Uje uone kama mtoto wa kike mwanafunzi atakubali kukuvulia kizembe. Hawa watoto wa sasa ni watu wazima kabisa kiakili na kimatendo. Hakuna anaebakwa, asilimia kubwa wapo kwenye mahusiano kama watu wazima tu. Na nani ana justify kuwa wa kiume ndo chanzo all the time? Kuna mazingira mengi ambayo wa kike anakuwa chanzo. Hawa wa siku hizi hadi kutongoza mwanaume kwenye simu wanatongoza. Kumuadhibu wa kiume tu ni kuonea jinsia ya kiume na sijajua lengo hasa huwa ni nini.

Wanafunzi wa kike hata hiki kidogo walichokuwa wanajilinda ni kwa kuogopa kuwa akipewa mimba ataachishwa shule na kukatiza ndoto zake. Hii ilikuwa adhabu inayomuogopesha. Sasa hivi unaiondoa alafu unategemea kuzuia mimba mashuleni au unapanga kufungua clinic shuleni? Maana itafika hatua itakuwa ni fashion kwa wanafunzi, kiasi kwamba itaonekana ndio ujanja na ambae hajazaa ni mshamba na wanamcheka.

Tujifunze kufikiria kwa kina kuokoa kizazi chetu. Tusipokee kila kitu tunacholetewa, na sisi tuna akili zetu, tuzitumie. Na namna nzuri ya kumuinua mtoto wa kike ni kumpandisha amfikie wa kiume, na wala sio kumshusha wa kiume alingane na wa kike.

Nawasilisha.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Hoja ya msingi kama mama mwanafunzi anaruhusiwa kurudi masomoni baada ya kujifungua na sheria ifanyiwe marekebisho baba yake asishtakiwe ili awe huru kulea mtoto na pili logic haipo tena iwapo kwenye jamii mtizamo kuhuhsu mimba za utotoni zimebadilika unamshitaki vipi mpiga mimba.
 
haya mambo banah, indonesia walikua wanawapima bikra mabinti kabla hawajaanza sekondari, saudi arabia walikua wanakataza wanawake kuendesha magari, huku sisi binti akizaa hatakiwi kurudi shule unajua vizazi vijavyo vikija kuhadithiwa hizi sheria watastaajabu sana,
Na sheria inayozuia ndoa na mapenzi ya jinsia moja iko mbioni kufumuliwa kwa mwendo huu
 
Mimi kitu ambacho mpaka leo hakijaniingiaga akilini ni suala la mama kuendelea na shule wakati baba amefungwa gerezani miaka 30! Yaani mama amlee mtoto peke yake miaka yote ya maisha yake, na mtoto akose malezi ya baba. . Wajinga wanashangilia kuwa wamemkomoa mwanaume kumbe ni mateso kwa huyo mzazi wa kike na maisha yaliyojaa msongo kwa mtoto.

Na sijui mtoto anakua anaambiwa baba yako yuko wapi? Na kama ni gerezani alifungwa kwa kosa gani? Kama kosa la baba yake lililomfanya akafungwa miaka 30 ni kumzaa yeye, sijui huyo mtoto kama atajiona ana thamani!!! Yaani baba kunizaa mimi ilikuwa makosa?? Kwa hiyo sikutakiwa kuzaliwa??? Inafikirisha sana.

Na kama lengo ni kuzuia mimba kwa nini isiwekwe sheria hata ya mtoto wa kike kufungwa au kupewa adhabu yoyote? Baba afungwe miaka 30 lakini mtoto wa kike waweke hata miaka mi3 tu inatosha. Uje uone kama mtoto wa kike mwanafunzi atakubali kukuvulia kizembe. Hawa watoto wa sasa ni watu wazima kabisa kiakili na kimatendo. Hakuna anaebakwa, asilimia kubwa wapo kwenye mahusiano kama watu wazima tu. Na nani ana justify kuwa wa kiume ndo chanzo all the time? Kuna mazingira mengi ambayo wa kike anakuwa chanzo. Hawa wa siku hizi hadi kutongoza mwanaume kwenye simu wanatongoza. Kumuadhibu wa kiume tu ni kuonea jinsia ya kiume na sijajua lengo hasa huwa ni nini.

Wanafunzi wa kike hata hiki kidogo walichokuwa wanajilinda ni kwa kuogopa kuwa akipewa mimba ataachishwa shule na kukatiza ndoto zake. Hii ilikuwa adhabu inayomuogopesha. Sasa hivi unaiondoa alafu unategemea kuzuia mimba mashuleni au unapanga kufungua clinic shuleni? Maana itafika hatua itakuwa ni fashion kwa wanafunzi, kiasi kwamba itaonekana ndio ujanja na ambae hajazaa ni mshamba na wanamcheka.

Tujifunze kufikiria kwa kina kuokoa kizazi chetu. Tusipokee kila kitu tunacholetewa, na sisi tuna akili zetu, tuzitumie. Na namna nzuri ya kumuinua mtoto wa kike ni kumpandisha amfikie wa kiume, na wala sio kumshusha wa kiume alingane na wa kike.

Nawasilisha.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Uki sahihi kabisa. Maamuzi mengine yanashangaza sana
 
Mkuu Kama sikosei mwaka 2017 mkoa wa Lindi uliongoza kwa utumiaji wa njia za uzazi wa mpango,hivyo kwa kifupi tu wakazi wa mkoa wa Lindi ikiwemo na mkoa wa mtwara wanatumia Sana njia za kisasa katika kuzuia mimba .

Kuna shule moja niliwahi fundisha huko mtwara kwa miaka mitano,huwezi amini ndani ya miaka yote hiyo ni mimba nne tu ndo zilizolipotiwa kwa shule hiyo.

Baada ya kuhama mazingira na kuja Mwanza ,Kuna shule nilipangiwa ,nilibahatika kuwa mwalimu wa darasa kwa kidato Cha Cha kwanza ,ambao walikuwa mikondo mitatu,Mimi nilipewa mkondo mmoja ,ndani ya nusu mhula kulikuwa na lipoti sita za watoto kupewa mimba katika mkondo wangu,nilipofanya analysis kwa shule nzima kwa mwaka huo kulikuwa na mimba zaidi ya 15 ,na hapo hakuna hata mimba moja iliyopata mhusika,au hata wahusika wa mimba kutiwa nguvuni,

Nilichogundua Ni kuwa watu wa Kanda ya ziwa hasa Hawa jamii ya wasukuma Wana taarifa hasi Sana juu ya njia za uzazi wa mpango,hivyo bado nasisitiza kuwa serikali licha kusisitiza watoto waliojifungua kurudi mashuleni bado wanayo nafasi pia ya kutoa elimu ya uzazi wa mpango huku ikisisitiza watoto kutumia njia za uzazi wa mpango.Hii itasaidia Sana kuwaokoa vijana wetu kupata watoto wasiotarajiwa.

Huku usukumani watu bado wako gizani Sana juu ya elimu ya uzazi wa mpango,hapa nilipo nina jirani yangu ambaye maisha yake Ni duni Sana,Cha kushangaza ana watoto wengi kuniliko Mimi mwenye unafuu wa maisha,kula shida ,kulala shida ,inafikia kipindi unatamani kumuuliza huu uzaaji wake Ni kwa faida ya Nani,but unakaa kimya tu!!!!

Elimu kwa watoto wetu ni muhimu Sana.
Unafanya utafiti kati ya Lindi na Mwanza ? Je, ulizingatia idadi ya watu ? Au umepuyanga tu ? Rudi kafanye utafiti unatuchosha tu.
 
kwa hyo mtoto akipata mimba adhabu yake AFUKUZWE SHULE?
Kuna mahusiano gani kushika mimba na kufukuzwa SHULE?
kwanini asiseme mtoto akipata mimba apewe aldhabu alafu aendelee na SHULE.ili iwe funzo kwa wengine
 
Duh..Kaamua Kumlipua Mama.
Ila Mama anapokaza Misuli Kutetea Mimba Mashuleni ...ni Kama ule Ushungi Unamsuta...!
Suala sio mimba za mashuleni.
BALI HAKI YA MTOTO WA KIKE KUPATA ELIMU.
Msichanganye vitu.
Kipi Bora mtoto wa kike apate mimba akiwa form 2 aachichwe SHULE.
Au apate mimba azae afike mpaka form 4 na inawezekana akafaulu na kuendelea juu.
Unapomfukuza SHULE unataka akafanye nini mtaani?
 
Mimi nashauri adhabu ya kumpa mwanafunzi IKAZIWE vya kutosha.
Yaani ukimpa mwanafunzi mimba unakamwatwa unaenda mahakamani ,JELA.
hapo wanaume tutawaogopa wanafunzi.
Ila kuwazuiq kurudi SHULE .ni UKATILI.
 
Mnapoteza muda tu hakuna atakayerudi shule. Ni wachache kutoka familia za walioelimika. Idadi kubwa hawatarudi shule hasa vijijini. Hili suala ni kuliacha tu lilivyo ingawa tunashukuru wameruhusiwa.
Ndo manq nikasema serikali imeruhusu kwa maana ukisikia ruhusa maana yakw sio lazim na kama sio lazima hakuna jambo la kupoteza muda atakae atarudi asiyetaka atabaki nyumbani.
 
Na sheria inayozuia ndoa na mapenzi ya jinsia moja iko mbioni kufumuliwa kwa mwendo huu
issue ya ndoa za jinsia moja ni tofauti kabisa na haki ya mtoto wa kike kupata elimu, utawekaje sheria ya kuzuia kundi flani kutopata elimu? kwanza sheria inawatambua kuwa ni wahanga wa ubakaji ila mnawapunish kwa kuwakataza kupata elimu loh!
 
Akisema hivyo anamaanisha anaporwa wateja wake wa ile taasis ya Mama Salma Foundation? Au alikuwa anataka kuanziasha taasisi nyingine ya kulea hao watoto Sasa ameona wakirudi shuleni atakosa wateja?
Inamaana umeshaamua kuwa hakuna atakalosema/fanya lenye nia njema zaidi ya tamaa ya kujinufaisha.......
 
Suala sio mimba za mashuleni.
BALI HAKI YA MTOTO WA KIKE KUPATA ELIMU.
Msichanganye vitu.
Kipi Bora mtoto wa kike apate mimba akiwa form 2 aachichwe SHULE.
Au apate mimba azae afike mpaka form 4 na inawezekana akafaulu na kuendelea juu.
Unapomfukuza SHULE unataka akafanye nini mtaani?
yeah,
 
"Mimi sikubaliani na suala la mtoto aliyepata ujauzito kurudi shule hata kidogo, hii ni kwa sababu ya Mila, desturi, utamaduni na mazingira pamoja na dini, hakuna dini yoyote inaruhusu mtoto wa kike kupata mimba kabla ya wakati"

Mhe.Salma Kikwete, mbunge wa Mchinga

Akisema hivyo anamaanisha anaporwa wateja wake wa ile taasis ya Mama Salma Foundation? Au alikuwa anataka kuanziasha taasisi nyingine ya kulea hao watoto Sasa ameona wakirudi shuleni atakosa wateja?
Tatizo tunashindwa kuelewa Kwamba wengi hupata Mimba sio KWa makusudi bali na maisha Magum huchangia, hivyo Mimba nyingi huwa ni KWa bahati mbaya,

Lakini wapo waliopata Mimba hakukata tamaa bali waliendelea na kitabu na KWa Sasa Wana elim ya kutosha,na nafasi nzuri za kazi

Sasa Kama tunasema ni dhambi,au mila zetu haziruhusu je vipi wanaopata na kuchomoa Mimba ?

Binafsi nafikiri waludi ila pawepo na vigezo vya mtoto kurudi, ambavyo tunaweza kukubaliana,

Mfano Kama alibakwa, leo unazuia vipi asirudi shule,
 
Back
Top Bottom