Salma Kikwete, Ridhwan Kikwete ni kina nani Katika Serikali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salma Kikwete, Ridhwan Kikwete ni kina nani Katika Serikali?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by OgwaluMapesa, Sep 15, 2010.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hivi mama salma kikwete , mke wa Rais Jakaya Kikwete ,Rihwan Kikwete Mtoto wa Rais Jakaya Kikwete ni sehemu ya uongozi wa taifa letu? kama jibu ni ndiyo ni ibara gani ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inayofafanua nafasi zao na wajibu wao kwa watanzania kwa kuwa Mke na mtoto wa Rais.
  Kama jibu ni hapana ,ubavu wa mwana na mama kuzunguka na kutamba mikoani katika mikutano ya hadhara na hafla mbalimbali anazozifanya akikipiga kampeni za wazi wazi za kumfagilia mumewe na chama chake cha Cha majambazi (CCM) Kwa kutumia rasilimali za umma anautoa wapi.?
  Nauliza maswali haya kwa sababu mwenye macho anaona na mwenye masikio anasikia kwa mama salma na Ridhwan Kikwete katika kampeni zao na hafla mbalimbali wanazoandaliwa zinagharamiwa fedha za walipa kodi wa Nchi hii.
  Ingawa uongozi wa serikali na chama tawala umeweka pamba masikionni ,ukweli wa mambo ni kwama salma na Ridhwan wamekuwa gumzo kwa mambo wanayoyafanya hasa wanapokuwa mikoani kwa kutmia nyenzo za serikali na kupata heshima zote anazopewa Rais kana kwamba wao ni sehemu ya taasisi ya Urais.
  Wanafanya vyombo na taasisi za serikali mikoani na wilayani kuwa na wakati mgumu kiasi cha cha kulazimika kumsomea ripoti za maendeleo ya mkoa ,polisi kuhangaika huku na kule kuhakikisha usalama wa mama salma na Rihwan na katika kufanya hivyo ,wananchi wa eneo husila kukwamishwa kwa muda shughuli zao kwa vile Rais asiyetambuliwa na katiba, anapitishwa.
  Siyo siri kwamba hadhi ya Urais anayopatiwa mama salma na Ridhwan haikuonekana kwa Mama maria Nyerere na Makongoro Nyerere.Ridhwan na Mama Salma wana nini cha ziada na kama anacho kwa nini haianishwi kwenye katiba ili watanzania tumjue tusimshangae na anachokifanya ?
   
 2. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Tanzania ni nchi ya kipekee sana hapa duniani kwani ni nchi inayoendeshwa kwa msingi wa mawazo ya mtu aliye madarakani na si katiba ya nchi. Nafikiri inabidi turudishe ule msemo wa zidumu fikra za mwenye-ziki wa chama ili tukae tukisikiliza ya kwake na kuiacha katiba.

  Kuna haja gani ya rais kuapishwa kuilinda katiba huku akijua ataibomoa kwa mikono yake?
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Development takes its cause
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Familia ya kikwete = CCM = Tanzania
   
 5. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  tanzania ni nchi ya kifalme....sasa wew uantegemea nini?
  nadhani umeelewa mkuu
   
 6. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  nimeongea na baadhi ya wazee wakubwa tu ndani ya serikali na pia ndani ya vyombo vya maamuzi katika CC na NEC ya CCM, hawaridhiki na hali ya mambo ndani ya chama hasa kwa jinsi familia ya JK inavyoingilia uendeshaji wa mambo nyeti ya chama na wengi walichukizwa na hatua ya hapa juzi kwa JK kumruhusu mwalimu Salma kuingia ndani ya CC wakati hana mamlaka hayo.
  kwa kudhihirisha chuki zao angalia mzee msekwa pamoja na msiba wa mwanae uliotokea juzi, alikwisha anza kukacha vikao vya CCM kabla na hata kuwa na mwelekeo tofauti hasa kwa kuona uozo huo wa JK na mbakaji Makamba, wazee wengine kama mkapa pia wameshtuka na wanaona huyu mkwere sasa amevuka mipaka.
  kwa kuda huu natafuta maoni toka pale TIS ili kuona msimamo wao kwa jinsi Taifa linapoelekea na nitatoa taarifa rasmi hapa na hatua ambazo TIS wanapanga kuchukua hivi karibuni.
   
 7. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2010
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hivi wamejaza form ya gharama za uchaguzi?
   
 8. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2010
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ridhiwani Kikwete avunja makundi Lindi
  [​IMG]Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa,Ridhiwani Kikwete akivishwa kitenge alipowasili katika Kata ya Nandagala, Ruangwa ikiwa ni ishara ya Mgombea urais kupitia chama hicho, Jakaya Kikwete kuwa atashinda kwa kishindo katika uchaguzi Mkuu.
  [​IMG]Ridhiwani akiwasalimia wananchi wa Kata ya Nandagala, Ruangwa, mkoani Lindi jana.

  [​IMG]Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa,Ridhiwani Kikwete akilakiwa na Mgombea ubunge Jimbo la Ruangwa kupitia CCM,Khamis Majariwa baada ya kuwasili jana katika Kata ya Nandagala, tayari kuanza ziara ya kuhamasisha vijana na wafuasi wa chama hicho kuweka mikakati ya ushindi mkubwa kwa cham

   
 9. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kazi ipo jamani, hata kwa Mkapa haikuwa hivi
   
 10. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ghaaaaaaa uchafu mtupu, hivi huyu JK anafanya nchi hii ni mali yake sio? Hebu nipeni nchi niwe rais kwa masaa mawili tu muone nitachowafanya JK, SALMA NA RIDHIWANI, hasa huyu dogo huyu mi ninammind kinoma, nikipata urais huyu lazima anyee ndoo miaka kibao akisaiidiana na dingi wake.Jama nchi hii iuzwe tu tugawane na kila mtu aishi atakako.:mad2:
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mkuu una busara!

  Nilifundishwa na daktari mmoja ambaye alinambia kuwa kawaida Historia ya uKombozi ni historia ya MAPAMBANO!....mapambano dhidi ya dhulma za daraja la watu wachache, wanaojiona kuwa ni mabwana!
  Tukiamua kupambana na daraja hilo la watu, na tukashinda basi tutasonga mbele, japo kwa hatua fulani...ndiyo maendeleo!.
  Hakuna maendeleo yasiyogharimu sadaka na watu kuumia katika mapambano!

  Watu kama akina JK, sALMA NA rIDHIWANI wapo ili historia ya nchi hii iandikwe na kuthibitika, watu wapambane na kundi hilo dogo, na hatimaye kizazi hiki kisonge mbele, ndiyo maendeleo!
  Tazama Kenya..ni mfano halisi wa hatua hizi...na bila mapambano ya aina ile hatuvuki ng'ambo ya pili!

  U can take my words to the Bank!
   
 12. K

  Kishazi JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Kwa kweli huu uongozi wa JK mimi sitaki hata kuusikia. Kero tupu, huyu Ridhiwani ana akili gani ya kuburuza wazee wa CCM kama siyo baba yake kaamua kukifanya chama kama chama cha familia. Mimi nawashangaa sana watu wanaomshabikia bila kujua kuwa mnakazana kuuingiza ukoloni mamboleo wa JK na wapambe wachache na mafisadi katika serikali. Kama miaka mitano ya kwanza mliona alivyowatoa kafara washikaji wake ambao aliwaona kama threat kwake kwa kigezo kuwa anakomesha ufisadi hali ni mabifu yao na kutumia matendo yake haya kama kampeni kwa sasa, tutegemee nini wananchi endapo atapewa miaka mitano mingine kama sio kukomeshana endapo utatoa comment tu, unauziwa kesi ya EPA. Tutarajie nchi yetu kuwa ya wachache tu ambao ni wapambe au wana mtandao hai tena wanaoaminika tu.

  Wana CCM amkeni mlipo, nyie mshangilieni kila anapopita, ila tarehe 31 mpeni surprise ya mwaka. Tendwa na Kiravu nawafahamu kuwa mna hekima na akili tatizo ni mfumo unabana IQ zenu, hebu mpeni moyo huyu jamaa ila kuanzia tarehe 31 usiku mkiona tu ukweli unaonyesha kuwa kapigwa chini uachieni na muuonyeshe wazi. Kwa hili Dr. Slaa atawaamini na kuwaacha kwenye viti vyenu.
   
 13. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2010
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  RIDHIWANI KIKWETE NAYE AANZA KAMPENI KILWA

  [​IMG]Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana Taifa, Ridhiwani Kikwete, akivishwa skafu na chipukizi Asha Khalifa alipowasili Kata ya Tingi, Jimbo la Uchaguzi la Kilwa Kusini,wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi kuanza ziara ya kuweka mikakati ya ushindi wa kimbunga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, mwaka huu. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA) ​
  [​IMG]Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana Taifa, Ridhiwani Kikwete, akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM, Kata ya Njinjo, Hemed Kipembekile alipowasili Kata ya Tingi, Jimbo la Uchaguzi la Kilwa Kusini,wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi kuanza ziara ya kuweka mikakati ya ushindi wa kimbunga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, mwaka huu. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA) ​
  [​IMG]Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapiduzi Tanzania Bara na Visiwani, Profesa wa Siasa Mtopa Ali Mtopa akitoa nasaha zake katika mkutano wa ndani wa viongozi wa UVCCM, Wilaya Kilwa, uliohutubiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la UVCCM Taifa, Ridhiwani Kikwete (katikati), mjini Kilwa Masoko,juzi. Ridhiwani na makada wengine wa UVCCM wameanza ziara ya kuhamasisisha vijana kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi mkubwa katika uchaguzi Mkubwa. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM,Mkoa wa Lindi Hassan Masala. ​
  [​IMG]Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana Taifa, Ridhiwani Kikwete, akihutubia katika mkutano Kata ya Tingi, Jimbo la Uchaguzi la Kilwa Kusini,wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi kuanza ziara ya kuweka mikakati ya ushindi wa kimbunga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, mwaka huu. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)​
   
 14. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  nawahurumia viongozi wa mikoani huko ambao sasa taka usitake lazima uwe kwenye mapokezi ya mke na mtoto wa rais maana ukionekana hutaki tu huna kazi.
   
 15. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nyerere angekuwa hai angesema "nchi inaongwanza na familia"
   
 16. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Viongozi wa CCM wanalifurahia hili jambo..wangeshaanza kuchukua hatua siamiini kwa umoja wao watashindwa vipi.!
  Ila kwakuwa kila mtu yuko kwa ajili ya tumbo...Nobody cares..!
  Ila "kama" akipita huo Urais ndo tutaiona sura halisi ya hii familia..
  Nashukuru Mungu sitakua mmoja wa aliyempitisha..
   
Loading...