Sallam SK: Tetema ya Rayvanny imeingiza Dola milioni 230

nina wasiwasi na hizi data, huwa kikawaida mtu wa marekani na mbongo wakisikiliza kitu malipo ni tofauti refer youtube na site nyengine zifananiazo. hata wewe leo ukienda show ya Msanii wa marekani unalipishwa kiingilio kikubwa kuliko show za kawaida kama Fiesta, hivyo wao wanakuwa wanalipwa zaidi sababu quality ya content zao ni kubwa.
Siyo kwamba wanangalia ni nchi gani watu wamestream sana?
 
Mleta uzi nafikiri hujasikiliza vizuri ile interview. Kasema tetema ina streams mill 23 spotify ambapo kwa streams mill 1 spotify wanalipa dollah kama elfu 5 kasoro, hapo aliposema ni dollar elfu 10 ndio kachanganya mambo.
Propagandist...kapotosha makusudi ndio zao kuleta taharuki😂
 
Katika mahojiano ya leo Meneja wa Diamond amedai Tetema ya Rayvanny imeingiza Dola bilioni 230 za Kimarekani, na kwamba Rayvanny ni tajiri na anaongoza.

Pesa hizo alizotaja Meneja SK ni nusu ya pesa za makenikia, ni pesa nyingi sana, sasa sijui ni kweli au kiki msikilize.

Naona huyu jamaa kaathirika na uuzaji madawa ya kulevya....nafikiri akili zake kaziacha Marekani pale alipokamatwa na madawa ya kulevya.
 
Mama yake huyu huyu inayedaiwa anakataa msaada kutoka kwa manaye 'eti' vyanzo vya kipato cha mwanaye haviendani na maandiko ya kwenye biblia.
Narudia, 'eti' mama yake ndiyo msimamo wake.
Madawa....Salim ni gwiji la uuzaji madawa ya kulevya na ndiyo maana Mama yake hataki hizo hela za kutesa watoto wa watu. Muulizeni Salim hivi kwanini alikamatwa Marekani na kapigwa ban kuingia kule. Sasa anatumia wanamuziki kusafirisha mizigo yake, Bongo fleva haina soko duniani ni hapa nyumbani tu.....mpuuzi huyu kijana anafikiri sisi ni mazezeta wa CCM?
 
Ni Kweli kabisa nimecheki pia Mase alipokua anahojiwa kuhusu umafia wa puff daddy, Mase anakwambia mikataba mingi ni magumashi na wasanii weng kwasababu ya uchanga wao na elimu ndogo wanasaini vitu ambavyo hawavijui mwa mfano Mase mkataba wake na Bad boys ambayo waliingia 1996 umekuja kuisha 2020 kumbuka 50cent alitaka kumsajili Gunit ukashindikana kabisa mwishowe Mase amekua mlokole, pia nliona clip ya busta rhymes anakwambia label nyingi zina fake maisha halis ya wasanii kwa mfano utavalishwa cheni fake,watakupa gar za kifahar,nguo kali,utapangiwa nyumba kali lakn bila msanii kujua kuwa anakuja kukatwa kwenye malipo yake ya show au streams.

Pia nliona kisa cha kundi mashuhuri la TLC kuvunjika aisee nilijua unyama uko Tz tu kumbe hata america label zimeua na kufilisi wengi,TLC walikua wakipewa nguo,viatu,cheni,miwani,magari etc hapo weka na tiketi za ndege,gharama za show,gharama za hotel wakienda tour au show,gharama za photoshot,gharama za airtime promoshen etc sasa TLC walikuja shituka kwenye album kwa mfano imeingiza bilion 4 wao wako 4 wanashangaa kwenye akaunti inawekwa 100mil wakiuliza wanaambiwa makato ya label kundi likafa....ndo mana hata hapa kwetu angalia fela alichowafanyia TMK

YAMOTO BAND ni wizi na dhruma,Yamoto walijengewa nyumba kwenye kiwanja kimoja na nyumba zimeungana kama train ndo madogo wakahoj mbona wakina chege wamejengewa separate sie kiwanja kimoja tukae wote? Kundi likafa, angalia harmonize kawalipa wasafi kiasi gan cha pesa kujitoa? Rich mavoko mpaka leo akaunti yake ya youtube anaishikilia sallam.
Mungu akubariki kwa "kuwaamsha" wasanii wa bongo ili wanufaike na jasho lao.
Umeandika ukweli 94%. Kongole sana.
 
Huyu jamaa anajua dola milion 230 kweli? Album ya thriller ya Michael Jackson in two years after being released ndio iliingiza 134 million dollars sasa huyu paka wa bongo ndio alete 230 labda ya mabox.

Waache kujitamba uongo haiwasaidii kitu maana huyo dogo kaanza kusema na ule mgahawa ni wake kwani akisema ukweli shida ipo wapi? Ndio maana wakija kupata matatizo watu wanaanza kuwabeza na kutisaodia sababu wanaona kama alichezea hela kumbe hata hakuwa nazo.
 
Back
Top Bottom