Salim aonya: Katiba, Muungano ujadiliwe na wananchi kwa uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salim aonya: Katiba, Muungano ujadiliwe na wananchi kwa uhuru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 8, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Waziri mkuu wa zamani Dk. Salim Ahmed Salim

  Dk. Salim: Chonde, chonde na Katiba


  Watanzania wa pande zote mbili za Muungano wana nafasi kubwa ya kutoa maoni yao kwa uhuru juu ya aina ya muungano wanaoutaka, Waziri mkuu wa zamani Dk. Salim Ahmed Salim, (pichani), amesema. “Zanzibar wana madukuduku yao, Tanzania Bara wana madukuduku yao juu ya muungano ni muhimu wakubaliane kikatiba,” alisema Dk. Salim katika mahojiano na NIPASHE yaliyofanyika Kiwengwa, mjini Zanzibar juzi.

  Alisema jambo la msingi kwa sasa ni wananchi kupewa nafasi ya kutafuta ufumbuzi wa dukuduku hizo kwa njia ya mjadala utakaoendeshwa kupitia mchakato wa kuratibu maoni ya wananchi juu ya katiba mpya. Alisema itakuwa ni vizuri kwa vyama vya siasa kujiweka kando ili kuachia wananchi nafasi kubwa zaidi kwa sababu katiba kimsingi inatakiwa iandikwe kwa kuzingatia maoni yao na matakwa yao.


  Dk. Salim alisema sehemu kubwa ya kizazi kilichopo kinaundwa na kizazi kipya hivyo ni vizuri wakapewa nafasi ya kushiriki na kuamua aina ya katiba ambayo wanaamini itakidhi matarajio yao. Akizungumzia mambo ambayo anaamini ni hatari kwa taifa, Dk. Salim alisema ni pamoja kuingiza udini na ukabila katika masuala ya siasa.

  Alionya kwamba wakati Tanzania inaendelea na mchakato wa kuandika katiba mpya, haitakuwa jambo zuri kwa taasisi za nje kuingilia shughuli za upatikaji wa katiba mpya.
  “Watanzania sio roboti, kila mmoja ana akili na fikira zake, muhimu kulinda umoja wetu, na wananchi hasa wa vijijini kupewa nafasi zaidi ya kutoa maoni juu ya katiba yao,” alisema Dk. Salim. Hata hivyo, Dk. Salim alisema hashagazwi na kitendo cha kuingilia mambo ya ndani ya mchakato wa katiba kwa sababu Tanzania ni sehemu ya ulimwengu na haiwezi kujitenga kuwa peke yake.

  Kuhusu miaka 50 ya uhuru, alisema Tanzania imefanikiwa kuwa na katiba yenye misingi mizuri ya viongozi kubadilishana madaraka na hivyo kudumisha amani. Dk. Salim alishauri kuwa itakuwa ni kosa kubwa kwa Watanzania kujaribu kuwa na katiba inayoondoa ukomo wa viongozi kukaa madarakani, kwani jambo hilo linaweza kuipeleka Tanzania kwenye migogoro ya kisiasa.


  Aidha, alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeleta faida kubwa kwa wananchi wake ikiwemo kujenga misingi ya umoja wa kitaifa tangu mwaka 1964. Alisema kwamba jambo la msingi hivi sasa ni wananchi kupewa nafasi ya kujadili kero za muungano na kutoa maoni yatakayosaidia kuimarisha muungano huo.


  Kuhusu sera ya mambo ya nje ya Tanzania, Dk. Salim alisema katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru Tanzania imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha uhusiano wake kimataifa.
  Hata hivyo alisema sifa hiyo haikuja yenyewe bali ilitokana na mabalozi waliokuwa wakiteuliwa kufanyakazi kwa kuweka mbele maslahi ya taifa badala ya maslahi binafsi.Alisema Watanzania wanaopewa nafasi za ubalozi ni vizuri wakafanyakazi kwa kuzingatia uadilifu na kujituma ili kujenga heshima kwa taifa lao. “Huwezi kujifundisha diplomasia kwa kukaa nyumbani na kupiga soga vijiweni, pia uaminifu kwa nchi, jambo la msingi ukiwa nje ya nchi ukipata kashfa hiyo ni kashfa ya nchi yako.” alisema Dk. Salim ambaye ni mwanadiplomasia mkongwe nchini.

  Alisema katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru mataifa mengi barani Afrika na Ulaya yanatambua mafanikio ya Tanzania katika kupingania ukombozi wa Bara la Afrika pamoja na misingi ya haki za binadamu na ubaguzi wa rangi. Hata hivyo, alisema kwamba vyama vya siasa bado vina mchango mkubwa katika kulinda na kutetea misingi ya umoja wa kitaifa katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Mimi binafsi naheshimu sana busara ya Salim Ahmed Salim kutokana na uzoefu wake wa masuala ya uongozi kitaifa na kimataifa. Amesheheni busra ila tu tatizo nabii hakosi heshima ila katika nchi yake mwenyewe.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Askofu Mkuu wa Mwanza Ruwaichi amjia juu Rais Kikwete

  KANISA Katoliki nchini (TEC) limeshitushwa na kutishwa na hatua ya Rais Jakaya Kikwete kusaini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011, harakaharaka kwa kuwa kunaweza kuipeleka nchi pabaya.
  Akizungumza juzi jijini Mwanza na Tanzania Daima muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kilichoandikwa na John Kasembo, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Jude Thadeus Ruwa'ichi, alisema Watanzania wengi walitaka muswada huo usisainiwe, na kwamba mkuu huyo wa nchi alipaswa kusikiliza mawazo ya wananchi wake, na si kuwahi kusaini na kuwa sheria.

  Rais huyo wa TEC alisema kitendo cha serikali kukusanya maoni katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar peke yake, haitoshi kujenga hoja ya kusaini ama kupitisha muswada huo wa Katiba.

  Ruwa'ichi alisema suala la kuundwa kwa Katiba mpya si hiari ya rais wala kundi na tabaka fulani, bali ni la Watanzania wote.

  Rais huyo wa TEC ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza alisema hatua ya kulipeleka suala la Katiba mbindembinde linaweza kuipeleka nchi kubaya na Kanisa Katoliki halitaki Watanzania wafike huko.
  Alisema walitegemea Kikwete angethamini na kujali maoni ya wadau wengine, lakini katika namna ya ajabu hakuonekana kujali chochote.

  Ruwa'ichi ambaye alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa kitabu hicho, alieleza kushangazwa na kitendo cha Bunge kupitisha harakaharaka muswada huo.
  "Hivi Bunge linashughulikia masilahi ya nani? Wabunge wamepewa dhamana na wananchi, hivyo ni lazima wawasikilize wanachotaka, halafu ndicho wakifanyie kazi, na si kuonekana kama ushabiki fulani.

  Alipoulizwa kuhusu suala la udini linaloonekana kutumiwa na baadhi ya wanasiasa nchini, Rais huyo wa Baraza la Maaskofu alikiri kuwapo kwa jinamizi hilo, na kusema ajenda ya udini kwa sasa imekuwa kama kichaka cha watu fulani kuficha maovu yao.
  Alionya kwamba iwapo serikali itaruhusu mijadala ya udini kutawala nchini, basi taifa lipo hatarini kupoteza ustawi wake, na akataka watu wasitumie mgongo wa dini kuficha madhambi yao.
   
 4. K

  KIROJO Senior Member

  #4
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Dk. Salim alishauri kuwa itakuwa ni kosa kubwa kwa Watanzania kujaribu kuwa na katiba inayoondoa ukomo wa viongozi kukaa madarakani, kwani jambo hilo linaweza kuipeleka Tanzania kwenye migogoro ya kisiasa"

  tena ni vema hata chama kikishika madaraka sio kikae mpaka kinaanza kuota magamba mara oooh tuvuane magamba kama Nyoka>10year stop wangie wengine hata kama hawafikisha idadi watujua namna ya kuunda serikali,just 10year eneough.
  hapo heshima itakuepo
  sio mpaka watu wanachakuchua chakachua chakachua aaaaaaa
   
 5. Walikughu

  Walikughu Senior Member

  #5
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tatizo Nchi hii hasa kwa sasa imeisha kuwa na matatizo makubwa hasa ya kiuongozi kila mtu anaona afanye kile anacho ona kinafaa ndiyo maana hawa wazee wanaweza kuonekana kile wanacho shauri ni kibaya si mumeona ndani ya chama tawala wanataka kuwaondoa wazee yaani maraisi wastafuu maana wanaona wanawatinga na mambo yao. Kuhusu mswada au mchakato wa kuaadaa katiba mpya inabidi wananchi washirikishwe kwa kiwango kikubwa baadala ya wanasiasa kutaka kuteka hoja ya katiba mpya, hasa chama tawala kiukweli walikuwa hawajajiandaa na hiyo hoja wameivamia tu ndiyo maana kila jambo watakalo taka kulifanya wanapata upinzani sana
  Mawazo ya mzee Salim Ahmed Salim Yaheshimiwe sana
   
 6. r

  raffiki Senior Member

  #6
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tell them brudaa..!Huyu jamii hana ambo ya mzaa kwenye sehemu nyeti za kazi,ana faa kukaa pale ikulu japo kwa miaka 5 apangilie tena nchi yetu then...tuweke misingi imara ktk katiba yetu kuepuka viongozi wenye kuona nafasi kaika chama na serikali ni genge la watu wa deal kama wanavyojitambua kuwa siku hizi ni kujipanga kwa deal tuu.
   
 7. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #7
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,133
  Likes Received: 1,363
  Trophy Points: 280
  Huwa ninapata taabu sana kuwasikiliza Viongozi waliokuwa mabubu wakati Mwalimu alipokuwa hai on Muungano.
   
 8. A

  Ame JF-Expert Member

  #8
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  Na magamba yalivyo kwa maslahi binafsi hata haya mu-encourage agombee 2015. A man of reputation and wisdom; Salute Mh. Dr. Salimu A. Salimu.
   
 9. T

  Tata JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,535
  Likes Received: 492
  Trophy Points: 180
  I like you comment brother.
   
 10. A

  Ame JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  Mwl naye alikuwa na matatizo yake japo nampenda nakumheshimu baba wa taifa langu; so kwakumheshimu tu ambayo pia ni wisdom usingeona mtu kama Salimu akileta confrotation za bila sababu huku public ikiwa haijawa na hitaji la mabadiliko kama ilivyo sasa.
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  John Malecela alipokuwa waziri mkuu chini ya Rais Mwinyi alijaribu kutaka kuvunja muungano kwa kuunga mkono hoja ya G 55 pale bungeni; kimbunga kilichomkumba toka Butiama hata kuja kukisahau mpaka hapo umauti utakapomfika!! Tsunami ile ndio iliwatia akili wengi wawe mabubu enzi ya MUSSA!!
   
 12. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #12
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,133
  Likes Received: 1,363
  Trophy Points: 280
  Ni Kambona peke yake alikumbwa na tsunami ya Mwalimu, wengine wote walikomaa na siasa mpaka leo wanakula jasho la kukomaa kwao. @ Ame wale walioweza kuona utata wa Muungano wakati Mwanzilishi wake akiwa hai ndio leo wanaweza kutusaidia sio waliokuwa mabubu! - Le Baharia
   
 13. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 160
  kila zama na kitabu chake. ukurasa mpya umefunguliwa ni muhimu kwa watu wazima na wenye uzoefu mkubwa kama hawa wakatoa mwongozo. Huyu jamaa namkubali sana. DU! ila jamaa huyu alipakwa uchafu vibaya 2005. sijui CCM watakubali ushauri wake
   
 14. p

  politiki JF-Expert Member

  #14
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,330
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  salim is not a man of principal anymore kama wengi mnavyodai, he is purely an opportunist. wapi salim a salim wakati maovu makubwa wanayofanyiwa wananchi na yeye amekaa kimya kila siku. wapi kiongozi mahiri atakaa kimya wakati wabunge wanaibia watanzania
  waziwazi kwa kutumia neno posho. nani ameshawahi kusikia salim akitoa au akikemea DOWANS, RICHMOND, EPA na maovu mengine ambayo yanaua uchumi wa nchi yetu. salim a.salim anavizia ili aone kama kuna chance naye achukue urais one day bila kuangalia alama za nyakati kwani viongozi wa aina yake tayari wamepitwa na wakati.
   
 15. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #15
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,133
  Likes Received: 1,363
  Trophy Points: 280
  Politiki SALUTE!
   
 16. r

  raffiki Senior Member

  #16
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Naamu nimekupata mkubwa,napenda hoja kama zako...!umeingia tunduni..sasa ni kweli uliyosema Salm haongelei au mie naita habwatuki kwa mabo uliyosema hayo. Kutokubwatuka kwake haimanishi kuwa sio kiongozi mzuri,nikuulize wewe wapi tumefika au wametufikisha wapi wanaobwatuka kila siku. Salim ni understanding wewe hawezi fanya ujinga huo na sio class yake hiyo...ndio maana kila siku mnasema mara ooh siasa utwara nara oh siasa ovyooovyooo mara oohh siasa uhasiii..sasa ulitaka mtu kama Salim aliye organised na smart aingie humu kwenye huo mkumbo wa hizo siasa zenu.Shame on u...ndio maana nasema na wengi wanataani Salim to be our next top leader asafinyee wazandiki nyiee...kila siku kuongelea mambo kama unayosema bila kutekeleza kwa vitendo.
   
 17. A

  Ame JF-Expert Member

  #17
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  Wengine wanafikiri kupiga kelele ndiyo uzalendo. Je nilini ameunga mkono kuwa DOWANS lazima ilipwe? Salimu anajua maana ya negotiation hasa akijua ame invest vipi kwenye hicho chama ambacho kime bakwa na mafisadi.
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Tofauti ya utanda wazi wa enzi hizo na leo ni mkubwa sana. Leo hatuhitaji kupanda jukwaani kupingana na Kikwete kwa kuwa nafasi hiyo hatuna na analindwa vilivyo na dola, kama ukijaribu utakutana na rungu la dola ilayomlinda.

  Lakini leo tuna majukwaa mengi na ya aina nyingi ambayo hata wewe unathubutu kutoa hoja, hii ni kutokana na wakati wa zama hizo kufikiwa ukingo na hizi ni enzi za kizazi kingine chenye kujengeka kwa mfumo wa teknolojia ya kizazi kipya ambayo huwawia vigumu viongozi na dola kushinikiza. Njia za panya ziko kila kona kizazi kipya kinapenya kila kona, ni ushauri wa kufaa wazee kufuata mkondo wa fikra za kizazi kipya zi kile zha zidumu fikra.

  Salim kapitia mengi na kukutana na wengi wa kimataifa, hivyo mwono wake ni mpana ambao kwa mtazamo wake na hoja aliyotoa kwa wanamagamba watamwona kama msaliti kumbe ni mtaifa mwenye hoja ya kujenga utaifa zaidi kuliko mfumo wa magamba unaojengeka kitabaka.
   
 19. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #19
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,043
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Huwa naheshimu sana mawazo na weledi wa huyu Mzee.Ni bahati mbaya sana wajanja walimchafua vilivyo mwaka 2005.Hii nchi ina watu hatari sana kwa kuchafua wenzao kwa sababu ya pepo ya magogoni!Nina hakika angeipata ile fursa mwaka ule sasa hivi hii nchi ingekuwa mbali zaidi ya hapa ilipo.Huo ndio ukweli hata kama wengine hawataupenda.
   
 20. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #20
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,133
  Likes Received: 1,363
  Trophy Points: 280
  Candid kuna siku utakuja kuyafahamu vizuri na utayajutia sana haya maneno, maneno yako yanaonyesha kuwa humfahamu sana unayempigania. HOWEVER ngoja niishie na huu mjadala.
   
Loading...