Sales team kwa ajili ya mauzo ya efd machines

potokaz

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
530
486
Wanahitajika vijana wa kuelimisha matumizi ya EFD kwa wafanyabiashara wenye TIN number pamoja na kuwahamasisha kununua mashine hizo kama ambavyo imeelekezwa na Serikali kupitia TRA.

Kwa kuwa zoezi la kuwaunganisha wafanyabiashara na mfumo huu ni endelevu na tayari Serikali imekwishaanza ukaguzi wa kuhakiki wafanyabiashara ambao hawajaaanza ktumia mashine za EFD, tukiwa kama kampuni iliyoidhinishwa na TRA ni jukumu letu kuhakikisha wafanyabiashara wananunua mashine hizi na kuanza kuzitumia kwa mujibu wa sheria.

Malipo ni kwa Commission, utalipwa kadiri unavyofanikiwa kuwaunganisha wafanyabiasha na mfumo wa matumizi ya EFD. Yaani kiwango fulani kwa kila mteja atakayenunua mashine ya EFD, watakaochaguliwa wataelezwa kiwango hicho na kupewa training.

Sifa

Elimu ya kidata cha NNE au Kidato cha SITA na umri kuanzia miaka 20.

Only for serious applicants.
Tuma maombi/CV na namba ya simu kwa e mail hii: etrsolutions@yahoo.com
Eleza ungependa kufanya mkoa gani kati ya Dar Es Salaam, Mwanza au Arusha.

Deadline 27/11/2014
 
Asante kwa taarifa. Nisaidie majibu ya maswali yafuatayo: 1.Je Mtu anaweza kutuma CV tu, barua au aweza tuma vyote(CV NA BARUA YA MAOMBI) kwa pamoja? 2. Hiyo ni kazi au kibarua? Na je kuna haki gani zingine mbali na commisions? 3. Recruitment course itachukuwa mda gani? Na itafanyikia wapi? 4. Je hiyo kazi au kibarua itakua ya mda mfupi au mda wote.
 
mbona nishaapply mda sana na leo mwatangaza tena au ndo nimeonekana siko serious???
 
Asante kwa taarifa. Nisaidie majibu ya maswali yafuatayo: 1.Je Mtu anaweza kutuma CV tu, barua au aweza tuma vyote(CV NA BARUA YA MAOMBI) kwa pamoja? 2. Hiyo ni kazi au kibarua? Na je kuna haki gani zingine mbali na commisions? 3. Recruitment course itachukuwa mda gani? Na itafanyikia wapi? 4. Je hiyo kazi au kibarua itakua ya mda mfupi au mda wote.

Ndugu Sokoro tuwasiliane kwa e mail hapo juu, maswali yako yatajibiwa huko
 
Back
Top Bottom