Salary ya november kutoka december

Mr Mayunga

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
313
40
Habar za asubuhi wana jamii,huku kwetu si salama!halmashauri yatu haijatuma pesa mpaka jana,maana yake inaweza ikatoka dec.Sijui kunatatizo gani,mazingira ya kufanyia kazi yenyewe ni magumu sanai.e.udini,ukabila,usisi vimetawala ,kazi yenyewe ni ngumu ila chakushangaza hela hazitoki kwa wakati.Lakini pia,hata pesa ikitoka benk ipo 30km hapa nilipo.Jaman,mnadhani kazi itafanyika kwa moyo mmoja,sijui!
hapa kwetu hali iko hivyo.
 
Pole sana , lakini nakushauri uwe unafuatilia historia ya mwenendo wa matukio mbalimbali hapa nchini. Unasahau kuwa mwezi wa 11 tulikuwa na Mkutano mkuu kule Dodoma? Sasa pesa za kuwalipa mshahara harakaharaka namna hiyo unadhani watazitoa wapi?
 
kwani safari za Kinana na team yake zimeisha??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Bila shaka utaratibu umebadilika sasa mshahara tarehe 1 mpaka 1
 
Pole sana ila kwenye mazingira magumu i.e udini,ukabila,usisi hapo umeniacha hoi!
 
wazo zuri ila hebu jaribu kufikiri mazingira aliyonayo kiasi kwamba leo december mosi na tayari anaongelea mshahara; tambua kuwa malipo kama alivyosema hayawezeshi miezi kukutana; hata mtaji kweli ni issue ingawa wazo la mradi pia lulu;

kuna haja ya kutazama upya malipo ya watumishi wa umma!
 
Kwa kipindi kirefu watu wa kada mbali mbali wamekuwa wakizungumzia Kufulia kwa Serikali ya CCM kuanzia Serikali kuu mpaka Serikali za mitaa.

Hata hapa JF watumishi katika wizara na taasisi wamewahi kuripoti hili Lakini kwa bahati mbaya wahusika wamekuwa wakikana hili. sasa

Kama serikali wanashindwa kutimiza wajibu wa msingi wa kuwalipa watumishi wake kwa muda muafaka unatarajia ufanisi kweli?

Ukienda kwenye mbao za matangazo utakutana na Matangazo kama haya:

Wadau hii ndiyo hali halisi wakati wanaangaika kuzunguka kusikiliza wananchi watendaji wanakufa njaa.

attachment.php


Naomba kuwasilisha
 

Attachments

  • IMAG0048.jpg
    IMAG0048.jpg
    71.3 KB · Views: 159
Kaka hiyo ni danganya TOTO pesa imetumika kwa kazi zingine na hao jamaa wameagizwa tu kufanya hivyo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom