Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Dumelang

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
3,194
5,598
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametaja mshahara wake kuwa ni Tsh mil 9.5, huku akiahidi atatoa Salary slip zake punde akitoka mapumzikoni Chato.

Hiyo imetokea wakati wa kipindi cha magazeti leo tarehe 01/04/2016 ambapo watangazaji walisoma habari iliyoandikwa na gazeti la nipashe kuwa Zitto na Lissu waomba ataje Mshahara wake na ukatwe kodi.

Wakiwa katika mjadala huo, walipokea taarifa kuwa Rais kawasikia na katuma taarifa ofisi za Clouds kujuza mshahara wake kuwa ni mil 9.5 na atatoa stakabadhi zake akirudi Dar.

Chanzo: Clouds 360 Asubuhi hii

==========
Kutoka Gazeti la Mwananchi:

Meneja wa kipindi cha 360 ambacho hufanya uchambuzi wa magazeti, Hudson Kamoga aliithibitishia Mwananchi kuwa Rais Magufuli alimpigia simu kumtajia mshahara wake.

Huo ndiyo mshahara ambao mkuu wa nchi ameutangaza kwa umma bila ya kutoa ufafanuzi kama unajumuisha marupurupu mengine kulingana na cheo chake.

Rais ameamua kuweka hadharani masilahi yake wakati kukiwa na mjadala mkubwa uliotokana na tamko lake alilolitoa mapema wiki hii kuwa atapunguza mishahara ya watendaji wakuu wa taasisi na mashirika ya umma kutoka Sh40 milioni hadi Sh15 milioni, akisema katika “Serikali ya Magufuli”, ambayo itadumu kwa miaka 10 iwapo atachaguliwa tena mwaka 2020, hakuna mtu atakayelipwa zaidi ya kiwango hicho.

Dk Magufuli, ambaye hivi sasa yuko nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko aliamua kutangaza mshahara wake baada ya wabunge wawili, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) na Tundu Lissu (Chadema) kuripotiwa kutaka atangaze mshahara wake baada ya tamko la kupunguza mishahara ya vigogo wa mashirika hayo ya umma.

Wakati wa kipindi cha asubuhi cha 360 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds, watangazaji walisoma habari hiyo na kuanza kujadili mshahara wa Rais.

Wakati wakijadili ndipo Rais alipowapigia simu kuwatajia mshahara wake.

Meneja wa kipindi cha 360 ambacho hufanya uchambuzi wa magazeti, Hudson Kamoga aliithibitishia Mwananchi kuwa Rais Magufuli alimpigia simu kumtajia mshahara wake.

“Aliniuliza kwa nini sikuwapo kwenye kipindi, nikamjibu kuwa nipo Arusha kwa majukumu mengine,” alisema Kamoga.

“Akaniambia niwaambie wenzangu ambao wapo kwenye kipindi kuwa mshahara wake wa mwezi ni Sh9.5 milioni na mshahara huo ameukuta na kwamba akirudi Dar es Salaam, twende ofisini kwake akatuonyeshe salary slip.”

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa alisema Ikulu hakuna mtu anayelipwa zaidi ya Sh9.5 milioni.

“Kwa hiyo kama Rais ameamua kuzungumza nao (Clouds) kuhusu mshahara wake, naomba asubiriwe akirudi Dar es Salaam akawaonyeshe salary slip yake kama atafikia hatua hiyo,” alisema Msigwa. Lakini uamuzi wake wa Rais kutangaza mshahara wake, umekosolewa na Lissu.

“Mshahara alioutangaza Rais unaendelea kuwaweka wananchi njiapanda kwa kuwa hauna uchanganuzi,” alisema Lissu alipoulizwa maoni yake kuhusu kiwango cha mshahara wa mkuu wa nchi.

“Anapaswa kueleza iwapo ni fedha ya jumla, marupurupu yapo humo ndani kwa sababu mshahara wa mbunge ni Sh3.6 milioni na anapohesabiwa marupurupu yake inafikia kiasi cha Sh12 milioni na hizi ndizo anazoondoka nazo.

“Sasa tunahitaji kujua kama ndiyo fedha anayokwenda nayo nyumbani au ni vinginevyo.”

Kabla ya Dk Magufuli kufanya hivyo, kumekuwa na mjadala kwa muda mrefu kuhusu mshahara wa Rais, na kila vyombo vya habari vilipojaribu kutaja, Ikulu ilikanusha mara moja lakini haikutoa ufafanuzi wa kiwango sahihi cha mshahara.

Mtandao wa African Review mwaka jana ulifanya uchambuzi wa mishahara ya marais Afrika na uliwataja marais watano wanaoongoza kwa kuwa na mishahara mikubwa kwa mwaka kuwa ni Paul Biya wa Cameroon anayelipwa dola 610,000 za Marekani, akifuatiwa na kiongozi wa Morocco, Mfalme Mohammed VI (dola 480,000) na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini (dola 272,000).

Katika orodha hiyo, Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete alishika nafasi ya nne akitajwa kupata dola 192,000 na wa tano alikuwa Rais Abdel Aziz Bouteflika wa Algeria, anayelipwa Dola 168,000.

Madhumuni ya utafiti wa mtandao huo yalikuwa ni kuangalia kiasi wanacholipwa marais wa Afrika kwa mwaka na kile inachopata taifa husika kwa muda huo.

Pia walilenga kuangalia uhusiano wa viongozi na wananchi wa kawaida wanaowangoza.

Kwa mujibu wa mtandao huo, vyanzo vya taarifa za mishahara ya marais hao vilipatikana kutoka mitandao na wanahabari wa nchi husika. Habari hizo ziliporipotiwa, Ikulu ilikuja juu lakini haikutaja mshahara halisi wa Rais.
 
Rais Dk john pombe magufuli ametaja mshahara wake kuwa ni Tsh mil 9.5, huku akiahd atatoa Salary slip zake punde akitoka mapumzikoni Chato.

Hiyo umetokea wakati wa kipindi cha magazeti leo tarehe 1/04/2016 ambapo watangazaji walisoma habari iliyoandikwa na nipashe gazeti kuwa Zito na Lissu waomba ataje Mshahara wake.

Wakiwa katika mjadara huo, walipokea taarifa kuwa Rais kawaskia na katuma taarifa clouds office kujuza mshahara wake kuwa ni mil 9 plus na atatoa stakabadhi zake akirudi Dar.

Source Clouds 360 Asubhi hii.

Aya sawa!!!
Raisi analipwa kidogo kuliko wakurugenzi wa mashirika ya umma sawaa!!
Ila katika kubana matumizi kama vipi adake milioni mbili tu;););)

Happy fools day
 
Hivi zito na lisu huwa swaelewa na wao wanalialia kimoyoyo hakuna posho za kijinga wameanza kujiuzuru,hawa jamaa hawataki kusema ukweli kwa watanzania kuwa jaman maisha yamebadilika siku hiz fedha hakuna wanaanza kumshambulia rais et taja mshahara.kuna baadhi ya wanasiasa nishaachaga kuwasikila kwasababu niwanafiki ni baraa wakibanwa wanaongea vingne kufikisha ujumbe nawaomba watulie sindano ziingie vizuri.
 
Hiyo habari ni ya ukweli haina uhusiano na siku yenu ya wajinga.

Ila milioni 9 ni nyingi sana kwa sababu hanunui chakula ulinzi,maji,umeme,usafiri,matibabu,mavazi yote anapewa bure.

Awe anapata laki 8 tu zinamtosha za kuwatumia ndugu zake chato wakimuomba ela.
 
Baada ya watu kutaka kujua yeye anapokea sh.ngapi awapigia simu clouds tv na kujibu swali hilo kuwa yeye anapokea sh.9.500.000 kwa mwezi na akimaliza likizo atatoa ufafanuzi wote

Source clouds Tv
 
Jamani hiyo habari ni ya kweli sio sikukuu ya wajinga iliyopo kwenye TV acheki sasa hivi clouds tv
 
Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema mshahara wake ambao yeye ameukuta na ambao analipwa ni Milioni 9 na laki 5.

Rais Dkt.Magufuli amelazimika kuyasema hayo wakati wa uchambuzi wa magazeti katika kipindi cha Clouds360.

Akizungumza na mtangazaji wa kipindi hicho Hudson Kamoga ameahidi akirudi kutoka likizo yupo tayari kuonyesha nyaraka za malipo ya mshahara wake.

Baada ya kusema mshahara wa juu uwe angalau Milioni 15 kumbe yeye hata Milioni 10 hajafikisha
 
Leo wakati nasikiliza Kunani Tanzania Magazetini Clouds TV kipindi, Gazeti la Nipashe nileandika taarifa kuhusu Zitto na Tundu Lissu kumtaka Raisi Magufuli kutaja mshahara wake ili wajue kiasi cha kodi anacholipa!
Haikuchukua muda, taarifa ya Breaking News ikasomwa na Mtangazaji Baby kuwa, Mh. Rais kapiga simu na kuwatajia kiwango cha mshahara wake na kuwa atakapotoka rikizo fupi aliyonayo atawaletea risiti ya mshahara wake! Mh. Rais ametaja kuwa Mshahara wake ni Milioni tisa na Laki tano (Tsh. 9,500,000/-)

Chanzo: Clouds TV, Kunani magazetini!
 
huu uzamwamwa unasemaje mambo ya kitaifa kwenye private media nyeti kama hayo ila kumbukeni leo 1/4
 
Back
Top Bottom