Salary Advance: Janga linalowatafuna Watumishi wa Umma

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,256
2,000
Kuna hiki kitu kinaitwa 'Salary Advance' ambapo mabenki yanawakopesha Watumishi wa Umma online kupitia akaunti zao za mishahara yao!

Nimeona NMB, CRDB wanayo hii huduma.

Unaweza kukopa mpaka 40% ya take home ya mishahara yao. Ni lazima uwe umejiunga na SIM Banking au NMB Mobile, kwani unatumia simu kuuchota huo mkopo.

Kwahiyo mtu akishapata mshahara wake, hapohapo anavuta huo mkopo. Mshahara wake unapoingia wanakata fasta juu kwa juu. Akipokea, anaomba tena siku hiyohiyo.

Nimeona Watumishi wengi wa serikali wanaitumia sana hii huduma. Imeshawaharibu kabisa Watumishi wa Umma.

Shida sana nchi hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom